Tafuta

2024.03.01 Papa Francisko akutana na washiriki wa m,kutano  kuhusu Mazingira magumu na Jumuiya kati ya ukarimu na kujumuisha. 2024.03.01 Papa Francisko akutana na washiriki wa m,kutano kuhusu Mazingira magumu na Jumuiya kati ya ukarimu na kujumuisha.  (Vatican Media)

Papa:ili kukaribisha wenye mazingira magumu lazima wawekwe katikati!

Papa akikutana mjini Vatican na washiriki wa toleo la pili lenye mada:“Kiti cha Ukarimu” lililomalizika Machi 1 Machi huko Sacrofano amesisitizia ukaribu kwa mfano wa Yesu ambaye alitaka kuwazoeza wanafunzi wake katika mtindo-maisha kwa kuwasiliana na watu wasiojiweza kati yao.Wanafunzi waliona jinsi alivyokutana na watu,waliona jinsi alivyokaribisha hadi kufa Msalabani kwa ajili yao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

“Mazingira magumu na Jumuiya kati ya ukarimu na kujumuisha” ilikuwa ni mada ya toleo la 2024 iliyofunguliwa tangu tarehe 27 Februari hadi tarehe 1 Machi 2024 katika Ukumbi wa Udugu huko Sacrofano Roma ambapo katika mwisho wa mkutano huo,  kama ilivyokuwa imepangwa tarehe Mosi Machi, 2024  Wajumbe hao wamekutana na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Baba Mtakatifu kwa mara nyingine tena amemkabidhi hotuba yake Monsinyo Filippo Ciampanelli, wa Sekretarieti ya Vatican ili aisome.  Katika hotuba hiyo Papa anabainisha jinsi ambavyo kwa siku hizi wamejikita katika mada ya “kiti cha Ukarimu.” Hapo ni mahali pazuri! Sio tu kwa sababu ni mahali pakubwa na kuna vifaa: panafaa kwa sababu panakaribisha! Ni mahali ambapo wazee, familia na watoto katika shida, wahamiaji wanakaribishwa. Hii ndiyo sababu ni jambo la kupendeza kwamba watawa wa Nyumba ya Udugu kwa kiasi fulani  wanasukka na wahuishaji wa mpango huo. Na kwa hiyo amewashukuru watawa hao. Lakini akijikita na mpango mzima wa siku hizi alisema ulikuwa tajiri sana na wa kuvutia sana.

Mkutano kuhusu mazingira magumi na jumuiya kati ya ukarimu na ujumuishwaji
Mkutano kuhusu mazingira magumi na jumuiya kati ya ukarimu na ujumuishwaji

Waliweka watu wa mazingira magumu katikati. Hiyo ni na walifanya kukubalika na mazingira magumu kuguswa  kama ambavyo angesema katika kemia – “kuzingatiwa katika aina zake tofauti.”  Baba Mtakatifu kwa hivyo anathamini  chaguo hili, kwa kawaida la kiinjili, na alipenda kuwachia baadhi ya mawazo ya kutafakari na safari yao. Kwanza kabisa: “ili kuwakaribisha kaka na dada walio katika mazingira magumu lazima nijisikie dhaifu na kukaribishwa hivyo na Kristo. Yeye daima hututangulia: alijifanya kuwa hatarini, hadi Mateso; alikaribisha udhaifu wetu kwa sababu, shukrani Kwake, tunaweza kufanya vivyo hivyo. Mtakatifu Paulo anaandika: “Mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama Kristo alivyowakaribisha” (Rm 15:7). Tukikaa ndani yake, kama matawi katika mzabibu, tutazaa matunda mazuri, hata katika shamba hili kubwa la ukarimu.

