Papa amekutana na kikundi cha watoto wa Ukraine na Palestina katika tukio la GMB
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Watoto wasio na miguu au mikono. Hofu isiyo na hatia walisimama kimya mbele ya Papa Francisko Jumamosi tarehe 25 Mei 2024, kwa furaha kwa saa moja katika siku ambayo watoto waliweza kupanua macho yake kwa kushangaa katika jengo zuri na sio kwa hofu kwamba bomu kubwa linaweza kurarua kipande cha mwili, familia, maisha. Kwa njia hiyo ilikuwa ni takriban watu thelathini walisimama karibu na Papa Francisko kutoka Ukraine, Palestina, Belarus na Indonesia. Haya yalizungumzwa na Padre Marcin Schmidt, Katibu mkuu wa Mfuko wa 5P Kimataifa, ambao uliwaruhusu watoto hawa kuja jijini Roma kwa Siku ya I ya Watoto Duniani. Akizungumza na Vyombo vya habari Vatican baada ya mkutano huo, Padre Schmidt alisema kuwa “Baba Mtakatifu alitukaribisha kwa tabasamu kubwa na furaha kuu, kile unachoweza kuona, kama babu wa kweli akiwakumbatia wajukuu zake.”
Wakati wa kusikilizwa, uwasilishaji wa Padre Schmidt wa watoto kwa Papa Francisko kutoka nchi kadhaa, tulikuwa na watoto kutoka Ukraine, kutoka hospitali ya (huko Lviv - ed.). Hawa ni watoto waliopoteza miguu, mikono na hata wazazi wao. Na wako hapa na madaktari wao, ni madaktari wazuri sana waliookoa maisha yao."Alisema Padre huyo. Pia katika kundi hilo kulikuwamo na Yana, msichana ambaye alikimbia mbio za Marathon huko Boston mwezi mmoja uliopita akiwa na miguu ya bandia. "Watoto wa kiukraine hawatabasamu,” Papa Francisko alisisitiza tena. Bado Yana anajumuisha "tumaini", nguvu ya ujasiri ambayo inataka kuamini katika upeo mzuri licha ya kila kitu. Licha ya upande wa giza wa sarafu, kwamba - Padre Schmidt alimkumbusha Papa “juu ya shimo la watoto la kuuzwa kwa viungo vya wazazi wanaowauza kama chips za biashara.”
Hata hivyo lakini tarehe 25 na 26 Mei 2024 ndiyo siku kuu ya sherehe kubwa ya watoto na ya kikundi hicho kilichotabasamu na Papa Francisko kama ilivyo kwa watoto pekee wanaoweza kufanya licha ya ubaya wa ulimwengu. “Pia tunaye hapa Waziri wa Haki za Watoto ambaye ndiye mwandishi wa Mkataba wa Haki za Watoto Duniani, aliyefanya kazi Syria. Na ndiyo tuzo pekee duniani inayotolewa na watoto,”aliorodhesha tena Padre Schmidt, akikumbuka kwamba Papa alipokea tuzo hiyo hiyo miaka minne iliyopita. “Tunawashukuru sana kwa kutupokea hapa, asante kutoka ndani ya mioyo yetu,” alirudia Padre Schmidt na Papa alijibu kwa Kiukraine: "Slava Isusu Khrystu” “Sifa kwa Yesu Kristo.”