Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko ameungana na viongozi mbalimbali Kusini mwa Afrika kutuma salam zake za rambirambi, kufuatia vifo vya watu 45 vilivyotokea nchini Afrika ya Kusini. Baba Mtakatifu Francisko ameungana na viongozi mbalimbali Kusini mwa Afrika kutuma salam zake za rambirambi, kufuatia vifo vya watu 45 vilivyotokea nchini Afrika ya Kusini.  (AFP or licensors)

Watu 45 Wafariki Dunia Afrika ya Kusini kwa Ajali Barabarani

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Sherehe ya Dominika ya Huruma ya Mungu, tarehe 7 Aprili 2024 wakati wa Sala ya Malkia Mbingu, ameungana na viongozi mbalimbali Kusini mwa Afrika kutuma salam zake za rambirambi, kufuatia vifo vya watu 45 vilivyotokea nchini Afrika ya Kusini. Katika ajali hii, mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 ndiye aliyenusurika na kwamba, anaendelea na matibabu. Viongozi wengi wametuma salam zao za rambirambi Botswana.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S., Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Sherehe ya Dominika ya Huruma ya Mungu, tarehe 7 Aprili 2024 wakati wa Sala ya Malkia wa Mbingu, ameungana na viongozi mbalimbali Kusini mwa Afrika kutuma salam zake za rambirambi, kufuatia vifo vya watu 45 vilivyotokea nchini Afrika ya Kusini, baada ya dereva wa Bus kushindwa kulimudu Bus, akajikuta akigonga kingo za daraja la Mmamatlakala na hatimaye, Bus likatumbukia chini urefu wa mita 50. Katika ajali hii, mtoto msichana mwenye umri wa miaka 8, ndiye pekee aliyenusurika na anaendelea na matibabu. Bus hili lilikuwa linasafiri kutoka Gaborone mji mkuu wa Botswana kuelekea mjini Moria Makao makuu ya Kanisa la Kikristo la Zion kama sehemu ya maadhimisho ya Sherehe ya Pasaka ya Bwana kwa mwaka 2024.

Ajalibarabarani yasababisha watu 45 kupoteza maisha Afrika ya Kusini
Ajalibarabarani yasababisha watu 45 kupoteza maisha Afrika ya Kusini

Baba Mtakatifu Francisko ana waalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuendelea kuwasindika ndugu zao kwa sala na sadaka zao za maisha katika kipindi hiki cha majonzi mazito. Wakati huo huo, Rais Mokgweetsi Masisi wa Botswana ametuma salam za rambirambi kwa ndugu na jamaa wa marehemu na Kanisa la Kikristo la Zioni katika ujumla wake. Naye Rais Cyril Ramaphosa ametuma salam za rambi kwa Serikali ya Botswana kufuatia ajali hii. Wachunguzi wa mambo wanasema ajali barabarani zinazidi kuongeza maradufu nchini Afrika ya Kusini. Takwimu zinaonesha kwamba, katika Kipindi cha Pasaka ya Mwaka 2023 kuna watu zaidi ya 200 walipoteza maisha kutokana na ajali barabarani. Uchunguzi wa kina unaendelea kufanywa ili kubaini chanzo cha ajali hii mbaya iliyopelekea watu 45 kupoteza maisha.

Ajali Afrika ya Kusini
08 April 2024, 16:03