Wazo la pili. Yesu alitumia sehemu kubwa ya huduma yake ya hadharani, hasa Galilaya, akiwasiliana na maskini na wagonjwa wa kila namna. “Hii inatuambia kuwa mazingira magumu kwetu hayawezi kuwa mada ‘sahihi kisiasa’, au shirika tu la mazoea, hata liwe jema. Ninasema hivi kwa sababu kwa bahati mbaya hatari ipo, huwa inanyemelea, licha ya nia njema, katika hali halisi kubwa na muundo zaidi, lakini pia katika hali ndogo, mazingira magumu yanaweza kuwa jamii, watu wasio na uso, huduma “utendaji” na kadhalika. Kisha ni lazima tubaki tukiwa tumeshikilia vyema Injili, kwa Yesu, ambaye hakuwafundisha wanafunzi wake kupanga huduma kwa wagonjwa na maskini.  Yesu alitaka kuwazoeza wanafunzi wake katika mtindo wa maisha kwa kuwasiliana na watu wasiojiweza kati yao.

Papa amewasalimu na kuzungumza na washiriki wa Mkutano kuhusu ukarimu
Papa amewasalimu na kuzungumza na washiriki wa Mkutano kuhusu ukarimu

Wanafunzi waliona jinsi alivyokutana na watu, waliona jinsi alivyokaribisha: ukaribu wake, huruma yake, upole wake. Na baada ya Ufufuko Roho Mtakatifu aliweka chapa mtindo huu wa maisha ndani yao. Hivyo basi, Roho daima aliwaumba wanaume na wanawake ambao walikuja kuwa watakatifu kwa kuwapenda watu wasiojiweza kama Yesu.” Katika hotuba hiyo Baba Mtakatifu akazia kusema kuwa “Baadhi wametangazwa kuwa watakatifu na ni mifano kwa ajili yetu sote; lakini ni wanaume na wanawake wangapi wamejitakasa kwa kuwakaribisha wadogo, maskini, walio dhaifu, waliotengwa! Na ni muhimu, katika jumuiya zetu, kushiriki historia za mashahidi hawa waliofichwa wa Injili kwa urahisi na shukrani.

Katika muktadha huo Papa Francisko amependa kuwaachia jambo jengine la mwisho. “Katika Injili maskini, walio katika mazingira magumu, si vitu, ni raia, ni wahusika wakuu pamoja na Yesu wa tangazo la Ufalme wa Mungu. Tumfikirie Bartimayo, kipofu wa Yeriko (rej, Mk 10,46-52). Historia hiyo ni nembo”, ambayo  Papa amependa kuwaalika  wasome  “tena mara kwa mara kwa sababu ni tajiri sana. Tukijifunza na kutafakari andiko hili tunaona kwamba Yesu anapata kwa mtu huyo imani aliyokuwa akiitafuta: Yesu pekee ndiye anayemtambua katikati ya umati na kelele, anasikiliza kilio chake kilichojaa imani.”

Papa amekutana na washiriki wa Mkutano kuhusu ukarimu na ushirikishwaji
Papa amekutana na washiriki wa Mkutano kuhusu ukarimu na ushirikishwaji

Na kwamba “ mtu huyo, ambaye kwa imani yake katika Bwana alipata kuona tena, alitoka, alimfuata Yesu na kuwa shahidi wake, kiasi kwamba historia yake iliingia kwenye Injili. Bartimayo aliye hatarini, aliyeokolewa na Yesu aliye hatarini, alishiriki furaha ya kushuhudia Ufufuko wake.” Kwa njia hiyo Papa amesema, ametaja hiyo hisotria lakini pia kuna nyingine nyingi, zenye sifa tofauti za mazingira magumu, si tu kimwili. Kwa mfano tumfikirie Magdalena: yeye, ambaye aliteswa na pepo saba, akawa shahidi wa kwanza wa Yesu aliyefufuka. Kwa muhtasari: watu walio katika mazingira magumu, waliokutana na kukaribishwa kwa neema ya Kristo na mtindo wake, wanaweza kuwa uwepo wa Injili katika jumuiya ya waamini na katika jamii.” Kwa kuhitimisha aliwashukuru kwa kujitolea kwao na kuwaomba waendelee. Mama Yetu awasindikize kila wakati. Alitoa baraka kutoka ndani ya Moyo wake na kuwaomba tafadhali wamwombee.

01 March 2024, 15:50