Tafuta

Shirikisho la Mchezo wa Draft “ Dama, Checkers” la Italia lilianzishwa mnamo 1924 huko Milano, na Bwana Luigi Franzioni na wengineo. Shirikisho la Mchezo wa Draft “ Dama, Checkers” la Italia lilianzishwa mnamo 1924 huko Milano, na Bwana Luigi Franzioni na wengineo.  (Vatican Media)

Jubilei ya Miaka 100 ya Shirikisho la Mchezo wa Draft Nchini Italia

Papa amewapongeza kwa kuendeleza mchezo huu ambao ni maarufu sana miongoni mwa wakimbizi. Katika mateso na mahangaiko yao mengi, wanapata faraja kucheza mchezo wa Darft, huku wakishirikiana na wenyeji wao, wanaowapatia faraja na ukarimu na kama sehemu ya ushirikiano. Huu ni mchezo unaoimarisha akili na hivyo kumwezesha mchezaji kukuza kipaji cha mantiki, kwani matumizi haramu ya michezo mingine yanaifanya akili "kusinzia."

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Shirikisho la Mchezo wa Draft “ Dama, Checkers” la Italia lilianzishwa mnamo 1924 huko Milano, na Bwana Luigi Franzioni na wengineo, na mnamo mwaka 1993 lilitambuliwa na Kamati ya Olimpiki ya Italia, CONI. Mchezo wa draft ni miongoni mwa michezo inayovuta hisia za watu wengi sana “vijiweni.” Huu ni mchezo unaochangamsha sana akili na kwamba, watu wengi wanaweza kuushiriki. Ni mchezo unaohitaji akili, uwezo wa kufikiri na kwamba, hauhitaji miundo mbinu mikubwa na kwamba, unaweza kuchezeka mahali popote pale ulipo! Ni mchezo unaowezesha kutekeleza utamaduni wa watu kukutana na kukaa kwa pamoja. Ni katika hali na mazingira kama haya, unawezesha mchezo wa Draft kuwa ni kwa ajili ya wote na kwamba, ni mchezo ambao umeenea sehemu mbalimbali za dunia!

Jubilei ya Miaka 100 ya Shirikisho la Mchezo wa Draft Italia
Jubilei ya Miaka 100 ya Shirikisho la Mchezo wa Draft Italia

Shirikisho la Mchezo wa Draft la Italia mwaka 2024 linaadhimisha Jubilei ya Miaka 100 tangu kuanzishwa kwake. Ni katika mukadha wa maadhimisho haya, Wajumbe wa Shirikisho la Mchezo wa Draft la Italia, Ijumaa tarehe 26 Aprili 2024 wamekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Baba Mtakatifu katika hotuba yake, amewapongeza kwa kuendeleza mchezo huu ambao ni maarufu sana miongoni mwa wakimbizi na wahamiaji. Kwa hakika katika mateso na mahangaiko yao mengi, wanapata faraja kucheza mchezo wa Darft, huku wakishirikiana na wenyeji wao, wanaowapatia faraja na ukarimu na kama sehemu ya ushirikiano hata katika mambo madogo madogo. Huu ni mchezo unaoimarisha akili na hivyo kumwezesha mchezaji kukuza kipaji cha mantiki, kwani matumizi haramu ya michezo mingine yanaifanya akili kusinzia.

Mchezo wa Draft unavuta hisia za watu wengi hasa "vijiweni."
Mchezo wa Draft unavuta hisia za watu wengi hasa "vijiweni."

Baba Mtakatifu amesema, imekuwa kwake ni furaha ya kuweza kukutana nao, ili kufahamiana sanjari na kuwapatia changamoto ya maisha ya michezo, ili kuondokana na tabia ya uchoyo na ubinafsi, hali ambayo inaweza kuwatumbukiza watu katika upweke hasi, lakini kwa njia ya michezo, kunaboresha mazingira na hali ya hewa. Baba Mtakatifu amewatakia heri na mafanikio mema katika mchezo huu na anawatia shime kuendelea kuupyaisha hata kwa njia ya maisha ya kiroho; utamaduni unaotekelezwa na Shirikisho la Mchezo wa Draft wakati wa matukio makuu.

Mchezo wa Draft

 

26 April 2024, 15:16