Tafuta

2024.05.24 Papa amekutana na Vijana katika vitongoji vya jiji la Roma. 2024.05.24 Papa amekutana na Vijana katika vitongoji vya jiji la Roma. 

Papa akutana na vijana wa Roma:kujitoa ni ujumbe wa matumaini!

Papa Francisko katika parokia ya MtakatifuBernadette katika vitongoji vya Roma vya Colli Aniene amekutana karibu saa moja katika mazungumzo na vijana 80,makatekista,skauti na wahuishaji juu ya mada za wito,sala,ushuhuda wa Kanisa na mashaka ya imani:"Ni safari.Hakuna mtu anayepaswa kuhukumiwa kama haamini."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, alitembelea Parokia moja pembezoni mwa jiji la Roma siku ya Ijumaa alasiri  tarehe 24 Mei 2024 kwa ajili ya  mkutano na kundi la vijana wa kike na kiume  wanaojiandaa kusherehekea Jubilei ya 2025. Kwa mujibu wa Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican  ilitoa taarifa  kwamba kwa kusindikizwa na Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti Mwakilishi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji mkutano huo ulifanyika ndani ya mpango wa Mwaka wa Sala ambao unawatayarisha hata  vijana wa Kikatoliki kwa ajili ya  Jubilei 2025.  Kwa hiyo wakiwa katika Parokia ya Mtakatifu Bernadette Soubirous katika kitongoji cha mji wa Roma  mashariki, Papa alipata fursa ya  kujibu maswali aliyoulizwa na vijana kuhusu maisha yao ya imani na maombi.

Papa akutana na vijana wa Parokia ya Mtakatifu Bernadetta mjini Roma
Papa akutana na vijana wa Parokia ya Mtakatifu Bernadetta mjini Roma

Mkutano huu unakuja baada ya mkutano wake wa tarehe 11 Aprili na watoto 200 wanaojiandaa kwa Komunyo ya Kwanza katika Parokia ya Mtakatifu Yohane  Maria Vianney jijini Roma.  Katika taarifa kwa vyombo vya habari aidha ilibainisha kwamba kuwasili kwa Papa katika jumuiya ya parokia hiyo ilikuwa mshangao na kwamba alikaribishwa kwa furaha na vijana waliokusanyika katika  mkutano wa kila Juma. Kikundi hicho kilijumuisha makatekista, viongozi wa vikundi vya vijana, na skauti, ambao wapata fursa ya kukaa  naye na kuuliza maswali kadhaa.

Kwa mfano kijana Tiziano, alimwuliza Papa jinsi gani ya ya kutambua wito. Papa Francisko alijibu kuwa: “Kila mmoja wetu lazima aulize swali hili, kwa sababu Bwana ana mpango kwa kila mmoja wetu. Kila mtu lazima ajaribu kuelewa kile ambacho Bwana anataka kutoka kwetu na kumwomba.” Kwa njia hiyo Papa alishirikisha  uzoefu wake kama kijana ambaye alianza kufanya kazi alipoingia seminarini: “Muulize Bwana katika sala: je unataka nini kutoka kwangu?” Papa pia alisisitiza umuhimu kwa vijana kamwe wasitembea peke yao na kukuza urafiki. “Wakati mwingine tunaweza kupotea kwenye njia isiyo ya kutokea( labyrinths)katika maisha. Jambo kuu la kutoka katika wakati wa giza siyo kutembea peke yako, kwa sababu peke yako unapoteza mwelekeo. Ni muhimu kuzungumzia hali yako,” Papa Francisko alifafanua.

Wakati wa maswali na majibu na vijana
Wakati wa maswali na majibu na vijana

Kwa kijana aliyekiri kutomwamini Mungu, Papa alikazia umuhimu wa kufanya safari kwamba: “Hakuna anayehukumiwa ikiwa haamini. Ni muhimu kuwa katika harakati. Nikiona kijana ambaye hasogei, ambaye amekaa tu maishani, na ambaye hapendi kuhama, inasikitisha. Lakini nikiona kijana ambaye anaanguka katika hali ya kutojali kisha akasonga mbele, simchukii Anasonga mbele kwa mawazo yaliyo bora.”

Papa akiwa anaandika jambo nyuma ya mgogo wa kijana
Papa akiwa anaandika jambo nyuma ya mgogo wa kijana

Katika mazungumzo pamoja na wenzi wa ndoa vijana, Papa pia alionesha hangaiko lake kuhusu kupungua kwa idadi ya watoto wanaozaliwa nchini Italia na umuhimu wa kutoa uhai, ambao, alisema: “sikuzote ni ujumbe wa Tumaini kuu.” Kwa njia hiyo Papa alijikita kwa muda mrefu na  mada aliyoipenda kuhusu  kuzaliwa kwa watoto, huku akipata msukumo kutoka kwa Benedetta mtoto mdogo ambaye alikuwa akizunguka-zunguka chumbani. Papa Francisko aliwahoji wazazi, wa mtoto huyo Stefano na Silvia, ambao walishirikisha  matatizo ya uzazi na pia "shaka kubwa" kwa ajili ya maisha ya baadaye ya binti wao katika ulimwengu wa leo hii.  Wakati huo huo, msichanamdogo  alisimama akisikiliza ambapo Papa alisema: “ Tazameni jinsi anavyojua kwamba wanazungumzia juu yake,” hivyo Papa alitabasamu.  Hata hivyo: “Kama mtu angefikiria kuwa na mtoto, kwa hofu, na vita, hangeweza kufanya hivyo. Lakini pamoja na magumu yote naweza kusema kwamba inafaa... Furaha inayotupa haielezeki,” hayo yalielezwa na Stefano baba wa mtoto huyo.

Nje ya Parokia alilakiwa na watu kadhaa
Nje ya Parokia alilakiwa na watu kadhaa

Papa Francisko, kama ilivyo mara nyingi, alisisitiza wasiwasi wake juu ya kiwango cha kuzaliwa nchini Italia ya zamani inayoendelea, na pia katika nchi kadhaa za Ulaya. Kisha alisisitiza umuhimu wa kuwa na watoto ambayo daima ni ujumbe wa matumaini makubwa.” Watoto ni  matumaini  huku akionesha msichana mdogo kwamba  yeye ni matumaini. Matumaini ni watoto. Ni kweli kwamba mtu anafikiria juu ya siku zijazo. Ni kweli ni hatari, lakini ni hatari zaidi kutokuwa nao. Ni hatari kwa jamii.” Hatimaye, alisema kwamba ili Kanisa lisadikike, “lazima lijivue mbali na ulimwengu wote. Kanuni za Kanisa ni zile za Injili, si zile za jamii inayojiita Katoliki.” Kabla ya kuhitimisha, Baba Mtakatifu Francisko aliwashukuru wote waliohudhuria na kuwapatia   kila mmoja nakala ya hati ya Tangazo la Jubilei  2025, katika toleo jipya na utangulizi wa Askofu Mkuu Rino Fisichella, Mwenyekiti Mwakilishi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji. Aliwashukuru kwa Ushuhuda wao na kufuaria ukweli waho huku akiwatakia waendelee kuwa waaminifu daima wakitafuta njia ya uzima.

PAPA KWA VIJANA KATIKA PAROKIA YA ROMA

 

24 May 2024, 20:15