Baba Mtakatifu Francisko atoa tena wito wa kusitisha vita Ukanda wa Gaza na kurejea tena kwenye meza ya majadiliano. Baba Mtakatifu Francisko atoa tena wito wa kusitisha vita Ukanda wa Gaza na kurejea tena kwenye meza ya majadiliano.   (AFP or licensors)

Papa Francisko Asikitishwa Na Mateso ya Watu wa Mungu Ukanda wa Gaza

Takwimu zinaonesha kwamba, kuna Wapalestina 30, 320 waliouwawa katika mapigano haya na kwamba, kuna watu 70, 457 wamejeruhiwa na kati yao watu 11, 000 wamejeruhiwa vibaya na wanahitaji msaada wa haraka. Hadi kufikia mwezi Januari 2024, kuna watu milioni 1.9 hawana makazi maalum huko kwenye Ukanda wa Gaza na baadhi yao, wameruhusiwa kupata hifadhi nchini Misri. Bila amani ni vigumu sana kujenga ulimwengu ili uweze kuwa ni mahali pazuri pa kuishi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Kwa mara nyingine tena, Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 3 Machi 2024 kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, amesema, anafuatilia kwa uchungu mkubwa mateso na mahangaiko ya wananchi wa Palestina na Israeli kutokana na uadui uliojengeka kati yao kwa miaka ya hivi karibuni. Takwimu zinaonesha kwamba, kuna Wapalestina 30, 320 waliouwawa katika mapigano haya na kwamba, kuna watu 70, 457 wamejeruhiwa na kati yao watu 11, 000 wamejeruhiwa vibaya na wanahitaji msaada wa haraka. Hadi kufikia mwezi Januari 2024, kuna watu milioni 1.9 hawana makazi maalum huko kwenye Ukanda wa Gaza na baadhi yao, wameruhusiwa kupata hifadhi nchini Misri.

Mateso ya watu wa Mungu Ukanda wa Gaza
Mateso ya watu wa Mungu Ukanda wa Gaza

Baba Mtakatifu anasikitika kusema kwamba, vita hii inaendelea kuharibu miundo mbinu pamoja na makazi ya watu, kiasi hata cha kuhatarisha mustakabali wa Wapalestina kwa siku za usoni. Kwa njia ya vita, haitawezekana kujenga ulimwengu ulio bora zaidi wa kuishi na kwamba, amani ya kweli ni kichocheo cha ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Baba Mtakatifu ametoa wito kwa Palestina na Israeli kusitisha mapigano mara moja huko kwenye Ukanda wa Gaza na kuanza kujikita katika majadiliano yanayosimikwa katika ukweli kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Hii iwe ni fursa pia kwa mateka wa vita kuachiliwa mara moja bila masharti, ili waweze kurejea tena makwao, kwani ndugu na jamaa wanawasubiri kwa hamu kubwa sana. Wananchi wahakikishiwe usalama wa maisha yao ili hatimaye waweze pia kupata misaada inayotolewa na Jumuiya ya Kimataifa. Baba Mtakatifu amewakumbuka pia watu wa Mungu nchini Ukraine wanaoendelea kuuwawa kila siku na kwamba, kuna mateso makali nchini Ukraine.

Vita Ukanda wa Gaza

 

04 March 2024, 14:25