2024.03.09 Kuwekwa wakfu wa kiaskofu, wa Askofu Vincenzo Turturro , Balozi wa Vatican nchini Paraguay. 2024.03.09 Kuwekwa wakfu wa kiaskofu, wa Askofu Vincenzo Turturro , Balozi wa Vatican nchini Paraguay.  (Vatican Media)

Balozi wa Paraguay Turturro amewekwa wakfu na Kard.Parolin

Monsinyo Turturro aliyeteuliwa na Papa mwezi Desemba 2023 kuwa Balozi wa Vatican huko Paraguay amepewa daraja la Uaskofu.Tangu 2019 alikuwa ni katibu binafsi wa Kardinali Parolin.Katika misa washiriki elfu moja walikuwepo pamoja na Papa.Katika mahubiri Kardinali Parolin ameonesha hatua za wito na kumshauri nyayo za Askofu Tonino Bello.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican Jumamosi tarehe 9 Machi 2024 liliwaona waamini elfu moja, wanafamilia, mapadre, maaskofu, makadinali, kama ishara ya upendo na heshima kwa mtu ambaye alitenda wema, unyenyekevu na wa kiroho wa huduma kuwa alama ya kazi yake.  Ni katika maadhimisho ya Misa Takatifu ya  kuwekwa daraja la Uaskofu  kwa Monsinyo Vincenzo Turturro, mwenye umri wa miaka 45, kuhani wa Puglia nchini Italia na tangu 2019, amekuwa katibu binafsi wa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican na ambaye aliteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko mnamo mwezi Desemba 2023, kuwa  Balozi wa kitume nchini Paraguay.  Hadi uteuzi wake alikuwa na wadhifa wa kuwa Mshauri wa Ubalozi kwa hiyo aliinuliwa hadhi ya Uaskofu mkuu.

Kwa miaka mingi katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican

Sherehe ilikuwa na  utulivu katika Madhabahu ya Kiti kitakatifu licha ya ushiriki wake mkubwa wa waamini na pia Baba Mtakatifu Francisko  alikuwepo ambaye mara baada ya kufika mapema na  kiti cha magurudumu, alipokelewa kwa makofi na kusalimiana na baadhi ya watoto.  Maadhimisho na kutoa wakfu wa kiaskofu ulitolewa na Kardinali Parolin. Akizungumza kuhusu wasifu wake alitoa maneno ya sifa na kutia moyo kwa mshiriki wake, ambaye sasa anaitwa kumwakilisha Papa katika nchi ya Amerika ya Kusini ambako uwepo wa Wakatoliki unafikia karibu asilimia 90 ya watu wote. Hata hivyo safari ya  Amerika ya Kusini kwa  Mteule Balozi Turturro, siyo ya mara ya kwanza kwani kwa miaka mingi alitumikia Ubalozi wa Vatican nchini Argentina, na hata kabla  yaani tangu kuingia kwake katika Huduma ya Kidiplomasia ya Vatican  mwaka 2009  aliwahi kwenda nchini Zimbabwe na Nicaragua! Katika miaka ya hivi karibuni alihamishiwa katika Kitengo cha Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa ya Sekretarieti ya Vatican kwa takriban miaka mitano alikuwa akifuatilia kwa karibu sana kazi ya Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin.

Balozi maana yake ni mjumbe

Kardinali Parolin akianza mahubiri yake, alionesha shughuli na mtindo wa Monsinyo Turturro ambazo anatakiwa kuwa nazo, awali ni busara, shauku na  uzoefu. Na baadaye akielezea nini maana ya Balozi, alisema awali ni mjumbe na kila ujumbe una sifa ya kivumishi cha kitume ili kusisitiza ukweli kwamba huduma hii ni suala la mambo ya kufanya au kutofanya, kusema au kutosema, lakini ni utume wa kuishi, maisha ya kutumia kwa ajili ya Kanisa na kwa ajili ya nchi ambayo mtu anajikuta ndani yake. Katika nchi hizio huwezi kamwe kuwa mgeni, si kwa sababu tu ya uwepo wa wazi wa Wakatoliki lakini zaidi ya yote kwa sababu watu, kama kila watu, wanaishi na kupendwa na Mungu ambaye sasa anamtuma.

