Tafuta

2024.03.16 Papa amekutana na Jumuiya ya Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesu' 2024.03.16 Papa amekutana na Jumuiya ya Hospitali ya Kipapa ya Bambino Gesu'  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa akutana na Jumuiya ya Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesu'

Papa Francisko akikutana na jumuiya ya Hospitali ya Watoto ya Kipapa katika Ukumbi wa Paulo VI Vatican,amesisitiza juu ya huduma itolewayo na wahudumu kwamba nguvu yao ya kujitoa ni upendo na hakuna kazi nyingine zaidi ya utume.Hotuba ilisomwa na Mons.Ciampanelli:ninapokuja “Bambino Gesù” Nina hisia mbili zinazopingana:Ninahisi uchungu kwa mateso ya watoto wagonjwa na wazazi wao na ninahisi matumaini"

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ilikuwa ni isahara nzuri iliyomwona Baba Mtakatifu Francisko akiwakumbatia wafanyakazi wa maeneo 6 ya vitengo vya Hospitali ya Kipapa ya  Watoto ya Bambino Gesù ambayo kwa hakika imejaa historia na mustakabali, unaofungamana pia na hatua za kutia moyo za utafiti.  Madaktari, wauguzi, watafiti, wafanyakazi wa utawala, wagonjwa na familia, walisikiliza maneno ya Baba Mtakatifu  Franciko kwa makini katika Ukumbi wa Paulo VI, Jumamosi tarehe 16 Machi 2024. Hata hivyo kabla ya hotuba, kulikuwa kumepangwa safu 6 za mbele, zenye tabasamu zaidi ya watoto 200 ambapo wakiwemo watoto wageni wachanga kutoka  mbali ya dunia  ambapo hawangekuwa na uwezekano wa matunzo au usaidizi, na zaidi ya yote kutoka katika mazingira yenye vita kama vile Ukraine na Gaza.

Papa na Jumuiya ya Hospitali ya Kipapa
Papa na Jumuiya ya Hospitali ya Kipapa

Tukio la fursa ya kukutana huku ilikuwa ni kufanya kumbukumbu ya miaka 100 tangu familia ya Salviati ilipotoa msaada wa hospitali hiyo kwa Papa Pio XI. Kuanzia siku hiyo, mnamo tarehe 20  Februari 1924, Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù, hospitali ya kwanza ya Kiitaliano iliyowekwa kwa ajili ya watoto, ikawa kwa kila mtu “Hospitali ya Papa”. Baba Mtakatifu Francisko alipowasili katika Ukumbi wa Paul VI, kikundi cha watoto kilifunua bendera yenye kauli mbiu “Maisha yasaidiayo maisha,” maneno ambayo pia yanaambatana na mipango mbalimbali iliyopangwa kwa 2024. Baadhi ya wagonjwa pia walimkabidhi Baba Mtakatifu kikapu chenye mawazo yaliyoandikwa kwa ajili yake na watoto na vijana waliolazwa katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù. Papa Francis ili asichoke, alimwomba Monsinyo Filippo Ciampanelli, wa Sekretarieti ya Vatican  kusoma hotuba yake. Katika hotuba hiyo Baba Mtakatifu alianza kuonesha furaha sana kukutana nao wakati wakikukumbuka  mia moja ya kuanzishwa kwa Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù,  Karne moja iliyopita, ilitolewa kwa ajili ya Vatican  na familia ya Salviati. Kwa hakika ilikuwa ni  hospitali halisi ya kwanza inayotolewa kwa ajili ya  watoto. Zawadi iliyokubaliwa na Papa Pio XI. Kwa njia hiyo Papa amependa kujikita kidogo kutafakari, kwa shukrani, juu ya utajiri wa taasisi hiyo, ambayo imeendelea zaidi ya karne ya historia, kwa kusisitiza mambo matatu: zawadi, huduma na jumuiya.

