Tarehe 5 Machi 2024 Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Pili ya Kimataifa ya Upokonyaji Silaha na Uhamasishaji wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha. Tarehe 5 Machi 2024 Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Pili ya Kimataifa ya Upokonyaji Silaha na Uhamasishaji wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha.   (©Scanrail - stock.adobe.com)

Siku ya Pili Kimataifa ya Upokonyaji wa Silaha Na Uhamasishaji wa Kuzuia Uenezi wa Silaha

Jumanne tarehe 5 Machi 20224, Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Pili ya Kimataifa ya Upokonyaji Silaha na Uhamasishaji wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha. Baba Mtakatifu anasikitika kuona kwamba rasilimali fedha na watu vinatumika vibaya, kwa kuendelea kuwekeza katika matumizi makubwa ya kijeshi na kutokana na hali ilivyo na hivyo wanaendelea kujenga hofu. Upokonyaji wa silaha kimataifa ni wajibu wa kimaadili, ili kuondoa hofu na kujengeana imani.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Tarehe 5 Machi 2024 Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Pili ya Kimataifa ya Upokonyaji Silaha na Uhamasishaji wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha. Kwa mara ya kwanza Siku hii iliadhimishwa tarehe 5 Machi 2023 kwa Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa namba A/RES/77/51 la tarehe 7 Desemba 2022, wazo lililotolewa na nchi ya Kazhstan kupinga majaribio ya Nyuklia ambayo yanaweza kusababisha athari kubwa kwa usalama wa watu na mali zao. Lengo kuu la Siku hii Kimataifa ni kukuza uelewa zaidi wa masuala ya upokonyaji wa silaha miongoni mwa wanachama wa Umoja wa Mataifa. Tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, malengo ya upokonyaji silaha na ukomo wa silaha yamekuwa ni msingi kama njia ya kujenga na kudumisha amani na usalama wa Jumuiya ya Kimataifa. Silaha ya maangamizi na hasa za kinyuklia zinaendelea kusababisha hofu na wasiwasi kutokana na nguvu za uharibifu na tishio linalowakabili binadamu. Malimbikizo ya silaha pamoja na biashara haramu ya silaha ndogo ndogo na nyepesi ni tishio kwa amani na usalama wa Jumuiya ya Kimataifa, ustawi na maendeleo endelevu. Teknolojia mpya zinazoendelea kuibuka kila kukicha kama vile silaha zinazojiendesha zenyewe, zinawakilisha changamoto kwa usalama wa Kimataifa. Kumbe, hii ni siku maalum ya kuongeza uelewa sanjari na kupokea maoni juu ya juhudi za upokonyaji wa silaha ili kuimarisha amani na usalama; kwa kuzuia na kukomesha ulimbikizaji pamoja na biashara ya silaha hasa zile za maangamizi, ili kudhibiti na kupunguza migogoro inayoendelea kumtesa mwanadamu.

Utengenezaji, ulimbikizaji na matumizi ya silaha za nyuklia ni hatari
Utengenezaji, ulimbikizaji na matumizi ya silaha za nyuklia ni hatari

Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Siku ya Pili ya Kimataifa ya Upokonyaji Silaha na Uhamasishaji wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha, Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 3 Machi 2024 mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican amesema kwamba, Jumanne tarehe 5 Machi 20224, Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Pili ya Kimataifa ya Upokonyaji Silaha na Uhamasishaji wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha. Baba Mtakatifu anasikitika kuona kwamba rasilimali fedha na watu vinatumika vibaya, kwa kuendelea kuwekeza katika matumizi makubwa ya kijeshi na kutokana na hali ilivyo na hivyo wanaendelea kujenga hofu. Jumuiya ya Kimataifa inapaswa kutambua kwamba upokonyaji wa silaha ni wajibu wa kimaadili. Hili ni jmbo linalopaswa kukumbukwa na kwamba, ili kupata suluhu na ufumbuzi wa changamoto hii, kuna haja ya kuwa na uwiano mzuri wa kuondokana na hofu ya silaha za maangamizi na hivyo Jumuiya ya Kimataifa kujengeana imani.

Silaha za nyuklia zinatishia usalama wa Kimataifa
Silaha za nyuklia zinatishia usalama wa Kimataifa

Amani inasimikwa katika misingi ya: Ukweli, haki, upendo na uhuru kama anavyofafanua Mtakatifu Yohane XXIII katika Waraka wake wa Kitume “Pacem in terris” yaani: “Amani Duniani.” Kimsingi, watu wanatofautiana kwa mambo mengi sana, lakini kanuni hizi zinaweza kutumika ili kuheshimu na kuwawajibisha wanasiasa, ili kujizatiti katika kudumisha: ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Hii ni changamoto kwa watu wa Mungu kudumisha upendo, kwa kukuza majadiliano yanayofumbatwa katika ukweli na uwazi; mshikamano na matumizi bora zaidi ya nguvu kazi. Amani duniani inahatarishwa sana kutokana na vitisho vya silaha za nyuklia na mchakato wa kuendelea kuwekeza katika biashara na matumizi ya silaha duniani. Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatican wanasema, amani siyo tu kutokuwepo kwa vita, kinzani wala mipasuko ya kijamii bali ni matunda ya haki, maendeleo, mshikamano wa udugu wa kibinadamu, utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote pamoja na kusimamia ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Baba Mtakatifu Francisko anasikitika kusema kwamba, viongozi wa Jumuiya ya Kimataifa wanaendelea kuwekeza sana katika biashara na matumizi ya silaha kama inavyojionesha katika vita inayoendelea sasa kati ya Urusi na Ukraine.

Siku ya Kimataifa
04 March 2024, 14:44