2024.03.02 Uzinduzi wa Mwaka wa 95 wa Mahakama Kuu ya Vatican 2024.03.02 Uzinduzi wa Mwaka wa 95 wa Mahakama Kuu ya Vatican  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:Bila ujasiri tuna hatari ya kuishia kutazama dhuluma nyingi ndogo na kubwa!

Katika siku ya kuzinduliwa kwa mwaka wa 95 wa kimahakama Mjini Vatican,Papa amesisitiza juu ya fadhila ya ujasiri."Ni muhimu katika utekelezaji wa haki.Ujasiri una nguvu ya unyenyekevu na msingi wake ni imani na ukaribu wa Mungu na unaoneshwa kwa namna fulani katika uwezo wa kutenda kwa subira na ustahimilivu,ukikataa hali ya ndani na nje inayozuia utimilifu wa wema."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na kutoa hotuba yake iliyosomwa na Monsinyo Ciampanelli wakati wa kuzindua mwaka wa 95 wa Mahakama ya Rufaa ya Kipapa mjini Vatican, mbele ya wahamasishaji wa Haki, wachunguzi, maafisa, wanasheria na wahudumu wa Mahakama, Jumamosi tarehe 2 Machi 2024. Katika hotuba hiyo Baba Mtakatifu anaanza kuwashukuru  mamlaka ya kiraia na kijeshi ya Italia kwa uwepo wao. Amewakushukuru kwa huduma yao, maridadi na inayohitajika; na pamoja na kikosi cha Ulinzi cha Vatican kwa ushirikiano wao uliohitimu. Katika tukio hili alipenda kutafakari kwa ufupi nao juu ya fadhila anayoifikiria mara kadhaa kufuatia matukio yanayohusu utoaji haki, pia katika serikali ya mji wa  Vatican. Ni kuhusu ujasiri.

Uzinduzi wa mwaka wa Mahakama Kuu ya Vatican
Uzinduzi wa mwaka wa Mahakama Kuu ya Vatican

Baba Mtakatifu amesema kuwa kwa Wakristo fadhila hii, ambayo kwa shida, ikiunganishwa na uhodari, huhakikisha ustahimilivu katika kutafuta mema na kumfanya mtu kuwa na uwezo wa kukabiliana na majaribu, haiwakilishi tu sifa fulani ya nafsi ya baadhi ya watu mashujaa. Badala yake ni sifa inayotolewa na kuimarishwa katika kukutana na Kristo, kama tunda la utendaji wa Roho Mtakatifu ambalo mtu yeyote anaweza kupokea ikiwa atamwomba. Ujasiri una nguvu ya unyenyekevu, ambayo msingi wake ni imani na ukaribu wa Mungu na unaoneshwa kwa namna fulani katika uwezo wa kutenda kwa subira na ustahimilivu, ukikataa hali ya ndani na nje inayozuia utimilifu wa wema. Ujasiri huu huwavuruga wafisadi na kuwaweka pembeni, kwa njia ya kusema, huku mioyo yao ikiwa imefungwa na kuwa migumu.

Papa akimsikiliza Hakimu Mkuu wa Makahama Kuu ya Vatican
Papa akimsikiliza Hakimu Mkuu wa Makahama Kuu ya Vatican

Hata katika jamii zilizojipanga vizuri, zinazodhibitiwa vyema na kuungwa mkono na taasisi, Papa akasisitza kuwa ujasiri wa kibinafsi daima ni muhimu ili kukabiliana na hali tofauti. Bila ujasiri huu mzuri, tuna hatari ya kujiuzulu na kuishia kutazama dhuluma nyingi ndogo na kubwa. Wale walio jasiri hawalengi uhusika wao wenyewe, bali mshikamano na kaka na dada zao wanaobeba uzito wa hofu na udhaifu wao. Tunaona ujasiri huo kwa kustaajabishwa na wanaume na wanawake wengi wanaopatwa na majaribu magumu sana: hebu tufikirie waathiriwa wa vita, au wale wanaokabiliwa na ukiukwaji wa mara kwa mara wa haki za binadamu, miongoni mwao ni Wakristo wengi wanaoteswa. Mbele ya dhuluma hizi, Roho hutupatia nguvu ya kutojiuzulu, inaamsha ndani yetu hasira na ujasiri: hasira katika uso wa ukweli huu usiokubalika na ujasiri wa kujaribu kubadili.

