2024.03.16 Wajimne wa Mfuko wa Askofu Camillo Faresin wa Maragnole ya Breganze. 2024.03.16 Wajimne wa Mfuko wa Askofu Camillo Faresin wa Maragnole ya Breganze.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa,Askofu Faresin alikuwa mchungaji wa watu maskini!

Papa alikutana na Wajumbe wa Mfuko wa Askofu mmisionari aliyeishi Brazil katika karne iliyopita na kufafanua juu ya upendo usio na kikomo wa kuhani kwa ajili ya maskini na wahitaji.Jina lake limejumuishwa katika“Bustani ya Wenye Haki”huko Yerusalemu kwa ajili ya kufanya yote awezayo kwa upendo na ujasiri katika kuwapendelea Wayahudi walioteswa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko alikutana na Wajumbe wa Mfuko wa Askofu Camillo Faresin, Jumamosi tarehe 16 machi 2024, ambapo hotuba yake imesomwa na Monsinyo Filippo  Ciampanelli, Afisa wa Sekretarieti ya Vatican. Katika Hotuba yake, Baba Mtakatifu anafurahi kuwakaribisha katika fursa ya miaka 20, tangu kuanza kwa Mfuko wao. Baba Mtakatifu anabainisha kuwa: “Leo mnaleta hapa pamoja  miaka ishirini iliyojaa mipango ya kuwahudumia walio maskini zaidi, ikifuatwa katika nyayo za Monsinyo Camillo Faresin, kwa muda mrefu Askofu wa Guiratinga huko Mato Grosso, mfano wa usikivu wa kimisionari na imani katika Mungu mpaji  na pia ya kaka zake wawili: Padre  Santo, pia mmisionari Msalesiani na Padre Giovanni Battista, kuhani  wa jimbo.”

Papa akibariki mtoto wa familia ya wajumbe wa Mfuko wa Mons.Camillo Faresin
Papa akibariki mtoto wa familia ya wajumbe wa Mfuko wa Mons.Camillo Faresin

Baba Mtakatifu katika ujumbe huo alibainisha jinsi ambavyo walipendekeza kuchukua kijiti cha upendo wao kwa kufanya ushupavu wao na mawazo mapana katika kuwatumikia wengine kuwa yao. Na hii imewafanya wafanye kazi yao huko Brazil, Italia na sehemu nyingine za ulimwengu, huku wakieneza katika nyanja tofauti: kutoka katika mafunzo hadi usaidizi wa kijamii, huduma ya afya, hadi kutoa hali ya maisha yenye heshima na fursa kwa kufanya kazi kwa watu wengi. Kwa kutazama kujitolea kwao, Baba Mtakatifu alipenda kusisitiza na kuhimiza njia mbili muhimu za utekelezaji. Kwanza ni kufanya kazi kati yao angalau na kufanya kazi pamoja.

Akianza kufafanua alisema kwanza: kazi kati ya walio wa mwisho. Monsinyo Faresin na kaka zake walikuwa watu wa malezi duni. Walijifunza thamani ya upendo na ari ya umisionari katika muktadha wa familia rahisi, iliyojitolea, ya kiasi na yenye heshima, familia kama yetu walio wengi. Katika mazingira hayo kwa neema ya Mungu waliweza kushika ujumbe na mwaliko wa maisha yao yajayo kuwa miongoni mwa watu wa mwisho wa kusaidia hata kidogo, na walifanya hivyo kwa upendo usiochoka, ukarimu na akili, hata katika matatizo makubwa.

Papa na wajumbe wa Mfuko wa Mons Faresin
Papa na wajumbe wa Mfuko wa Mons Faresin

Papa amesema kuwa “Tukumbuke, katika suala hili, kwamba jina la Askofu Camillus limejumuishwa, huko Yerusalemu, kati ya wale walio katika “Bustani ya Wenye Haki”, hasa kwa sababu, hata kabla ya kuondoka kwenda Brazil, aliyozuiliwa Roma kwa sababu ya Vita vya II vya  Kidunia, hakujiruhusu kuzuiwa na hali, akifanya yote awezayo kwa upendo na ujasiri katika kuwasaidia Wayahudi walioteswa. Hivi ndivyo ilivyokuwa katika maisha yake yote, kama kuhani na kisha Askofu, akiwa na msukumo usiozuilika wa kuwa karibu na walio na bahati mbaya zaidi. Hadi, mara tu mamlaka yake ya uaskofu ilipokwisha, aliomba na kupata kibali cha kubaki miongoni mwa watu wake, huko Mato Grosso, hadi kifo chake kama mtumishi mnyenyekevu wa wanyenyekevu, hivyo akiendelea kujificha, kama rafiki na msindikizaji katika safari, huduma ile ile ambayo alikuwa ameifanya kwa miaka mingi kama kiongozi na mchungaji.