Papa Francisko alikuwa kwenye misa ya kuwekwa wakfu
Papa Francisko alikuwa kwenye misa ya kuwekwa wakfu

Na huko Paraguay, ambapo mjumbe mpya ataondoka hivi karibuni, hakika atafanya kwa mtindo wake mwenyewe: kuingia kwenye ukweli ambao anajua unatangulia na kuzidi kwa shauku inayoonyesha umri wake na uzoefu katika huduma ya Vatican. Kardinali Parolin aliongeza kuwa, atafanya hivyo pia, anajua kwamba anajali hasa, kutunza historia ya neema ambayo Bwana amempatia, kupitia mizizi ya familia na ya Jimbo la Molfetta-Ruvo- Giovinazzo-Terlizzi ambao kwa siku hiyo walikuwepo na wakimkumbatia kwa nguvu.

Maneno ya Don Tonino

Kardinali pia alikumbusha kwamba, kwa kuzungumzia jimbo la Molfetta, siyo rahisi kutomtaja aliyekuwa mchungaji wake asiyeweza kusahaulika, Don Tonino Bello(Askofu): Kardinali Parolin alisema: “Inapendeza sana askofu ambaye aliongozana na hatua za kwanza za wito wako na miaka ya kwanza ya seminari.” Katika hiyo amependa kutumia maneno Mtumishi wa Mungu ili yawe nguzo ya  Monsinyo Turturro kwa ajili ya huduma yake mpya. Kwanza kabisa wakati huu wa Kwaresima ambao unatangulia Pasaka: Don Tonino alipenda kuuona kama “safari yenye changamoto kwa ujumla ya mtu, safari inayotoka kichwani hadi miguuni. Kutoka katika majivu yaliyowekwa juu ya kichwa hadi kuosha miguu siku ya Alhamisi Kuu. Kutoka kichwani hadi vidole kukumbatia utu wetu wote, kushinda kila umbali na Bwana”.

Wakati wa kusali Litania
Wakati wa kusali Litania

Kardinali Parolin aidha alisema jambo la pili, ni mavazi na usemi maarufu wa Kanisa la aproni ambapo Don Bello alibainisha  kwamba kati ya zawadi nyingi ambazo zinapendezesha mavazi ya kuwekwa wakfu inakosekana mara nyingi aproni, mojawapo ya mavazi ya kikuhani, iliyokumbushwa na Injili. Hata hivyo, inakosekana kwa sababu haiachi kamwe, kwa sababu inapaswa kuvaliwa kimazoea na kutoondolewa, kwa kufuata mfano wa Yesu ambaye aliamka na kuchukua nguo, lakini hakuweka kitambaa cha kufuta chini.

Wakati wa kuvalishw Mitra
Wakati wa kuvalishw Mitra

Na bidii hii ya kutumikia, kwa Monsinyo Vincenzo, iwe ndiyo roho ya huduma yake, alisisitiza Kardinali Parolin. Na Hatimaye, mahali, katika kesi hii  kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, ambapo, Kardinali aliwahakikishia, Roho Mtakatifu yuko karibu kushuka juu yao: awajaze na neema yake na kuwafanya kuwa na furaha na moyo mwepesi wa kutumikia akina dada na kaka waliokabidhiwa mikononi mwao katika uchungaji wao kwa sababu wao ndio makanisa anamokaa Bwana wao na wetu.

