Tafuta

2024.03.24  Papa aongoza Misa ya Dominika ya Matawi ikiwa ni mwanzo wa Mateso, kifo na Ufufuko wa Bwana. 2024.03.24 Papa aongoza Misa ya Dominika ya Matawi ikiwa ni mwanzo wa Mateso, kifo na Ufufuko wa Bwana.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa amewaombea waathirika wa kigaidi huko Moscow

Katika sala ya Malaika wa Bwana siku ya Dominika ya Matawi ya Papa ameonesha masikitiko yake kwa shambulio la Urusi,akiomba uongofu wa mioyo ya wale wanaopanga na kutekeleza vitendo hivi vya kinyama vinavyomchukiza Mungu,ambaye aliamuru: 'Usiue'.Baba Mtakatifu amewaombea wale wanaoteseka na vita,kama vile Ukraine na Gaza na amewakumbuka walinda amani wawili waliouawa nchini Colombia katika siku za hivi karibuni.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu amewaombea waathrika wa "shambulio la kigaidi huko Moscow nchini Urusi, mara baada ya hitimisho la Ibada ya Misa Takatifu ya Dominika ya Matawi tarehe 24 Machi 2024 iliyofanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Katika maelezo yake alionyesha huzuni yake kwa kile kilichotokea nchini Urusi siku mbili zilizopita, na alimwomba Mungu kuwakaribisha waathirika, kuwafariji familia zao na kugeuza mioyo ya wale wanaopanga, kupanga na kutekeleza haya, vitendo visivyo vya kibinadamu vinavyomchukiza Mungu, ambaye aliamuru: Usiue'.

Wamini katika uwanja wa Mtakatifu petro katika siku ya Matawi
Wamini katika uwanja wa Mtakatifu petro katika siku ya Matawi

Baba Mtakatifu alianza kusema “Wapendwa kaka na dada, Yesu aliingia Yerusalemu kama Mfalme mnyenyekevu na mwenye amani: tufungue mioyo yetu kwake! Ni Yeye pekee anayeweza kutukomboa kutoka kwa uadui, chuki, vurugu, kwa sababu Yeye ni huruma na msamaha wa dhambi. Tusali kwa ajili ya kaka na dada wote wanaoteseka kwa sababu ya vita;” Baba Mtakatifu akiendelea alisema “Ninaelezea ukaribu wangu kwa Jumuiya ya Mtakatifu  Josè wa Apartado, nchini Colombia, ambapo msichana na mvulana waliuawa siku chache zilizopita. Jumuiya hii ilitunukiwa mwaka wa 2018 kama mfano wa kujitolea kwa uchumi wa mshikamano, amani na haki za binadamu.”

Baba Mtakatifu na Tawi kubwa la Matawi
Baba Mtakatifu na Tawi kubwa la Matawi

Papa Francisko akiendelea alisema: “Na ninawahakikishia maombi yangu kwa wathiriwa wa shambulio la kigaidi la woga lililotekelezwa jioni nyingine  huko Moscow. Mungu  awakaribishe katika amani yake na awafariji familia zao. Na aongoze mioyo ya wale wanaopanga, kupanga na kutekeleza vitendo hivi visivyo vya kibinadamu, vinavyomchukiza Mungu, ambaye aliamuru: "Usiue" (Kut 20:13).”

Hosana mwana wa Daudi
Hosana mwana wa Daudi

Papa Francisko aidha alisema: "Ninwasalimia ninyi nyote, waamini wa Roma na mahujaji kutoka nchi mbalimbali. Hasa ninawasalimu wajumbe kutoka mji wa Sanremo, ambao mwaka huu pia, waaminifu kwa mila ya karne nne, walitoa matawi  ya mitende yaliyofumwa kwa sherehe hii. Asante, Sanremo! Bwana awabariki.

Misa ya Papa ya Matawi

Baba Mtakatifu Francisko hakuishia hapo hasa akifikiria sehemu zenye vita kwamba: “Ninawaza kwa namna ya pekee Ukraine inayoteswa, ambako watu wengi wanajikuta hawana umeme kutokana na mashambulizi makali ya miundombinu ambayo, pamoja na kusababisha vifo na mateso, yanahusisha hatari ya janga kubwa zaidi la kibinadamu.

Papa wakati anaanza kuwasalimia waamini na mahujaji
Papa wakati anaanza kuwasalimia waamini na mahujaji

Tafadhali, tusisahau Ukraine inayoteswa na kufikiria Gaza ambayo inateseka sana, na maeneo mengine mengi ya vita. Na sasa tunageuka katika sala kwa Bikira Maria: tujifunze kutoka kwake kukaa karibu na Yesu katika siku za Juma Takatifu, kufikia furaha ya Ufufuko.” Amehitimisha.

Papa wakati wa sala ya Malaika ameombea waathirika wa shambulio la kigaidi Urusi
24 March 2024, 12:45