Jumuiya ya Hospitali ya Kipapa imekutana na Papa
Jumuiya ya Hospitali ya Kipapa imekutana na Papa

Baba Mtakatifu akianza kutafakari kipengele cha kwanza zawadi alisema “ Leo Bambino Gesù ni mojawapo ya vituo vikubwa zaidi vya utafiti na matibabu ya watoto barani Ulaya, mahali pa kukumbukwa kwa familia zinazotoka ulimwenguni kote. Walakini, kipengele cha zawadi kinabaki kuwa cha msingi katika historia na wito wake, pamoja na maadili ya bure, ukarimu, kupatikana na unyenyekevu. Katika suala hili, ni vizuri kukumbuka ishara ya watoto wa Arabella Salviati ambao, mwanzoni mwa historia yao, walimpatia mama yao benki ya nguruwe ili kujenga hospitali ya watoto. Hii  inatueleza kwamba kazi hii kubwa pia inategemea juu ya zawadi za unyenyekevu, kama ile ya watoto hao kwa faida ya wenzao wagonjwa. Na kwa mtazamo huo huo, ni vizuri, katika wakati wetu, kutaja ukarimu wa wafadhili wengi shukrani ambao iliwezekana kuunda Kituo cha Huduma Shufaa (Palliative care) huko Passoscuro kwa wagonjwa wadogo sana wanaosumbuliwa na magonjwa yasiyoweza kupona.

Watoto walimwona asaini
Watoto walimwona asaini

Ni kwa nuru hii tu tunaweza kuelewa kikamilifu thamani ya kile wanachofanya, kutoka katika vitu vidogo hadi vikubwa, na wanaweza kuendelea na ndoto kwa siku zijazo.  Aidha hebu tufikirie, kwa mfano, juu ya matarajio ya makao makuu mapya jijini Roma, ambapo majengo yamewekwa hivi karibuni, kwa makubaliano kati ya Vatican  na Serikali  ya Italia. Pamoja na dhamira muhimu ya kiuchumi ya kawaida na isiyo ya kawaida inayohusishwa na ulinzi na matengenezo ya miundo na vifaa; kuhakikisha ubora wa kitaaluma wa madaktari na waendeshaji; kwa utafiti wa kisayansi; hadi kufikia hatua ya kukaribisha watoto wenye uhitaji kutoka duniani kote, wanayoitoa bila kutofautisha hali ya kijamii, utaifa au dini. Katika haya yote karama ni kipengele cha lazima cha nafsi yao na kitendo chao.

Katika hotuba hiyo muktadha wa pili ni wa  huduma ya matibabu. Baba Mtakatifu amesema Sayansi, na kwa hivyo uwezo wa kuponya, unaweza kusemwa kuwa wa  kwanza kati ya kazi ambazo zina sifa ya Hospitali ya Bambino Gesù leo hii. Ni jibu thabiti wanalotoa kwa maombi ya dhati ya usaidizi kutoka katika familia zinazoomba usaidizi na, inapowezekana, uponyaji kwa watoto wao. Kwa hivyo, ubora katika utafiti wa matibabu ni muhimu. Papa Francisko amewahimiza kukuza kwa bidii hali ya  kujitolea kwa ubora zaidi na kwa uangalifu maalum kwa wagonjwa dhaifu zaidi, kama vile wagonjwa wanaougua magonjwa hatari, adimu au nadra sana.

