Tafuta

Njia ya Msalaba,Papa asali akiwa Mt.Mtakatifu Marta:upendo una mwanzo mpya

Papa hakuwepo katika Njia ya Msalaba katika Colosseo,Roma na akashiriki akiwa nyumbani,lakini tafakari yake ya kugusa moyo na dhamiri iliyoongoza vituo 14 imejikita katika Mwaka wa Sala na mtazamo wa Yesu anayetoa maisha ili kutuokoa."Kuanguka na kuinuka ni nguvu itokanayo na upendo kwani apendaye hakai,anaanza tena,hachoki,hukimbia na kupaa."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ni mazungumzo na Yesu ambayo Baba Mtakatifu Francisko ameeendeleza katika tafakari ya Njia ya Msalaba siku ya Ijumaa Kuu usiku tarehe 29 Machi 2024 katika Uwanja wa Colosseum,(magofu ya Kale jijini Roma,mahali walipoteseka Wakristo wa kwanza) hata kama Yeye hakuweza kuudhuria kama ilivyotangazwa kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya vyombo vya Habari vya Vatican kwa waandishi wa Habari kwamba: “Ili kulinda afya yake kwa kuzingatia Mkesha na Misa Takatifu ya Dominika  ya Pasaka, jioni ya leo Baba Mtakatifu Francisko atafuatilia Njia ya Msalaba kwenye Uwanja wa Colosseum akiwa nyumba ya Mtakatifu Marta.” Kwa hiyo, aliyemwalikisha alikuwa ni Makamu wake Kardinali Angelo de Donatis. Katika tafakari hiyo kwa hiyo ni mazungumzo ya ana kwa ana na Kristo, yanayojumuisha tafakari, maswali, utangulizi, maungamo, miito. Sala ndefu ya ndani ambayo, katika Mwaka huu wa Sala, unaotangulia kuandaa Jubilei ya 2025 umeruhusu moyo wa mwanadamu kunena hasa.

Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu
Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu

Katika vituo kumi na vinne, kulikuwa na mateso ya Yesu katika safari ya Golgota, makutano kando ya njia ya Uchungu, macho ya upendo ya Maria ambaye chini ya Msalaba alikuwa Mama wa watu wote, wanawake wenye uwezo wa ishara za huruma na za ujasiri katika hali ya kushangaza zaidi, lakini pia hata muda mfupi, Mkirene akiwa tayari kutoa msaada wake kwa Mnazareti aliyehukumiwa kifo;  Yosefu wa Arimathaya ambaye alitoa kaburi ambalo Mungu atashinda kifo, na kuchochea uchunguzi wa dhamiri ambayo inageuka kuwa maombi, na vile vile  maombi ya mwisho ambayo yanarudia jina la Yesu mara kumi na nne!

Tufuate njia ya Msalaba
Tufuate njia ya Msalaba

Katika utangulizi wa tafakari ya Njia ya Msalaba Papa Francisko anabainisha kuwa “Bwana Yesu, tunapoutafakari msalaba wako, tunatambua kwamba ulijitoa mhanga kabisa kwa ajili yetu. Sasa tunachukua muda huu kuwa nawe. Tunataka kuutumia kwa ukaribu na wewe. Ukiwa njiani kutoka Gethsemani hadi Kalvari, hukuacha kusali. Katika Mwaka huu wa Sala, tunakusindikiza katika safari yako ya sala. Kutoka katika Injili ya Marko inabainisha kwamba alikwenda mpaka mahali paitwapo Gethsemane… Yesu akawachukua Petro na Yakobo na Yohane pamoja naye, akaanza kuhuzunika na kufadhaika. Akawaambia, kaeni hapa mkeshe. Akaenda mbele kidogo, akaanguka chini, akaomba…” Aba, Baba, kwako wewe mambo yote yanawezekana; uniondolee kikombe hiki; lakini si kama ninavyotaka mimi, bali kama unavyotaka wewe.” Akaja akawakuta wamelala; akamwambia Petro, “Je, hukuweza kukesha hata saa moja?” (14:32-37).

Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu
Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu

Bwana, ulijitayarisha kwa kila siku ya maisha yako kwa maombi, na sasa, huko Gethsemane, unajitayarisha kwa Pasaka yako. Abba, Baba, kwako mambo yote yanawezekana, wasema, kwa maana sala ni kabla ya mazungumzo na urafiki wa karibu, lakini wakati huo huo pambano na sala: Niepushe kikombe hiki kwangu! Maombi pia ni dhamana na sadaka: Lakini si kama ninavyotaka mimi, bali unavyotaka wewe. Katika maombi yako, ulipitia mlango mwembamba wa mateso yetu ya kibinadamu na kuyapitia kikamilifu. Ulikuwa na huzuni na kufadhaika (Mk 14:33), ukiwa na woga mbele ya kifo, umekandamizwa chini ya mzigo wa dhambi zetu, na kukandamizwa na huzuni isiyoelezeka. Hata hivyo katikati ya pambano hili, ulisali “kwa bidii zaidi”(Lk 22:44), na kwa njia hii ukageuza uchungu wako kuwa sadaka ya upendo. Kwetu, uliomba jambo moja tu: kubaki na wewe na kukesha. Hukuomba kitu kisichowezekana, lakini ukaribu tu. Ni mara ngapi, ingawa, nimepotoka mbali na wewe! Ni mara ngapi, kama wanafunzi, badala ya kukesha, badala yake nimelala usingizi!

