Iran,rambirambi za Papa kwa kifo cha Rais Raisi
Vatican News
Papa Francisko alituma telegram ya rambirambi kwa kuondokewa na Rais wa Iran Ebrahim Raisi, iliyotumwa kwa Grand Ayatollah Sayyed Ali Hosseini Khamenei, kiongozi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Katika salamu hizo Papa anaandika: “Ninatuma salamu za rambirambi kwa kifo cha Rais Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje, Hossein Amir-Abdollahian na wote waliopoteza maisha katika ajali ya helikopta iliyotokea 19 Mei 2024.” Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anazikabidhi “roho za marehemu kwenye rehema za Mwenyezi" na "na sala za kuwaombea wale wanaoomboleza msiba wao, hasa familia zao, natuma hakikisho la ukaribu wa kiroho kwa Taifa katika wakati huu mgumu".
Ajali hiyo
Ndege aliyokuwa akisafiria Rais Raisi, pamoja na watu wengine wanane, akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje, Amir-Abdollahian, ilianguka jana katika milima ya kaskazini-magharibi mwa Azerbaijan, alikokuwa akirejea. Mkia wa helikopta pekee ndio uliobaki ukiwa mzima, huku chumba cha marubani kikiwa kimeteketea. Kuhusu ajali hiyo bado haujawekwa wazi japo inasadikiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo inadaiwa kuwa ni kutokana na hali mbaya ya hewa inayoendelea katika eneo hilo na kufanya shughuli za uokoaji kuwa ngumu sana ambazo zilianza mara baada ya maafa hayo.zaidi ya timu 70 kazini. Ndege isiyo na rubani iliyotumwa kutoka Uturuki ilitambua eneo la ajali.
Sherehe za mazishi
Mazishi yamefanyika tarehe 21 Mei 2024, mchakato mrefu wa sherehe za mazishi ya rais ulianza na sherehe ya kwanza mjini Tabriz. Safari hiyo itakamilika siku ya Alhamisi 23 Mei mjini Mashhad, wakati mabaki ya Raisi yatakapofika kwenye Madhabahu ya Imam Reeza, msikiti mkubwa zaidi duniani kwa eneo. Mazishi ya kwanza yatafanyika Tabriz, jiji lililo karibu na eneo la ajali; jioni, kutakuwa na sherehe ya mazishi huko Qom, mahali ambapo Raisi mchanga alifunzwa katika seminari. Siku ya Jumatano, sherehe hizo zitahamia mji mkuu Tehran, kama Makamu wa Rais Mahsen Mansouri alivyotangaza kwenye televisheni. Asubuhi ya 23 kusini mwa Khorasan kabla ya kuwasili kwenye madhabahu ya Imam Reza.