Baba Mtakatifu amekazia kusema kuwa  alichotuachia ni mfano mzuri wa kuiga: kuwa na wa walio wa mwisho, daima! Lakini kwa jinsi gani? Kwa kuchagua na kupendelea, katika mipango yao, hali halisi duni na iliyodharauliwa zaidi kama mahali maalum pa kukaa, na kama nchi ya ahadi ambayo wanaweza kwenda na ambayo wanaweza kupiga hema zao  kuanza kazi mpya (taz. Kumb 1, 8). Na wafanye hivyo kwa uwepo thabiti karibu na jumuiya unazohudumia, kutoka ndani, ili kufanya kazi kati ya maskini na kushiriki maisha yao iwezekanavyo. Ni kwa njia hii tu, kwa kweli, tunaweza kuhisi “mapigo” ya mahitaji halisi ya kaka na dada ambayo Bwana anaweka kwenye njia yetu; na zaidi ya yote tunatajirishwa na nuru, nguvu na hekima inayotokana na kuwa pamoja na Yesu, aliyepo pekee katika viungo vinavyoteseka zaidi vya Mwili wake.

Wajumbe wa Mfuko wa Mons. Faresin
Wajumbe wa Mfuko wa Mons. Faresin

Baba Mtakatifu Francisko amejikita na mutadha wa pili ambao ni kufanya kazi pamoja. Kwa njia hiyo katika shughuli zao amewasihi kila mara wajaribuni kuunda harambee, baina yao na ukweli mwingine wa kidini na wa ushirika. Papa Francisko aidha anajua jinsi ambavyo tayari wanashirikiana, katika kazi mbalimbali, na Masista Wamisionari wa Mapenzi ya Kimungu wa Bassano ya Grappa na mashirika mengine. Ni njia sahihi. Kufanya kazi pamoja, kwa hakika, tayari ndani yake yenyewe ni tangazo la Injili iliyo hai; na kwao, na vile vile njia ya akili ya kuboresha rasilimali, ni njia ya mafunzo katika upendo na ushirika. Walisisitiza hili kwa kulipa mojawapo ya matukio yao ya hivi karibuni kwa mada hii: Kutenda pamoja ili kuendeleza pamoja. Hiyo ni kweli: kutenda pamoja, kiukweli, haimaanishi kutenda mema tu, lakini pia na zaidi ya yote kukua kwa umoja katika wema, mmoja kumtumikia na kumsaidia mwingine.

Hatimaye, kufanya kazi pamoja pia ni onyesho la imani katika maongozi ya Kimungu. Askofu Faresin alilifafanua kuwa: “chanzo kinachohakikisha vyema rasilimali” kwa ajili ya kazi ambazo Mungu anataka.” Na rasilimali muhimu zaidi kwa kazi za Bwana sio vitu, lakini ni sisi, kwa busara tumewekwa karibu na kila mmoja kwa sababu tunashiriki kile tulicho nacho, kwa  shauku yetu, ubunifu wetu, ujuzi wetu na uzoefu, na pia udhaifu wetu na unyonge. Kutokana na ushirikiano huu wa wagonjwa, katika uthamini wa mchango wa kila mtu, matunda ya mabadiliko makubwa ufika na uthabiti, kama historia ya zamani na ya sasa ya Mfuko wao unavyoshuhudia. Baba Mtakatifu kwa njia hiyo alirudia kuwashukuru kwa kile wanachofanya na jinsi wanavyofanya; na kwa sababu hiyo wanaweka uhai  wa kumbukumbu ya moyo mkuu na mkarimu wa kichungaji wa Askofu Camillo Faresin. Mama yetu awaweke katika upendo mnyenyekevu na ujasiri. Hotuba ilihitimisha kwa baraka na kuomba wamwombee!

Wajumbe wa Mfuko wa Mons Camillo Faresin
Wajumbe wa Mfuko wa Mons Camillo Faresin
Hotuba ya Papa kwa Wajumbe wa Mfuko wa Askofu Camillus
16 March 2024, 18:46