Tufuate njia ya Msalaba
Tufuate njia ya Msalaba

Katika kituo cha kwanza, “kinachotufanya tutafakari ni ukimya wa Yesu mbele ya jaribu la uwongo linalomhukumu, ukimya wenye kuzaa matunda ambayo: ni maombi, ni upole, ni msamaha, ni njia ya kukomboa uovu, kubadilisha kile kinachokuja kuteseka katika zawadi iliyotolewa. Ukimya ambao mwanadamu wa leo hii  haujui, kwa sababu hapati wakati wa kusimama na kubaki na Mungu na kuliacha Neno lake litende, lakini hutikisa, kwa sababu unafundisha kwamba sala huzaliwa kutoka katika moyo unaojua kusikiliza.”Anabainisha Papa.

Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu
Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu

Msalaba ambao Kristo analemewa nao katika (kituo cha pili) “unakumbusha uzoefu ambao kila mtu anapitia: maumivu, uchungu, tamaa, majeraha, kushindwa, misalaba ambayo sisi pia hubeba. Yesu, unawezaje kusali huko? Je ukitoa sauti kwa ombi la kawaida, nini cha kufanya unapohisi kulemewa na maisha? Anauliza Papa. “Kristo anatualika tumkaribie, ikiwa tumechoka na kuonewa, ili atupe burudisho, lakini tunacheua, tunazama katika mateso, na kisha Yeye anakuja kukutana nasi, akibeba misalaba yetu mabegani mwake na  utuondolea mzigo huo.”

Njia ya Msalaba
Njia ya Msalaba

Hata hivyo “Yesu anaanguka katika (kituo cha tatu), lakini ana nguvu za kuinuka; nguvu inayomsukuma kusonga mbele ni upendo, kwa sababu apendaye hakai chini, anaanza tena; apendaye hachoki, hukimbia; anayependa huruka." Baba Mtakatifu Francisko wakati akitafakari juu ya kituo cha nne anabainisha kuwa “Baada ya Ekaristi, Kristo anatupatia Maria, zawadi kuu kabla ya kufa kwake. Yesu akiwa njiani kuelekea Kalvari na Mama yake: makabiliano ambayo yanaibua uangalifu na huruma, na ambayo yanatusukuma kumgeukia yeye kwa Maria - Mama ambaye Mungu huwapatia watu wote  kuwa na uwezo wa kulinda neema kumbuka msamaha wa Mungu na maajabu, kufurahia maajabu ya riziki na kulia kwa shukrani.”

Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu
Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu

Papa anatafakari kuwa “Mkirene anayemsaidia Yesu kubeba msalaba katika (kituo cha tano), badala yake anatufanya tutafakari juu ya dhana ya kuufanya peke yake katika kukabiliana na changamoto za maisha. Ni ngumu sana kuomba msaada, kwa kuogopa kutoa maoni ya kutokuwa sawa, tunakuwa waangalifu kila wakati kuonekana wazuri na kujionesha! Si rahisi kuamini, hata kidogo. Wale wanaosali, hata hivyo, wanajua kuwa wana uhitaji”. Papa  Fransisko anaongeza kusema kuwa “ na Yesu, ambaye daima hujikabidhi katika sala, hakudharau msaada wa Mkirene, ambaye ishara yake inafundisha kwamba kuwapenda wengine kunamaanisha kuwasaidia wengine pale pale, katika hali hiyo ya udhaifu wao ambao wanaona aibu.” Miongoni mwa umati unaoshuhudia onyesho la kipuuzi  la kuuawa kwa Mnazareti pia kuna wale wanaotoa hukumu na shutuma, wanaomtupia machafu na dharau bila kumjua na bila kujua ukweli.

Njia ya Msalaba
Njia ya Msalaba

Baba Mtakatifu anatambua kuwa “Inatokea pia leo, inatosha kengele moja ya kutukana na kuchapisha sentensi, lakini huko Yerusalemu, wakati wengi walipiga kelele na kumhukumu Yesu, mwanamke alifanya njia yake ambaye hasemi na akatenda.  Yeye hakukosa huruma bali alishikwa na hurumia. Akaenda kinyume nao peke yake, kwa ujasiri wa huruma, akahatarisha upendo, akatafuta njia ya kupita kati ya askari ili tu kuupa uso wake faraja ya kubembeleza.”Ishara ya faraja, ni ile ya Veronika, (kituo cha sita) ambayo inaingia katika historia na ambayo inatuweka uso kwa uso na Kristo, upendo usiopendwa, ambaye hata leo, anatafuta kati ya umati wa watu wenye mioyo nyeti kwa mateso yake na  maumivu, waabuduo kweli, katika roho na kweli.”

Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu
Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu

Lakini msalaba una uzito, unabeba mzigo wa kushindwa, kudhalilishwa. Kisha Yesu anaanguka kwa mara ya pili (kituo cha saba) na tunajiona ndani yake tunapokandamizwa na vitu, tukilengwa na maisha, kutoeleweka na wengine, kushinikizwa katika mshiko wa wasiwasi na kushambuliwa na huzuni, tunafikiri hatuwezi kuamka tena, au tunaporudi katika makosa yetu na dhambi zetu, tunapopigwa kashfa na wengine na ndipo tunatambua kwamba sisi ni wazimu na  hakuna tofauti. Lakini pamoja na Yesu, tumaini halina mwisho na baada ya kila anguko tunasimama tenea,kwa sababu Mungu hungoja na kusamehe daima, hata kama tunaanguka mara nyingi. Papa Francisko amesisitiza kuwa “Nikumbushe kwamba kuanguka kunaweza kuwa nyakati muhimu za safari, kwa sababu huniongoza kuelewa jambo pekee la muhimu: kwamba ninakuhitaji, Yesu, kwa sababu maisha huanza tena kutoka katika msamaha wa Mungu.”

Njia ya Msalaba
Njia ya Msalaba

Yesu anakutana na wanawake wa Yerusalemu (kituo cha nane) na kwa Papa  Fransisko amesema  “ni fursa ya kuwahimiza kutambua ukuu wa wanawake, wale ambao wakati wa Pasaka walikuwa waaminifu na wa karibu na Kristo, lakini ambao hadi leo hii  wametupwa, wakiteseka na hasira na vurugu. Kilio chao kinatufanya tujiulize ikiwa tunajua jinsi ya kusogezwa mbele ya Yesu, aliyesulubishwa kwa ajili yetu, ikiwa tunalia kwa uwongo wetu au katika misiba, kwa wazimu wa vita, kwenye nyuso za watoto wasiojua tena kutabasamu, kwa akina mama wanaowaona wakiwa na utapiamlo na njaa na hawana machozi tena ya kudondoka.”

Waamini katika Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu
Waamini katika Njia ya Msalaba Ijumaa Kuu

Na tukitafakari juu ya Kristo kwa kuvuliwa nguo zake (kituo cha tisa), mwaliko wa Papa Francisko ni kuona Mungu ameumbwa mwanadamu katika mateso, katika wale waliovuliwa hadhi yao, katika Kristo waliofedheheshwa kwa kiburi na ukosefu wa haki, kwa faida isiyo ya haki iliyopatikana kwa ngozi ya wengine, kwa kutojali kwa ujumla na kuvua mengi ya kijuu juu.” Msalabani, basi, wakati maumivu ya kimwili ni makali zaidi, akiwasamehe wale wanaomtia misumari mikononi mwake” (kituo cha kumi), Yesu anatufundisha kwamba tunaweza kupata ujasiri wa kuchagua msamaha, unaoweka huru moyo na anazindua upya uzima na anatufunulia kimo cha maombi ya maombezi, ambayo yanaokoa ulimwengu.

Katika wakati wa giza na uliokithiri zaidi Yesu alipaza sauti ya kuachwa kwake (kituo cha kumi na moja), Papa anakazia kusema kuwa ni fundisho gani tunapaswa kulithamini? Katika dhoruba za maisha: badala ya kukaa kimya na kukaa ndani, piga kelele kwa Mungu, ambaye katika kituo cha kumi na mbili anazingatia mwizi aliyejikabidhi kwa Kristo, na ambaye naye anamwahidi Mbingu na hivyo kufanya msalaba, uwe nembo ya mateso; picha ya upendo, ikibadilisha giza kuwa nuru, kujitenga kuwa ushirika, maumivu kuwa ngoma na hata kaburi, kituo cha mwisho cha maisha, kuwa mahali pa kuanzia matumaini”, Alipendekeza Baba Mtakatifu  Fransisko.

Watawa katika Njia ya Msalaba
Watawa katika Njia ya Msalaba

Mama Maria ambaye anamkaribisha Yesu aliyekufa mikononi mwake (kituo cha kumi na tatu), mwishoni mwa Njia ya Msalaba Papa anabainisha kuwa “anatusaidia kusema ndiyo tazama mimi hapa kwa Mungu, yeye ambaye mwenye nguvu katika imani, anaamini kwamba maumivu, yakivukwa na upendo, huzaa matunda ya wokovu; na kwamba mateso ya Mungu hayana neno la mwisho. Na hatimaye “Yosefu wa Arimathaya, aliyeweka chini ya ulinzi mwili wa Yesu ili kuupatia maziko yanayostahili (kituo cha kumi na nne) anatuonesha kwamba kila zawadi itolewayo kwa Mungu ina thawabu kubwa zaidi, upendo huo haubaki bila kujibiwa, bali hutoa mwanzo mpya na  kwamba kwa kutoa mtu anapokea, kwa sababu uzima hupatikana wakati umepotea na unamilikiwa unapotolewa.”

29 March 2024, 22:57