Tafuta

2024.03.15 Kardinali Paul Josef Cordes. 2024.03.15 Kardinali Paul Josef Cordes. 

Papa,Kard.Cordes alikuwa mwaminifu,mkarimu&makini kwa vijana!

Kufuatia na kifo cha Cordes 15 Machi 2024 wa miaka 89,Roma,mmoja wa wavumbuzi wa WYD na rais mstaafu wa Baraza la Kipapa la Walei,Papa ametuma rambirambi akimkumbuka kwa upendo ambaye alitumikia Bwana na Kanisa kwa uaminifu na ukarimu,makini katika masuala ya ulimwengu wa vijana.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 machi 2024 ametuma Telegramu ya rambi rambi kufuatia na kifo cha Kardinali Paul Josef Cordes, kilichotokea tarehe 15 Machi 2024 jijini Roma akiwa na umri wa miaka 89. Katika salamu za rambi rambi zilizotumwa kwa Bwana Klaus na Rainer Baumgardit, anabainisha kuwa, baada ya kupata habari za kifuo cha Mjomba wao Kardinali Paul Joseph Cordes, anaelezea ukaribu wake kwao, na wanafamilia wote, kama ilivyo haya Jimbo Kuu la Paderbon ambapo alifikia kikuhani na baadaye kuwa Askofu Msaidizi. Baba Mtakatifu anamkumbuka kwa upendo ambaye alimtumikia Bwana na Kanisa kwa uaminifu na ukarimu, makini katika masuala ya ulimwengu wa vijana na mahitaji ya watu wadhaifu,  ambao aliwasilisha upendo na huruma ya Kristo.

Kardinali Cordes
Kardinali Cordes

Baba Mtakatifu aidha amemfikiria kwa shukrani ya huduma yake aliyoitoa kwa miaka mingi Vatican, kwanza kama Makamu Rais wa Baraza la Kipapa la Walei kisha akawa Rais wa Baraza la Kipapa la COR UNM, ambapo hakuacha nguvu ya kushuhudia Ubaba wa Maombi ya Papa kwa Maskini zaidi. Kutokana na hiyo Baba Mtakatifu anainua sala kwa Bwana ili kwa maombezi ya Bikira Maria, ampokee huyo mwaminifu, mtumishi na Mchungaji katika mbingu ya Yerusalemu na kwa moyo anawatumia wote wanaoomboleza kuondoka kwake duniani, baraka yake.

Kardinali Paul Josef Cordes, Rais mstaafu wa Baraza la Kipapa "Cor Unum", alizaliwa tarehe 5 Septemba 1934 Kirchhundem, Jimbo kuu la Paderborn  nchini Ujerumani. Baada ya kumaliza masomo yake ya msingi, alianza shahada yake ya matibabu. Mwaka 1956 alihisi wito wa maisha ya kipadre ukitokea ndani yake na, baada ya kuacha masomo yake ya chuo kikuu, akaingia katika seminari kuu ya Paderborn. Katika kipindi hiki pia alihudhuria kozi ya mwaka mmoja katika seminari ya chuo kikuu cha Lyon. Akapewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 21 Desemba 1961. Baada ya kutekeleza kipindi cha kazi ya kichungaji katika parokia mbali mbali za jimbo, kunako mwaka 1969 alianza tena masomo yake kwa kuhudhuria kozi ya mafundisho ya kweli katika Chuo Kikuu cha Mainz. Mnamo 1971 alipata digrii ya taalimungu, akitetea tasnifu yenye kichwa: Umetumwa kutumika. Ukuhani wa daraja:historia, ufafanuzi, mada, utaratibu,iliyochapishwa mwaka wa 1990 kwa Kiitaliano na Piemme (Casale Monferrato). Mnamo mwaka wa 1972 Kardinali Döpfner, aliyekuwa rais wa Baraza la Maaskofu wa Ujerumani, alimteua kuwa katibu wa Tume ya kichungaji ndani ya Baraza lenyewe. Ilikuwa ni katika kipindi hiki ambapo, hasa kwa nguvu ya nafasi yake, alianza kushirikiana na vyama, harakati na taasisi mbalimbali za kikanisa nchini Ujerumani. Uzoefu ambao aliweza kuutoa kwa sinodi ya majimbo ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, iliyofanyika kuanzia mwaka 1972 hadi 1975, ambapo maaskofu, mapadre na walei walishiriki. Sinodi ilikuwa imeitishwa kwa ajili ya mashauri na maamuzi ya asili ya kichungaji.

Papa Paulo VI alimteua kuwa Askofu msaidizi wa Paderborn tarehe 27 Oktoba 1975. Alipokea daraja la uaskofu tarehe 1 Februari 1976. Mwaka 1980 Yohane Paulo II alimwita kutumikia Curia Romana kwa kumteua kuwa makamu wa rais wa Baraza la Kipapa la Walei. Hii ilifuatiwa na uteuzi kama washauri wa ofisi zingine za Curia Romana. Papa pia alimteua kwa niaba yake kufuatlia utume wa Ofisi ya Kimataifa ya Ufufuko wa Karismatiki ya Kikatoliki na Njia ya Neocatecumenali nafasi ambayo alishikilia hadi Desemba 1995.

Alikuwa mtangazaji wa Kituo cha Kimataifa cha Vijana cha Mtakatifu  Lorenzo, kilichozinduliwa huko Roma mnamo 13 Machi 1983. Ilikuwa wakati wa mkutano katika Kituo hicho - hafla hiyo ilikuwa sherehe ya Mwaka Mtakatifu Maalumu 1983-1984 - wazo la kuandaa mkutano ulizaliwa na vijana duniani kote. Tukio hilo lilifanyika Dominika ya Matawi 1984 na kuashiria kuzaliwa kwa Siku za Vijana Duniani(WYD).

Kardinali Cordes
Kardinali Cordes

Tarehe 2 Desemba 1995 alipandishwa hadhi ya Askofu mkuu na kuteuliwa kuwa rais wa Baraza la Kipapa la Cor unum. Yeye ndiye mwandishi wa machapisho mbalimbali, aliyezaliwa zaidi ya yote kutokana na ujuzi wake wa ukweli wa harakati na jumuiya mpya za kikanisa. Za hivi karibuni zaidi ni: Ushiriki hai katika Ekaristi, Ushiriki wa Actuosa katika jumuiya ndogo ndogo (1996), Ishara za matumaini. Harakati na ukweli mpya katika maisha ya Kanisa katika mkesha wa Jubilei (1998), Kupatwa kwa Baba. Na kilio(2002).

Katika miaka ya hivi karibuni amepewa dhamana ya utume mbalimbali duniani ili kuleta upendo na mshikamano wa Papa kila mahali. Aidha aliweza kushiriki katika kazi ya Kongamano la Caritas la Shirikisho zima la Urussi, lililofanyika mjini Moscow kuanzia tarehe 18 hadi 21 Oktoba 2007. Katika tukio hili alitembelea Novosibirsk, ambako alikutana na wamisionari wa upendo wa Mama Teresa wa Calcutta ambao wamekuwa wakifanya kazi katika eneo hilo kwa miaka mingi, na wafanyakazi wa shule ya Wafransiskan. Mnamo Oktoba 18 huko Moscow alikutana na Patriaki wa Kanisa la Orthodox la Urusi, Alexy II. Na amekuwa Rais mstaafu wa Baraza la Kipapa Cor Unum la wakati huo, tangu tarehe 7 Oktoba 2010. Cha mwisho hata hivyo aliweza kushiriki katika mkutano wa Machi 2013 uliomchagua Papa Francisko.

Rambi rambi
16 March 2024, 18:13