Kitabu cha kumbukumbu ya Francisko kuhusu Benedikto XVI:“Alikuwa kama Baba"
VATICAN NEWS
Benedikto alikuwa mtu mkuu kwa upole. Katika kesi nyingine baadhi ya watu walimtumia, labda bila ubaya, na walipunguza harakati zake. Kwa bahati mbaya, kwa maana nyingine, walikuwa wanamzunguka. Alikuwa ni mtu nyeti sana, lakini hakuwa mdhaifu, alikuwa mwenye nguvu. Lakini kwake mwenyewe alikuwa mnyenyekevu na alipendelea kutojilazimisha. Kwa njia hiyo aliteseka sana. Haya ni baadhi ya meneno ambayo Papa Francisko anayakumbuka ya Mtangulizi wake Benedikto XVI, katika kitachu cha mahojiani na Mwandishi Javier Martínez-Brocal (“El Sucesor”, Editorial Planeta), kitakachochapishwa Jumatano tarehe 3 Aprili 2024.
“Aliniacha nikue na alikuwa na uvumilivu”, anaeleza Papa Francisko. Na ikiwa aliona jambo lisilo sawa, alikuwa anafikiria mara tatu, au mara nne kabla ya kuniambia. Aliniacha nikue na alinipatia uhuru wa kuchukua maamuzi. ” Papa amesimulia, uhusiano ambao alifanya uzoefu wa karibu ya miaka 10 ya kuishi mjini Vaticani, na Papa Mstaafu kwamba: “Aliacha huru na hakuniingilia kamwe.”
Katika fursa ambayo kulikuwa na maamuzi ambayo hakuelewa, aliniomba maelezo kwa namna ya kawaida kabisa. Alinieleza: “Tazama sikuelea hilo, lakini maamuzi yako mikononi mwako,” na mimi nilimweleza sababu na yeye alifurahi.” Papa Francisko katika kitabu ameeleza kwamba mtangulizi wake kamwe hakuwahi kupinga uamuzi wake wowote kwamba: “Hakuwahi kuniondolea msaada wake. Labda kulikuwa na jambo ambalo hakulikubali, lakini hakulisema kamwe.”
Papa Francisko aidha alikumbuka wakati mwingine hata katika kumuaga Papa Mstaafu Benedikto XVI, Jumatano tarehe 28 Dicembre 2022, alipomuona kwa mara ya mwisho kwamba: “Benedikito alikuwa amelala kitandani. Alikuwa bado na fahamu, lakini alishindwa kuzungumza. Alinitazama, alinishika mkono, alikuwa anaelewa kile ambacho ninasema, lakini hakuweza kueleza neno lolote. Nilibaki kwa muda kitambo, kwa kumtazamo na kumshika mkono. Ninakubuka kabisa macho yake mang’avu… Nilimwambia maneno machanche kwa upendo na limbariki. Na kwa namna hiyo tuliagana naye.”
Kwa upande wa mwendelezo kati ya upapa, Papa Francisko alisema kuwa: “Kile ambacho ninaona kwa Mama wa mwisho… ni kwamba kila mfuasi daima amekuwa na alama ya mwendelezo, mwendelezo na tofauti,” kwa sababu katika mwendelezo wa kila mtu umepelekea karama yake binafasi… daima kuna mwendelezo na hakuna mpasuko.”
Papa Francisko amekumbuka na kusimulia kesi maalum ambazo alitetewa na Papa Benedikto XVI: “Nilipata mazungumzo mazuri sana na yeye wakati alikuwa Kardinali na nilikwenda kukutana naye kwa kushangazwa na maneno yake juu ya ndoa, kwa wanandoa ambapo Yeye alikuwa wazi kabisa na wao. Siku moja walifika nyumbani kwake ili kunishtaki mbele yake eti nilihamasisha ndoa za mashoga. Papa Benedikito hakuwa na wasi wasi kwa sababu alikuwa anajua kabisa kile ambacho mimi ninafikiri. Yeye aliwasikiliza wote, mmoja baada ya mwingine, na kuwatuliza kwa kuwaelezea kila kitu. Ni mara hiyo ambapo aliwaeleza kwamba ‘kwa kuwa ndoa ni sakramenti’, haiwezekani kutolewa kwa watu wawili mashoga, lakini kwa namna fulani ilikuwa ni lazima kutoa dhamana fulani au ulinzi wa raia kwa hali ya watu hawa.”
Hii ni kwamba “Nilisema kuwa Nchini Ufaransa kuna mtindo mmoja wa ‘vyama vya kiraia” ambao kwa mtazamo unaweza kuwa mbadala mwema, kwa sababu hautazami ndoa. Kwa mfano- nilifikiri- inawezekana kuwakaribisha wazee watatu waliostaafu ambao wanahitaji kushirikishana huduma za kiafya, urithi, makazi na mengine. Nilikuwa nina maana ya kusema kuwa, hii ilionekana kama suluhisho la kupendeza kwangu. Baadhi walikwenda kumwambia Benedikto kwamba mimi nilikuwa nahamaisha uzushi. Yeye aliwasikiliza kwa makini sana na kuwasaidia kutofautisha mambo… Aliwambia wao kuwa: “Huu siyo uzushi.” Ni kwa jinsi gani alinitetea!... Daima alinitetea.” Papa amebainisha.
Papa Francisko aidha katika mahojiano hayo pia alijibu swali la mwandishi katika kitabu kwa mtazamo wa kifo cha Papa Mstaafu. Papa alijibu: “Walinisababishia maumivu makali: ambapo baada ya mazishi kesho yake wakachapisha kitabu ambacho waliniweka chini juu, wakisimulia mambo yasiyo ya kweli, ni huzuni sana. Hata hivyo sishangai, kwa maana kwamba hayaniathiri. Lakini yalinifanya vibaya kwa namna ambato Benedikto alivyotumiwa. Kitabu kilichapishwa siku ya mazishi na nilipata uzoefu kama ukosefu wa heshima na ubinadamu.”
Hatimaye, Papa Francisko alionesha wazi kwa mwandishi Javier Martínez-Brocal kuwa tayari amekwisha fanya marekebisho kuhusiana na mazishi ya kipapa yajayo huku akielezea kwamba lwa jinisi ya mkesha wa mazishi ya Papa Benedikto XVI yalivyokuwa yalikuwa ya mwisho kuhusu mwili kuwekwa juu ya Geneza na catafalque na mto. Kwani ameeleza kwamba: “Mapapa waangaliwe na kuzikwa kama kila mtoto wa Kanisa. Kwa hadhi, kama ilivyo kwa kila mkristo.”