Ukaribu wa mchungaji mwema

Kardinali Parolin akijikita kufafanua juu ya fimboya kichunaha ya kiaskofu alifafanya juu ya ukaribu na umuhimu wa kuwa mchungaji mwema. Hii ndiyo siri ya kukabiliana na changamoto za huduma ya mrithi wa mitume, ambayo kabla yake ni halali na ni muhimu kujisikia kuwa hatujajiandaa.  Kardinali Parolim alisema: “Mpendwa Monsinyo Vincenzo, ni shauku ya kujikabidhi kwa Bwana ndiyo inayokutegemeza wakati huu, kwa kubaki ndani ya Yesu uliweza kukubali mwaliko wa kwenda. Kwa kukaa ndani Yake unasukumwa kwenda na itakuwa hivi kwako kama mjumbe."

Kukumbatiana na Papa Francisko

Na mara baada ya upako wa mafuta ya Crisma na utoaji wa Injili, pete, pallium, kofia na fimbo ya kichungaji, makofi ya nguvu yaliyodumu kwa muda mrefu. Askofu Mteule Turturro, alionekana kujisogeza, akitabasamu kwa kila mtu aliyekuwepo na kisha akapokea kumbatio kutoka kwa Kardinali Parolin na Askofu Mkuu  Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican  wa Mahusiano na Mataifa, na Mashirika ya Kimataifa na baadaye akaelekea  kwa Papa Francisko ambaye  pia alimshika mikononi mwake kwa muda mfupi mwakilishi wake mpya kwa ajili ya Nchi ya Paraguay.

Barua ya Askofu kijana

Mwishoni mwa sherehe, kulikuwa na maneno mafupi ya Askofu Mkuu Turturro ambaye, kwa hisia, alitaka kukabidhi mawazo yake kwa njia ya barua iliyotumwa kwa usahihi kutoka katika Basilica hiyo  kwenda katika  Kanisa atakalokwenda huko Paraguay. Anayekuandikia kwa mkono unaotetemeka ni askofu kijana ambaye kwa neema ya Mungu na ubunifu wa mama Kanisa ananituma  kama balozi. Ninajionesha kwa ukweli na umuhimu wa kijana kwa maandishi ninaendelea kurudia mimi ni kijana tu, sijui nifanye nini...". Balozi huyo kwa njia hiyo alifuatilia kwa ufupi maisha yake akionesha njia tofauti alizopitia kuanza na  familia, kazi, imani katika Mungu Mpaji , uzuri wa Jimbo lake na maaskofu aliokutana nao. Maisha ambayo yana mizizi yake katika ardhi ngumu na yenye harufu nzuri ambayo nilikuwa mzaliwa wa Puglia, ambayo kama mzeituni mkarimu hauogopi kutoa matunda yake kwa Kanisa” aliongeza.

Askofu Mkuu Turturro akisoma barua yake
Askofu Mkuu Turturro akisoma barua yake

Wema wenye huruma wa Baba Mtakatifu Francisko, mikono yenye subira ya Kardinali Pietro, moyo shupavu wa wakuu na ndugu wa Sekretarieti ya Vatican unipeleke kwenu, wapendwa kanisa la Paraguay. Sijui utajiri mwingi unaowapamba, lakini Tayari ninahisi ninakupenda ...", aliendelea Askofu Mkuu Turturro. Na aliomba na kuomba sala ili apate kutoka kwa Mwenyezi Mungu unyenyekevu wa moyo unaomng'oa mtu kutoka mahali pa heshima na kushinda hamu ya kukaa nyuma ya pazia. Bwana awape moyo wangu wenye kusitasita na mikono yangu isiyo na uzoefu, unyenyekevu wa kusimama karibu: kwa vijana, kwa familia, kwa wafanyakazi wasio na utulivu, kwa wachungaji kwa upendo na Injili, kwa wagonjwa. Kwa kila mtu nina hamu isiyozuilika ya kupiga kelele: Bwana yu pamoja nawe, nina hakika naye. Bwana kamwe hatutupi.” Alihitimisha.

Baada ya misa takatifu
Baada ya misa takatifu
Kukwekwa wakfu wa kiaskofu kwa Balozi wa Vatican nchini Paraguay
09 March 2024, 16:03