Tafuta

Kabla ya Katekesi ya Papa amekutana na watu wawili mmoja Mwisraeli na mwingine mpalestina lakini wenye historia inayofanana ya kupoteza watoto wao katika hali isiyo na utulivu Nchi Takatifu. Kabla ya Katekesi ya Papa amekutana na watu wawili mmoja Mwisraeli na mwingine mpalestina lakini wenye historia inayofanana ya kupoteza watoto wao katika hali isiyo na utulivu Nchi Takatifu.  (Vatican Media)

Papa amekutana na Rami Elhanan na Bassam Aramin,mwisraeli na mpalestina marafiki!

Kabla ya Katekesi,Papa Francisko alikutana na Rami Elhanan na Bassam Aramin,mwisraeli na Mpalestina wote wawili waliopoteza binti zao wa miaka 10 na 13.Papa alisema:“Hawaangalii uadui wa vita,bali urafiki wa watu wawili wanaopendana na ambao walipitia kusulubiwa sawa.”Papa aidha katika salamu ametoa hata wito kwa ajili ya Mashariki ya Kati na Ukraine inayoteswa na vita.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatano tarehe 27 Machi 2024 kabla ya Katekesi katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, Baba Mtakatifu Francisko alikutana na kusalimiana nao kwa muda mfupi bwana Rami Elhanan na Bassam Aramin, wa kwanza ni Mwisraeli na wa pili wa Kipalestina wote wawili walifiwa na watoto wao wa kike Smadar, mtoto wa Rami Elhanan, aliyekufa kwenye shambulio la mnamo 1997 huko Yerusalemu; Abir, binti wa  Bassam Aramin, alieyeuawa mnamo  2007 na risasi ya mwanajeshi wa kiisraeli wakati anatoka shuleni. Haya yameelezwa na Ofisi ya Vyombo vya habari.

Wakati wa kukutana na kusalimiana nao Mwisraeli na mpalestina marafiki
Wakati wa kukutana na kusalimiana nao Mwisraeli na mpalestina marafiki

Historia ya Rami Elhanan na Bassam Aramin,na kujitolea kwao kwa pamoja kwa ajili ya amani katika haki kupitia chama cha The Parents Circle, ilisimuliwa hata katika riwaya ya Apeirogon na mwandishi Colum McCann, aliyekuwepo kwenye Katekesi ya Papa Francisko pamoja na wasanii mnamo tarehe 23 Juni 2023 na mshindi wa Tuzo ya Terzani.

Historia za maisha yao wanaume hawa wawili zinafanana za kupoteza watoto wao katika vita
Historia za maisha yao wanaume hawa wawili zinafanana za kupoteza watoto wao katika vita

Hata hivyo wakati wa Katekesi, Baba Mtakatifu Francisko aliwataja watu hao kwamba: “Na hapa leo  katika katekesi  hii, kuna watu wawili, baba wawili. Wao ndio wa kwanza: Mwisraeli mmoja na Mwarabu mmoja. Wote wawili walipoteza binti zao katika vita hivi na wote ni marafiki; hawaangalii uadui wa vita, bali wanaangalia urafiki wa wanaume wawili wanaopendana na ambao wamepitia kusulubiwa sawa. Hebu tufikirie ushuhuda huu mzuri sana wa watu hawa wawili walioteseka katika binti zao kutokana na vita katika Nchi Takatifu. Ndugu wapendwa, asante kwa ushuhuda wenu.”

Salamu mbali mbali- Kiarabu

Katika Salamu mbali mbali  za lugha tofauti pia  Baba Mtakatifu kwa wanaozungumza lugha ya Kiarabu alisema: “Tunapokaribia sikukuu ya Pasaka, tubebe akilini na mioyoni mwetu mateso ya wagonjwa, maskini na wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii, tukiwakumbuka pia wahanga wasio na hatia wa vita, ili Kristo kwa Ufufuko wake awape amani na faraja zote. Kwenu nyote wanaozungumza Kiarabu, ninaona Walebanon wengi hapa, Bwana awabariki, awabariki kila mtu na kuwalinda daima kutokana na maovu yote!”

Salamu kwa lugha ya Kiitaliano

Baba Mtakatifu Francisko aliwakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wa  parokia, vyama na shule, hasa kwa wanafunzi wa Taasisi ya Marconi ya Gorgonzola na wale wa Taasisi ya Carlo Alberto Dalla Chiesa wa  Afragola. Katika hali halisi  ya kiroho ya Juma Takatifu, “Ninamewasalimia kwa upendo vijana, wagonjwa, wazee na wanandoa wapya.” Papa amewaalika watu wote kuishi siku hizi katika sala, ili kujifungulia kwa neema ya Kristo Mkombozi, chemchemi ya furaha na huruma. “Na ndugu, tuombe amani. Bwana atupe amani katika Ukraine inayoteswa, ambayo inateseka sana chini ya milipuko ya mabomu; pia katika Israeli na Palestina, kuwe na amani katika Nchi Takatifu. Bwana awape amani wote, kama zawadi ya Pasaka yake.Baraka yangu kwa wote!”

Papa amekutana na mwisraeli na mpalestina wenye historia sawa
27 March 2024, 15:37