Ujumbe wa Papa,vijana,miaka 5 ya Christus Vivit:ninyi ni tumaini hai la Kanisa katika safari!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 25 Machi 2024 ametoa ujumbe wake kwa ajili ya vijana katika fursa ya miaka 5 tangu kuchapishwa kwa Wosia wa Kitume wa Christus vivit uliochapishwa kunako tarehe 25 Machi 2019. Katika ujumbe huo, Baba Mtakatifu anaanza kuandika kwamba: “Wapendwa vijana: Yesu anaishi na anawapenda kuwa hai! Ni uhakika ambao daima unajaza furaha ya moyo wangu na unanisukuma sasa kuwaandakia ujumbe huu, miaka mitano tangu kuchapishwa kwa Wosia wa Kitume wa Christus vivit, tunda la Mkutano wa Sinodi ya Maaskofu ambao ulikuwa na tema: “Vijana, imani na mang’amuzi ya miito.” Awali ya yote, ninapenda maneno yangu yawe chanzo cha kupyaisha tumaini kwenu. Katika muktadha wa sasa wa kimataifa, kiukweli uliogubikwa na migogoro mingi na mateso mengi, ninaweza kufikiria kwamba wengi wenu, wanahisi kukata tamaa. Kwa hiyo ninatamani kuanza pamoja nanyi kutoka katika tangazo ambalo ni msingi wa tumaini kwa ajili yenu na kwa ubinadamu wote kwamba: “Bwana anaishi.”
Kristo anaishi na anakukupenda bila kikomo
Ninasema kwa kila mmoja wenu kwa namna ya pekee: Cristo anaishi na anakupenda bila kikomo. Na upendo wake kwa ajili yako haulazimishwi kwa kuanguka kwako au makosa yako. Yeye ambaye alitoa maisha kwa ajili yako, hasubiri kukupenda, kwa sababu ya ukamilifu wako. Tazama mikono yake iliyofunguliwa juu ya Msalaba na “uache ukombolewe daima upya”, tembea naye kama rafiki, mpokee katika maisha yako na umwache ashirikishane furaha, matumaini, mateso na uchungu wa ujana wako. Utaona kuwa safari yako itaangaziwa na kwamba hata uzito ulio mkubwa zaidi utageuka kuwa hatari kidogo, kwa sababu atakuwa Yeye anayebeba pamoja nawe. Kwa sababu hiyo ninaomba kila siku Roho Mtakatifu ambaye “akufanye uingie daima zaidi katika moyo wa Kristo, ili wewe daima uweze kujazwa zaidi na upendo wake, mwanga wake na nguvu yake.
Mfanye kusikika sauti pia maisha na moyo
Ni kwa jinsi gani ninatamani kuwa tangazo hili liweze kumfikia kila mmoja wenu, na kwamba kila mmoja atambue uhai na ukweli wa maisha yake binafsi na ahisi shauku ya kuushirikisha kwa marafiki zake! Ndiyo, kwa sababu ninyi mna utume mkubwa huu: kushuhudia kwa wote furaha ambayo inazaliwa kutokana na urafiki na Kristo. Mwanzoni mwa Upapa wangu, wakati wa Siku ya Vijana(WYD) huko Rio de Janeiro, niliwaeleza kwa nguvu: “mfanye kusikika”, Hagan lio! Na tena leo hii ninarudi kuwaomba: Mfanye kusikika, pazeni sauti, sio tu na sauti bali na maisha na moyo, wa ukweli huu: Kristo anaishi! Kwa sababu Kanisa liwe na msukumo wa kuamka, wa kijiweka daima kwa upya katika mwendo na kubeba tangazo lake kwa ulimwengu mzima.
14 Aprili ni miaka 40 tangu mwanzo wa WYD
Tarehe 14 Aprili ijayo, tutakumbuka miaka 40 tangu mkusanyiko mkubwa wa kwanza wa vijana ambao katika muktadha wa Mwaka Mtakatifu wa Ukombozi, ulikuwa ni chipukizi cha Siku ya Vijana Duniani ya wakati ujao. Mwisho wa mwaka huo wa Jubilei mnamo 1984, Mtakatifu Yohane Paulo II alikabidhi Msalaba kwa Vijana na utume wa kuupeleka ulimwenguni kote kama ishara na kumbukumbu kuwa ni Yesu aliyekufa na kufufuka tu kuna wokovu na ukombozi. Kama mjuavyo vema, huu unahusu Msalaba wa mbao bila Msulubiwa, ulipendwa namna hiyo ili kutukumbusha kuwa huo unasheherekea hasa ushindi wa Ufufuko, na ushindi wa maisha juu ya kifo, kwa kusema kwa wote: Kwanini mnamtafuta kati ya wafu yule aliye hai? Hayupo hapa amefufuka (Lk 24,5-6). Na ninyi pia mtafakari Yesu namna hiyo aliye: hai na aliyejaa furaha, mshindi wa kifo, rafiki anayewapenda na anayetaka kuishi ndani mwenu. Ni hivyo tu, katika nuru ya uwepo wake, kumbu kumbu ya wakati uliopita italeta matunda na mtakuwa jasiri wa kuishi wakati uliopo na kukabiliana na wakati ujao na tumaini. Mtaweza kuchukua kwa uhuru historia ya familia zenu, babu zenu, wazazi wenu, tamaduni za kidini za nchi zenu ili kuweza kuwa ‘wajenzi wa kesho’, “mafundi” wa siku zijazo.
Wosia wa Christus vivit ni tunda la Kanisa
Wosia wa Christus Vivit ni tunda la Kanisa ambalo linataka kutembea pamoja na kwa hiyo linajiweka katika usikivu, katika mazungumzo na mang’amuzi thabiti katika utashi wa Bwana. Kwa njia hiyo zaidi ya miaka mitano iliyopita, katika matazamio ya Sinodi ya vijana, wengi wenu, kutoka sehemu mbali mbali za ulimwengu waliombwa kushirikishana matarajio binafsi na shauku binafsi. Mamia ya vijana walikuja Roma na walifanya kazi pamoja kwa siku kadhaa, wakikusanya mawazo ya kupendekeza: Shukrani kwa kazi yao, maaskofu waliweza kutambua na kujikita kwa kina katika maono mapana zaidi na ya kina ya ulimwengu na ya Kanisa.
Sinodi ni kipimo cha msingi cha Kanisa
Ulikuwa uzoefu wa kisinodi wa kweli ambao ulileta matunda mengi na ambao uliandaa njia na kwa Sinodi mpya, ambayo tupo tunaishi sasa, katika miaka hii hasa juu ya kisinodi. Kama tunavyosoma kwenye Hati ya Mwisho ya mnamo 2018, kiukweli “Ushiriki wa vijana ulichangia “ kuamsha tena hali ya kisinodi ambayo ni “kipimo cha msingi cha Kanisa.” Na sasa katika hatua mpya ya mchakato wa kikanisa, tunahitaji ubunifu wenu kuliko hapo awali ili kuvumbua njia mpya daima katika uaminifu wa mizizi yenu. Vijana wapendwa, ninyi ni tumaini hai la Kanisa katika safari.” Kwa njia hiyo ninawashukuru kwa uwepo wenu na mchango wenu katika maisha ya Mwili wa Kristo. Na tafadhali: msitukoseshe kamwe kelele zenu nzuri, msukumo wenu kama ule wa injini safi na iliyopangwa vizuri, na njia yenu halisi ya kuishi na kutangaza furaha ya Yesu Mfufuka. Kwa njia hiyo ninasali, na hata ninyi tafadhali msali kwa ajili yangu.