Papa atakuwa Luxembourg na Ubelgiji kuanzia tarehe 26-29 Septemba 2024
Vatican News
Mwezi Septemba, ambao utafunguliwa kwa ziara ya Kitume ya Indonesia, Papua New Guinea, Timor-Lest na Singapore, utamalizika kwa safari nyingine ya kimataifa kwa Baba Mtakatifu Francisko kwenda Ubelgiji na Luxembourg. Kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Vatican, Jumatatu tarehe 20 Mei 2024 imethibitisha ziara ya Baba Mtakatifu katika nchi hizo mbili za Ulaya kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba 2024.
Katika taarifa hiyo imethibitisha kuwa: “Kwa kukaribisha mwaliko wa Wakuu wa Nchi na mamlaka za kikanisa, Baba Mtakatifu Francisko atafanya Ziara ya kitume huko Luxembourg na Ubelgiji, kuanzia tarehe 26 hadi 29 Septemba 2024, akielekea Bruxelles, Leuven na Louvainla- Neuve”. Na zaidi tunasoma katika maelezo ya Vatican kwa mujibu wa msemaji wa Vyombo vya habari Dk. Matteo Bruni kwamba: “Ratiba ya safari hiyo itachapishwa kwa wakati unaofaa.”
Papa mwenyewe alizungumza kuhusu safari ya Ubelgiji wakati wa mahojiano na shirika la utangazaji la Mexico N+ mnamo Desemba 2023. Akizungumzia kuhusu safari iliyokatishwa ya kwenda Dubai kutokana na maumivu ya mguu na uwezekano wa safari za siku zijazo, ambapo Papa Francisko alieleza kwamba, “wakati safari nyingine bado zinaendelea kufanyiwa utafiti, moja nchini Ubelgiji ilikuwa na uhakika.”