Ujumbe wa Papa kwa wanajeshi huko Lourdes:Huduma ya amani katika giza la kihistoria!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Imekuwa ni utamaduni ambao ulianza miaka 64 iliyopita na kila wakati ni wa kusisimua kwa kile ambacho kinaibua mwonekano wa maelfu ya sare mbalimbali zilizopangwa kwenye sala mbele ya Grotto ya Massabielle huko Lourdes nchini Ufaransa. "Kwa askari anayechagua kupiga magoti wakati wa maisha yake mbele ya Mama Yetu wa Lourdes, kwa wito wa kijeshi ni wazi ambapo popote mnapotumwa toeni ushuhuda wa Injili kati yenu!" Ndivyo Baba Mtakatifu ameandika Ujumbe wake uliotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, wakati wa afla ya hija ya kila mwaka ya kimataifa kwa maaskari katika Mahali Patakatifu Lourdes nchini Ufaransa, inayoongozwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Kama Bernadette ambaye alihimizwa na Bikira kuwaombea mapadre wamjengee Kanisa la ibada ili kuwaruhusu watu kuja katika maandamano, vivyo hivyo Papa Francisko amewaalika Askari hao: “waanze safari pia kiroho, kwanza kabisa kwa Mungu, lakini pia kwa kaka na dada zetu, ili kujenga ulimwengu unaounga mkono na wa kidugu.”
Ahadi ina nguvu kwa ajili ya huduma ya amani duniani
Katika ujumbe huo Baba Mtakatifu anaonesha juu ya “ahadi ambayo ina nguvu zaidi kwa sababu inawalenga wale ambao wanaitwa kuchukua nafasi isiyoweza kubadilishwa kwa manufaa ya wote na huduma ya amani duniani.” Hata kwa wale wanaovaa sare, Papa Francisko amebainisha kuwa “hija ni uzoefu wa imani unaotuwezesha kugundua uzuri wa kutembea pamoja, kusaidiana na kufikia wengine. “
Baba Mtakatifu Francisko aidha amebainisha kuwa: “hija inakuruhusu kuwa karibu na wenzenu wagonjwa na waliojeruhiwa mikononi na kuwatunza na kuleta huruma ya Mungu kwa ulimwengu wa kijeshi.” Ulimwengu, unawahitaji, hasa katika wakati huu wa giza katika historia yetu. Tunahitaji wanaume na wanawake wa imani wenye uwezo wa kuweka silaha zao chini ili kuwa katika huduma ya amani na udugu.” Alihitimisha ujumbe wake.