Jumuiya ya Watoto  ya Bambino Gesu  imekutana na Papa
Jumuiya ya Watoto ya Bambino Gesu imekutana na Papa

Si hivyo tu, bali ili sayansi na utaalamu zisibaki kuwa neema ya walio wachache, Papa amewaomba waendelee kuyafanya matunda ya utafiti wao  yapatikane kwa kila mtu, hasa pale penye uhitaji mkubwa, kama wanavyofanya kwa mfano kwa kuchangia mafunzo ya madaktari na wauguzi wa Afrika, Asia na Mashariki ya Kati. Kwa kuzungumzia juu ya matibabu, Papa amesema tunajua kwamba ugonjwa wa mtoto huathiri washirika wake wote wa familia. Kwa sababu hiyo, ni faraja kubwa kujua kwamba kuna familia nyingi zinazosaidiwa na huduma zao, zinazokaribishwa katika vituo vinavyounganishwa na hospitali na kuwasindikiza na wema na ukaribu wao.  Hiki ni kipengele cha kufuzu, ambacho hakipaswi kupuuzwa kamwe, hata ikiwa anajua kuwa wakati mwingine wanafanya kazi katika hali ngumu. Badala yake wanatoa kitu kingine, lakini sio fadhili na huruma. Hakuna huduma bila uhusiano, ukaribu na huruma, katika viwango vyote.

Hotuba ya Papa ilisomwa na Mons. Ciampanelli
Hotuba ya Papa ilisomwa na Mons. Ciampanelli

Na hatimaye  Papa ameeleza kwamba ni kutafakari muktadha wa tatu ambao ni jumuiya. Mojawapo ya maneno mazuri sana yanayoelezea utume wa Hospitali ya Bambino Gesu’ ni “Maisha yanayosaidia maisha.” Baba Mtakatifu anabainisha kuwa “Ni nzuri, kwa sababu inazungumza juu ya utume wanaofanya pamoja, na hatua ya kawaida ambayo zawadi ya kila mtu hupata nafasi. Hii ndio nguvu yao ya kweli na msingi wa kukabili changamoto ngumu zaidi. Kiukweli, kazi yao si kama nyingine nyingi: ni utume ambao kila mtu anautekeleza kwa njia tofauti. Kwa wengine wanahusisha kujitolea kwa maisha yote; kwa wengine wanatoa wakati wa mtu kama watu wa kujitolea; kwa wengine bado ni mchango wa damu yao wenyewe, ya maziwa yao wenyewe - kwa watoto wachanga waliolazwa hospitalini ambao mama zao hawawezi kutoa -, hadi mchango wa viungo, seli na tishu, zinazotolewa na watu walio hai au kuchukuliwa kutoka katika miili ya watu waliokufa. Mapenzi yanawasukuma baadhi ya wazazi kwa ishara ya kishujaa ya kuridhia mchango wa viungo vya watoto wao ambao hawakufanikiwa kuishi. Katika haya yote kinachojitokeza ni “kufanya pamoja,” ambapo karama mbalimbali huchangia manufaa ya wagonjwa wadogo.

Wafanyakazi wa Hospitali ya Kipapa
Wafanyakazi wa Hospitali ya Kipapa

Katika hotuba hiyo, Baba amependa kuwaeleza jambo moja kuwa “ Ninaungama kwamba wakati ninakuja  “Bambino Gesù” Nina hisia mbili zinazopingana: Ninahisi uchungu kwa mateso ya watoto wagonjwa na wazazi wao; lakini wakati huo huo ninahisi matumaini makubwa, nikiona yote yanayofanywa huko ili kuwaponya. Asante! Asante kwa haya yote. Msonge mbele katika kazi hii yenye baraka. Ninawabariki kutoka ndani ya moyo wangu na kuwaombea. Nanyi pia, tafadhali mniombee. Asante.” Ilihitimishwa kusomwa na hata hivyo baada ya kusomwa hotuba yake, Baba Mtakatifu Francisko naye alisema kuwa: “Sasa nitatoa baraka kwa kila mtu: kwa wagonjwa, kwa madaktari, kwa wauguzi na kwa watu wote wanaofanya kazi katika hospitali hii. Tumuombe Mama Yetu atusaidie tusonge mbele. Salamu Maria,…” na baada ya sala, Papa aliwapa baraka na kuanza kuwasalimia wote ambao walipangiwa hasa watoto walio katika hopitali ya kipapa.”

Papa na watoto wa Gesu bambino
16 March 2024, 18:44