Uzinduzi wa Mwaka wa Makahama Vatican
Uzinduzi wa Mwaka wa Makahama Vatican

Katika hotuba hiyo, Baba Mtakatifu anazidi kukazia kuwa, kwa ujasiri huu tunaitwa pia kukabiliana na ugumu wa maisha ya kila siku, katika familia na katika jamii, kujitolea kwa mustakabali wa watoto wetu, kulinda nyumba yetu ya pamoja, kuchukua majukumu yetu ya kitaaluma. Na hii inatumika hasa kwa eneo ambalo wanafanyia kazi, lile la usimamizi wa haki. Kiukweli, pamoja na fadhila za busara na haki, ambazo lazima zifahamishwe na hisani, na pamoja na kiasi kinachohitajika, kazi ya kuhukumu inahitaji fadhila za nguvu naujasiri, bila hiyo  hekima inahatarisha kubaki tasa. Inahitaji ujasiri ili kuuthibitisha ukweli kwa uthabiti, tukikumbuka kwamba kutenda haki siku zote ni tendo la upendo, fursa ya masahihisho ya kindugu ambayo yananuia kumsaidia mwingine kutambua kosa lake.

Uzinduzi wa Mwaka wa 95 wa Kimahakama Vatican
Uzinduzi wa Mwaka wa 95 wa Kimahakama Vatican

Papa Francisko anabainisha kuwa hii inatumika pia wakati tabia ambazo ni mbaya na za kashfa zinaibuka na lazima zikubaliwe, hata zaidi zinapotokea ndani ya jamii ya Kikristo. Wanahitaji kuwa na ujasiri wakati wanashughulika na kuhakikisha mwenendo wa haki wa majaribio na uko chini ya ukosoaji. Uimara wa taasisi na uthabiti katika usimamizi wa haki unaoneshwa na utulivu wa hukumu, uhuru na kutopendelea kwa wale wanaoitwa kuhukumu katika hatua mbalimbali za mchakato. Jibu bora zaidi ni ukimya wa bidii na kujitolea kwa dhati kufanya kazi, ambayo huruhusu Mahakama zetu kusimamia haki kwa mamlaka na bila upendeleo, kuhakikishia mchakato unaostahili, kwa kuzingatia upekee wa mfumo wa Vatican.

Katika hotuba hiyo Baba Mtakatifu akazia kusisitiza kuwa "hatimaye, ujasiri unahitajika ili kusihi katika sala kwamba nuru ya Roho Mtakatifu daima iangaze utambuzi unaohitajika ili kufikia matokeo ya hukumu ya haki. Pia katika muktadha huu Baba Mtakatifu amependa  kuwakumbusha kwamba mng’amuzi yanafanywa kwa kupiga  magoti yao, kuomba karama ya Roho Mtakatifu, ili kuweza kufikia maamuzi ambayo yanaendana katika mwelekeo wa wema wa watu na wa ulimwengu wote na  jumuiya ya kikanisa. Kiukweli, kama ilivyoelezwa katika Sheria ya CCCLI kuhusu kanuni ya Serikali, “kusimamia haki si hitaji la muda tu. Sifa kuu ya uadilifu, kiukweli, inaakisi na kufupisha madhumuni yenyewe ya mamlaka ya mahakama ya kila Nchi, ili kukuza ambayo dhamira ya kibinafsi, ya ukarimu na ya uwajibikaji wa wale waliowekewa jukumu la mamlaka ni muhimu.” Kwa njia hiyo ameongeza kuwa: “Ahadi hii inahitaji kuungwa mkono na maombi.

Uzinduzi wa mwaka wa 95 wa Mahakama ya mji wa Vatican
Uzinduzi wa mwaka wa 95 wa Mahakama ya mji wa Vatican

Baba Mtakatifu akazia kusema kuwa wao hawapaswi kuogopa kupoteza wakati kwa kujitolea zaidi kwake, Papa amekazia. Na kwa hili pia inahitaji ujasiri na nguvu ya kiroho. Kwa  Mahakimu wa Mahakama, wahamasishaji wa Haki, wachunguzi, maafisa, wanasheria na wahudumu wa Mahakama, Baba Mtakatifu anawatakia katika huduma yao ya haki, inaweza kudumishwa daima pamoja busara, na ujasiri wa kikristo. Anawaombea kwa Bwana ili aimarishe fadhila hii ndani yao. Anawabariki kwa moyo wote na kazi yao, huku akiikabidhi kwa Bikira Mtakatifu,(Speculum iustitiae)Kioo cha Haki. Na tafadhali wasisahau kumuombea.

Uzinduzi-Mwaka wa 95 wa Mahakama Vatican
02 March 2024, 13:22