Tafuta

Papa aongoza Ibada ya Misa ya Dominika ya Matawi:Juma Kuu Takatifu!

Katika kumbukumbu ya kuingia kwa Bwana ndani ya mji wa Yerusalemu ilikuwa ni usomaji wa Injili na baadaye maandamamo na Misa ambayo kifungu cha Injili ya Marko kinawasilisha historia ya Mateso ya Kristo na baada ya Misa Papa Francisko alisali sala ya Malaika wa Bwana katika maadhimisho ya Dominika ya Matawi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.Tumeingia katika Juma Kuu Takatifu la Mateso,kifo na Ufufuko wa Bwana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, waamini wanaokadiriwa kufikia 60,000, chini ya anga zuri lililobadilisha juma na mawili ili kufungua maadhimisho ya Dominika ya Matawi tarehe 24 Machi 2024 iliyoongozwa na Baba Mtakatifu Francisko katika ukumbusho wa kuingia kwa Bwana ndani ya mji wa Yerusalemu kama ilivyosikika historia nzima kutoka Mwinjili Marko iliyosomwa katika utangulizi wa adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu.

Papa wakati wa Misa ya Matawi
Papa wakati wa Misa ya Matawi

Baba Mtakatifu alibariki na kunyunyiza matawi ya mizeituni na mitende kama ishara halisi ya siku kwa maji matakatifu, ambapo wote walioudhuria walishikilia mikononi mwao, kama ilivyokuwa katika kila Kanisa Katoliki Ulimwenguni. Maandamano hayo yalifuata, wakiwa wamebeba mitende na mizaetuni zaidi ya watu 400 ambao walielekea kwenye uwanja wa Kanisa kuu kutokea katikati ya uwanja huo. Makardinali, maaskofu na mapadre wakonselebranti walichukua nafasi zao karibu na madhabahu, huku wakiimba wimbo usemao: "Hosana! Mbarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana! Mbarikiwa  Ufalme ujao wa Baba yetu Daudi! Hosana juu mbinguni! "

Maandamano
Maandamano

Mandhari ilikuwa ni nzuri Liturujia ya Neno la Adhimisho la Ekaristi lilijumuisha usomaji unaoimbwa na sauti nyingi za Mateso ya Yesu yaliyochukuliwa tena kutoka katika Injili kulingana na Marko. Kupitia maneno ya mwinjili tunakumbuka tena mapito ya mateso ya Kristo na  ukatili aliofanyiwa. Baada ya kusomwa mateso hayo, ilifuata ukimya mkubwa. Ni mateso, yale ya Kristo, ambayo yana machungu ya nyakati zote na ya wanadamu wote pamoja na udhaifu wake, yaliwasilishwa kwa Bwana katika sala ya ulimwengu wote au sala ya waamini iliyohitimisha Liturujia ya Neno.

Mtazamo wa juu wa waamini na uwakilishi wa maandamano katikati
Mtazamo wa juu wa waamini na uwakilishi wa maandamano katikati

Kama tulivyosema katika misa ya Dominika ya Matawi, Somo la Kwanza lilisomwa kwa lugha ya Kihispania. Zaburi iliimbwa na Kwaya ya Kikanisa cha Sisita, Somo la Pili lilisomwa kwa ugha ya kiingereza, wakati maombi ya ulimwengu: Ombi la Kwanza liliombwa kwa lugha ya kichina, la pili lugha ya kifaransa, la tatu kwa lugha ya kipoland na nne lugha ya kijerumani na la tano ilikuwa ni lugha ya Kiyoruba kwa mara ya kwanza katika matukio haya. Katika maombi kulikuwa na kuombea Kanisa ili siku zote litafute umoja, upatanisho na ushirika; kwa watawala walioitwa kuhamasisha amani na mema ya watu; kwa wanaume na wanawake wote wanaoteseka; kwa Wakristo wanaoteswa; kwa kila jumuiya ya Kikristo ili iwe shahidi wa imani yake yenyewe, katika sala na mapendo.

Familia iliyopeleka vipaji
Familia iliyopeleka vipaji

Mwishoni mwa maadhimisho hayo, moja kwa moja kutoka kwenye uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Baba Mtakatifu  Francisko alisali Sala ya Malaika wa Bwana, na baadaye alitoa baraka zake na kuzunguka katika kigari kidogo  huku akiwasalimu waamini na mahujaji waliokuwa wakimshangilia na kumsalimia katika  uwanja huo.

Misa ya Matawi 24 Machi 2024
Maandamano
Maandamano
24 March 2024, 12:45