Maaskofu wa Marche:Papa yuko karibu na matatizo halisi ya maisha yetu!
Vatican News
Maneno ya dhati, ya ukweli, ya moja kwa moja, kutoka kwa mtu aliye karibu na shida halisi za maisha yetu ndivyo alisema Askofu Nazzareno Marconi, rais wa Baraza la Maaskofu wa Marche, kwa waandishi wa Vatican News katika mazungumzo ya tarehe 11 Machi 2024 mara baada ya kukutana na Baba Mtakatifu wakiwa katika ziara ya Kitume (Visita ad Limina). Takriban saa mbili za mazungumzo hasa ya upole ambapo Papa, aliuliza kila mtu kujitambulisha na kuorodhesha changamoto na matatizo ya majimbo yao binafsi.”
Papa kuonesha mshakamani na hali za majimbo
Kwa mujibu wa Askofu Marconi alibainisha kuwa, Papa hasa alionesha mshikamano kwa hali ambayo majimbo yetu yanapitia kutokana na tetemeko la ardhi, mafuriko ... Hali zilizozidi wakati wa Uviko 19 na kwamba sehemu nzuri ya mazungumzo ililenga “changamoto za kichungaji za wakati huu wa mabadiliko makubwa, hasa ukaribu wa familia na vijana na ugumu wa kusambaza imani kati ya vizazi.” Maneno pia alisisitiza katika taarifa iliyotolewa baada ya kusikilizwa na Baraza la Maaskofu wa Marche kuwa “Papa Francisko alijibu maswali, kuhimiza njia ya pamoja ya Makanisa ya Marche, kuonesha mshikamano na matatizo yetu, hasa nyenzo tata na zaidi ya yote ujenzi wa kijamii baada ya tetemeko la ardhi, janga na mafuriko. Papa, alithibitisha maaskofu katika ufahamu wao wa kazi ngumu ya kulivusha Kanisa la mkoa wa Marche kutoka katika mapokeo ya zamani na imani iliyopatikana zaidi ya yote katika parokia ndogo hadi siku zijazo tofauti.”