Tafuta

Papa:Yesu hatunyoshei kidole ni kutukumbatia,maisha,kutukomboa na dhambi zetu!

Mbele ya Yesu hakuna siri: Yeye anatazama ndani ya mioyo,katika moyo wa kila mmoja wetu.Kiukweli hakuna aliye mkamilifu,wote ni wadhambi,wote tunakosea na ikiwa Bwana angetumia utambuzi wa udhaifu wetu kwa ajili ya kutuhukumu hakuna ambaye angeokoka.Amesema hayo Papa Francisko kuhusu Injili ya Dominika ya IV ya Kwaresima kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Machi 10.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika  Dominika ya  Nne ya Kwaresima ambayo inaitwa "laetare" maana yake ni Dominika ya furaha, Waamini na mahujaji walikusanyika kama kawaida katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican tarehe 10 Machi 2024 kusikiliza tafakari ya Baba Mtakatifu na kusali naye sala ya Malaika wa Bwana. Baba Mtakatifu Kupitia Dirisha la Jumba la Kitume alianza tafakari hiyo ambapo baada ya kuwasalimia alisema kuwa “Katika Dominika hii ya Nne ya Kwaresima, Injili inatuwakilisha sura ya Nikodemu (Yh 3,14-21), Mfarisayo “mmoja wa wakuu wa Kiyahudi (Yh 3,1). Yeye aliona ishara alizotimiza Yesu, alizitambua katika Yeye kama Mwalimu aliyetumwa na Mungu na alikwenda kukutana naye usiku, ili hasionekane. Bwana alimpokea  alizungumza naye na yeye kumuonesha jinisi alivyokuja sio kwa ajili ya kuhukumu bali kuokoa ulimwengu(rej. Yh 3,17). Jinsi gani ilivyo nzuri!

Baba Mtakatifu Francisko ameongeza kusema kuwa “Mara nyingi katika Injili tunaona Kristo anavyoonesha nia za watu anaokutana nao, na mara nyingi kuibua nje tabia za uwongo, kama zile za wafarisayo (rej. Mt 23, 27-32), au kwa kufanya watafakari juu ya maisha yao yasiyo na msimamo, kama ule wa Msamaria )Yh 4,5-42). Mbele yake Yesu hakuna siri: Yeye anatazama ndani ya mioyo, katika moyo wa kila mmoja wetu. Na uwezo huu unaweza kutia wasi wasi, kwa sababu ikiwa umetumiwa vibaya, unaharibu watu, kwa kuwaweka katika hukumu isiyo na huruma. Kiukweli hakuna aliye mkamilifu, wote ni wadhambi, wote tunakosea, na ikiwa Bwana angetumia utambuzi wa udhaifu wetu kwa ajili ya kutuhukumu, hakuna ambaye angeokoka.

Papa ametoa tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana
Papa ametoa tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana

Papa ameongeza kusema: “Lakini si hivyo. Yeye kwa dhati haitaji kutunyoshea kidole, lakini kwa ajili ya kutukumbatia, maisha yetu, ili kutukomboa na dhambi zetu, na kwa ajili ya kutuokoa. Kwake Yesu hana haja ya kutufanya kuwa na mchakato au kutuweka katika hukumu; Yeye anataka kwamba kati yetu  pasiwepo yeyote apotee. Mtazamo wa Bwana juu yetu sio mwanga wa kupofusha ambao huangaza na kutuweka katika shida, lakini ni mwanga wa upole wa taa ya kirafiki, ambayo hutusaidia kuona mema ndani yetu na kutambua uovu, kubadilisha na kuponya kwa msaada wa neema yake.

Yesu hakuja kuhukumu, bali kuokoa ulimwengu. “Hebu tujifikirie sisi wenyewe, ambao mara nyingi, mara nyingi tunawahukumu wengine; mara nyingi sana kwamba tunapenda maneno mabaya, kutafuta uvumi dhidi ya wengine. Tumwombe Bwana atupe sura hii yote ya huruma, tuwaangalie wengine jinsi anavyotutazama sisi sote.”

Muonekano wa waamini wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 10 Machi 2024
Muonekano wa waamini wakati wa sala ya Malaika wa Bwana 10 Machi 2024

Hata hivyo katika mahubiri yote yaliyotarishwa kwa Dominika hii, Baba Mtakatifu anakazia kusema kuwa: “Ikiwa Kristo hatumii utambuzi wa dhambi zetu kwa kutuadhibu, lakini kwa kutukomboa katika msamaha, na  sisi Wakristo tunaalikwa kufanya hivyo hivyo. Ikiwa Baba hakumtuma Yesu kuhukumu ulimwengu, kwa hakika hakututuma sisi kwa ajili hiyo! Kinyume chake ni hukumu ngapi hasi, ni hukumu ngapi tunazotoa kwa urahisi sana. Lakini anayemjua Yesu na nuru ya wokovu wa Mungu, sio mkuki wa hukumu binafsi.

Kwa hiyo utambuzi na uelewa ambao tunao juu ya wengine sio kwa ajili ya kuwahukumu, lakini ni kwa ajili ya kuwasaidia. Baba Mtakatifu amebainisha kuwa: “Tujiulize kwa hiyo: je mimi ninaacha niokolewe na Yesu, kwa kujiweka mbele na mtazamo wake hasa katika sala na katika kuungama? Na ninapoona vizingiti katika wengine, ninafanyaje? Ninafikiria jinsi ya kuwasaidia au kuwahukumu na kuwasema, ninawahukumu na kuwasengenya? Na ninatambua matukio ya ulimwengu, Je, ninaongeza hasi kwa maoni yangu au ninasali, ninahusika au ninatafuta kufanya kitu?” Maria atusaidie kutamani mema ya mmoja na mwingine.

Tafakari ya Papa 10 Machi 2024: Dominika ya IV ya Kwaresima
10 March 2024, 14:03