Tafuta

Upendo wa Papa kwa Watoto Upendo wa Papa kwa Watoto  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:tokomeza hali zinazolinda wanaotumia nafasi zao kama ngao!

Katika Kongamano la III la Amerika ya Kusini linaloendelea Panama kwa lengo la kukuza utamaduni wa kutunza na kuheshimu haki za watu linaongozwa na:"Udhaifu na unyanyasaji.Kuelekea maono mapana zaidi ya kuzuia.Katika ujumbe uliotumwa kwa washiriki Papa anasisitiza haja ya mabadiliko kamili ya mawazo katika dhana mahusiano yanayozingatia upendeleo wadogo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe wake kwa washiriki wa Kongamano la Tatu la Amerika ya Kusini linaloendelea katika mji mkuu wa Jamhuri ya Panama, kuanzia tarehe 12 hadi 14 Machi 2024, Baba Mtakatifu Francisko anarejea mkutano na Wajumbe kutoka Baraza la  Amerika Kusini ya Kati “Juu ya Uchunguzi na mafunzo kwa ajili ya Ulinzi wa Watotokatika  Kituo cha Utafiti na Mafunzo kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto,” mnamo   tarehe 25 Septemba 2023 Jijini Roma. Baba Mtakatifu akikumbuka hotuba yake alikuwa amesisitiza dhamira ya Kanisa ya kuona katika kila mmoja wa waathirika uso wa Yesu anayeteseka, lakini pia haja ya kuweka chini ya miguuni yake mateso ambayo tumepokea na yaliyosababishwa, huku wakiwaombea  watenda dhambi wasio na furaha na waliokata tamaa, uongofu wao. Kwa njia hiyo Ujumbe wa Papa Francisko  katika Kongamno hilo lenye kuongozwa na kauli mbiu: “Udhaifu na Unyanyasaji: kuelekea maono mapana ya kuzuia”  alimkabidhi Bwana ili kazi yao iweze kuendelea mbele katika kutokomeza janga la nyanyaso katika maeneo yote ya jamii.

Neema ya Bwana ni zawadi lazima tuiombe

Baba Mtakatifu amebainisha kwamba: “Mungu anatuita tubadilike kabisa kifikra juu ya dhana yetu ya mahusiano, kwa kupendelea udogo, maskini, mtumishi, mjinga kuliko kuwa mkuu, tajiri, bwana, mwenye elimu, na ili kuwa na  uwezo wa kukaribisha neema ambayo tunapewa na Mungu na kujifanya kuwa zawadi kwa ajili ya wengine. Kuona udhaifu binafsi kama kisingizio cha kuacha kuwa watu wa maana na Wakristo wanyoofu, wasio na uwezo wa kudhibiti hatima binafsi, kutaunda utoto wenye kiburi, na kwa njia yoyote hauwakilishi udogo ambao Yesu anatualika kuwa nao. Kinyume chake, nguvu za Yule ambaye kama Mtakatifu Paulo anajivunia udhaifu wake mwenyewe na kutumaini neema ya Bwana (taz. 2 Kor 12:8-10) ni zawadi ambayo ni lazima tuiombe kwa kupiga magoti yetu kwa ajili yetu na kwa ajili ya wengine.Katika hayo, tutaweza kukabiliana na kinzani za maisha na kutoa mchango kwa manufaa ya wote katika wito ambao tumeitiwa.”

Kutokomeza hali zinazolinda wanaotumia nafasi zao kama ngao

Na kwa mtazamo wa kuzuia, Baba Mtakatifu amebanisha kwamba bila shaka kazi yao inalenga kutokomeza hali zinazowalinda wale  watu wanaotumia nafasi zao kama ngao kujilazimisha kwa njia potovu, lakini pia kuelewa kwa nini hawawezi kuhusiana na wengine kwa njia nzuri. Vivyo hivyo, sababu inayofanya wengine wakubali kwenda kinyume na dhamiri zao, kwa woga, au kujiruhusu kudanganywa na ahadi za uwongo, wakijua ndani kabisa ya mioyo yao kwamba haiwezi kutojali lakini wako kwenye njia mbaya.”

Uhusiano wa kibinadami kwa kila jamii, na hata Kanisa ni kufanya kazi kwa ujasiri

Baba Mtakatifu ameendelea kueleza kuwa “Uhusiano wa kibinadamu katika kila jamii, hata katika Kanisa, unamaanisha kufanya kazi kwa ujasiri ili kuunda watu waliokomaa, walioshikamana ambao, wakiwa thabiti katika imani yao na kanuni za maadili, wanaweza kukabiliana na uovu, wakishuhudia ukweli kwa herufi kubwa. Jamii ambayo haijaegemezwa katika dhamira hizi za uadilifu wa kimaadili itakuwa jamii ya wagonjwa, yenye uhusiano wa kibinadamu na wa kitaasisi uliopotoshwa na ubinafsi, kutoaminiana, woga na udanganyifu. Lakini tunakabidhi udhaifu wetu kwa nguvu ambazo Bwana anatupatia. Na tutambue kwamba “hazina hii tunayo katika vyombo vya udongo, ili ionekane kwamba uwezo huu usio wa kawaida hutoka kwa Mungu wala si kutoka kwetu” (2Kor 4:7). Tunamwombe Mfalme wa mashahidi neema hii ili kuwa mashahidi wake duniani. Bwana awabariki na Bikira Mtakatifu awalinde. Na tafadhali wasisahau kumuombea. Papa amehitimisha Ujumbe wake.

Papa Francisko alituma Ujumbe wake kwa washiriki wa Mkutano huko Panama
12 March 2024, 18:23