Imechapishwa Barua Binafasi ya motu proprio inayoendana na kuoanisha sheria za Mahakama kuu ya Kitume  na mageuzi ya Curia Romana. Imechapishwa Barua Binafasi ya motu proprio inayoendana na kuoanisha sheria za Mahakama kuu ya Kitume na mageuzi ya Curia Romana. 

Papa anabadilisha sheria ya Mahakama Kuu katika mageuzi ya Curia

Kwa barua ya mkono wake (motu Proprio) ya Papa Francisko ya “Munus Tribunalis” baadhi ya mabadiliko ya kiufundi-mafunzo yanawekwa katika sheria zinazosimamia Mahakama Kuu ambalo hutatua mizozo inayotokana na matendo ya mamlaka ya kiutawala ya kikanisa.

Vatican News

Jumamosi tarehe 2 Machi 2024 Baba Mtakatifu Francisko amechapisha Barua Binafsi ya motu proprio ambayo inaendana na kuoanisha sheria za Mahakama Kuu ya Kitume na mageuzi ya Curia Romana ili kutekelezwa na Katiba ya “Praedicate Evangelium.” Sheria ya Mahakama Kuu ambayo imerekebishwa kidogo na mabadiliko ya kileksika, ilikuwa imetangazwa na Benedikto XVI mnamo Juni 2008.

“Katikakutekeleza wajibu wake kama Mahakama Kuu ya Kanisa- Papa Francisko anaandika katika utangulizi kuwa Mahakama Kuu ya Kitume inajiweka katika huduma ya ofisi kuu ya kichungaji ya Papa wa Roma na utume wake wa ulimwengu wote." Kwa njia hii, "kusuluhisha mizozo inayotokana na kitendo cha mamlaka ya kiutawala ya kikanisa, Mahakama Kuu hutoa uamuzi wa uhalali juu ya maamuzi yaliyotolewa na taasisi za  Curia katika huduma yao kwa Mrithi wa Petro na kwa Kanisa la ulimwengu wote.”

Mabadiliko hayo yanahusu uingizwaji wa neno “makasisi” na “makuhani” katika Ibara ya  1 ya sheria yake mwenyewe; badala ya neno “Dicastery” na neno “Mahakama” katika ibara ya 3 na kwa neno “Kuwekwa Tasisi za Curia Romana “ katika ibara  ya 32; badala ya usemi “uliotolewa na Mabaraza ya Curia Romana” na usemi “uliotolewa na taasisi za Curia  katika ibara ya 34; badala ya usemi “Kuhamasisha na kuidhinisha uanzishwaji wa mahakama za majimbo” na usemi “kuidhinisha uundaji wa mahakama za kila aina zinazoundwa na maaskofu wa majimbo zaidi katika Ibara ya  35; badala ya neno “Dicastery” na Taasisi ya Curia katika vifungu vya 79, 80, 81, 92 na 105.

02 March 2024, 13:36