Papa Francisko:kushinda wazimu wa vita,vijana wengi wanakufa!
Vatican News
Kushinda wazimu huu wa vita ambayo daima ni kushindwa. Ni matumaini ambayo Papa aliyaeleza mwishoni mwa katekesi yake Jumatano tarehe 13 Machi 2024, siku ambayo ameadhimisha miaka kumi na moja ya Upapa. Kama ilivyokuwa katika vikao vilivyotangulia, kutokana na mafua, Papa Fransisko hakuweza kusoma katekesi yake badala yake, alimkabidhi Padre Pierluigi Giroli usomaji huo; Lakini hata hivyo yeye mwenyewe alisoma salamu zake kwa Kiitaliano, ambamo kwa mara nyingine tena akapyaisha mwaliko wa kuwaombea watu wanaokumbwa na migogoro. “Ninawaalika kila mtu kuendelea na kujitolea katika ratiba ya Kwaresima, tayari kutekeleza ishara za mshikamano wa Kikristo popote Mpaji anapowaita kufanya kazi. Na tafadhali, na tudumu katika maombi ya bidii kwa ajili ya wale wanaoteseka na matokeo mabaya ya vita.
Baba Mtakatifu amewaeleza waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwamba amepokea “Rozari na Biblia ya askari kijana aliyekufa katika maoambano”. Alisali kwa ajili ya “Vijana wengi, vijana wengi wanakwenda kufa!" Hapa kuna ombi la maombi: “Tumwombe Mungu atupatie neema ya kuushinda huu wazimu wa vita ambao daima ni kushindwa. Na tafadhali, na tudumu katika maombi ya bidii kwa ajili ya wale wanaoteseka na matokeo mabaya ya vita."
Papa amewasalimia Wamisionari Wakalmeri wanaofanya Mkutano Mkuu, na wale wa Moyo Mtakatifu wa Yesu huku akiwatia moyo wa kulinda urithi wa kiroho katika mashirika hayo ya kitawa. Amewasalimu waamini wa parokia ya Santa Maria Goretti huko Frigole, waamini wa Mtakatifu Domenica kutoka maeneo tofauti, Kitivo cha Sheria ya Kanoni cha Mtakatifu Pio. Salamu pia zimewaendea wanafunzi wa Shule ya Afisa Mdogo wa Jeshi la Wanamaji la Taranto Italia, ambao amewahimiza kutekeleza huduma yao kwa uaminifu na ukarimu.
Hatimaye, mawazo yake yamewaendea wagonjwa, wazee, wanadoa za hivi karibuni na vijana, hasa wanafunzi wengi waliokuwapo, hasa katika Taasisi ya Carbone e Rosati kutoka Sora, Italia. Papa amewaalika kila mtu kuendelea na kujitolea katika ratiba ya Kwaresima, tayari kutekeleza ishara za mshikamano wa Kikristo popote ambapo Mungu mpaji anawaita kufanya kazi. Amewakaribisha mahujaji wote wanaozungumza Kiingereza, hasa vikundi kutoka Uholanzi na Marekani. Kwa matakwa ya dhati kwamba Kwaresima hii itakuwa wakati wa neema na kufanywa upya kiroho kwa ajili yenu na familia zenu, ninawaombea wote furaha na amani ya Bwana Yesu. Mungu awabariki!
Baba Mtakatifu amewasalimia wa lugha ya kipoland. Katika nyakati zetu hizi za kutisha, ambazo mara nyingi tunakumbana na yaliyo mabaya zaidi katika ubinadamu, ni muhimu kugundua tena umuhimu wa kusitawisha ndani yetu tabia ya mazoea na thabiti ya kutenda mema. Jifunzeni haya kutoka kwa Watakatifu wenu, mkitafuta msaada wa neema ya Mungu. Nawabariki kutoka ndani ya moyo wangu. Ninawasalimu kwa upole mahujaji wanaozungumza Kifaransa, hasa vikundi vingi vya shule ambavyo vimetoka Ufaransa. Ndugu na dada, katika kipindi hiki chenye baraka za Kwaresima, tumgeukie Bibi Yetu, Kiti cha Hekima, ili kwa maombezi yake atusaidie kujiweka katika huduma ya wema. Mungu awabariki!
Baba Mtakatifu:amewasalimu waamini wanaozungumza Kiarabu. Mkristo anaitwa kukuza wema katika maisha yake, kwa sababu inamruhusu sio tu kufanya matendo mema, lakini kutoa bora zaidi yake mwenyewe. Bwana awabariki nyote na kuwalinda daima na mabaya yote! Baba Mtakatifu: Wapendwa kaka na dada wanaozungumza Kijerumani, tusisahau kwamba Bwana mwenyewe anatusindikiza katika njia ya wema. Kwa hiyo tunatumaini msaada wake wa kuweza kueneza mema anayohitaji sana ulimwenguni pote.