Tafuta

2024.05.19 Papa katika sala ya Malikia wa Mbingu 2024.05.19 Papa katika sala ya Malikia wa Mbingu  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko:Tuombe roho Mtakatifu alete maelewano katika mioyo,familia na jamii!

Mara baada ya Takafakari ya Neno la Mungu na sala ya Malkia wa Mbingu katika Siku Kuu ya Pentekoste kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican,Papa ameomba Roho Mtakatifu alete maelewano katika migogoro,familia,jamii na ulimwengu mzima,kuwapa watawala ujasiri wa kutekeleza ishara za mazungumzo, ambayo yalete mwisho wa vita.Na ameshukuru makaribisho ya hija yake huko Verona.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya tafakari na sala ya Malkia wa Mbingu akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican amewageukia waamini na mahujaji waliofika katika siku kuu ya Pentekoste tarehe 19 Mei 2024 wakiwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na kusema kuwa “Roho Mtakatifu ndiye anayeumba maelewano! Na huunda kuanzia hali halisi tofauti, wakati mwingine hata kukinzana. Leo, katika sikukuu ya Pentekoste, tumwombe Roho Mtakatifu, Upendo wa Baba na Mwana, ili kuunda maelewano katika mioyo, maelewano katika familia, maelewano katika jamii, maelewano katika ulimwengu wote; Roho azidishe umoja na udugu kati ya Wakristo wa madhehebu mbalimbali; kuwapatia watawala ujasiri wa kutekeleza ishara za mazungumzo, ambazo zinaweza hatimaye kufikia mwisho wa vita.” Baba Mtakatifu  akiendelea amesema: “Vita vingi leo: hebu tufikirie Ukraine - mawazo yangu yanakwenda hasa kwa jiji la Kharkiv, ambalo lilipata mashambulizi siku mbili zilizopita -; hebu tufikirie Nchi Takatifu, Palestina, Israeli; tufikirie sehemu nyingi zenye vita. Roho awaongoze viongozi wa mataifa na sisi sote kufungua milango ya amani.”

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu  Petro 19 Mei 2024
Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro 19 Mei 2024

Hija ya Verona

Baba Mtakatifu afikiria hija yake ya kichungaji aliyotelekea Jumamosi tarehe 18 Mei 2024 amesema “Ninatoa shukrani zangu kwa ukaribisho na upendo wa Verona jana: Watu wa Verona walikuwa wazuri! Asante asante. Hasa, ninafikiria gereza la Verona, ninawafikiria wafungwa, wafungwa ambao wamenishuhudia kwa mara nyingine tena kwamba maisha, ubinadamu na matumaini yanazunguka nyuma ya kuta za gereza. Asante" yangu ya dhati inawaendea wafanyakazi wote wa gereza, na hasa kwa mkurugenzi, Dk. Francesca Gioieni.”

Papa amewasalimu waamini waliokuwa Uwanja wa Mtakatifu Petro
Papa amewasalimu waamini waliokuwa Uwanja wa Mtakatifu Petro

Salamu kwa wanahija

Aidha Papa Francisko amewageukia mahujaji na kusema: “Nawasalimu ninyi nyote, mahujaji kutoka Roma na kutoka sehemu mbalimbali za Italia na duniani kote. Hasa ninawasalimu wale kutoka Timor-Leste - nitawatembelea hivi karibuni!  wale wa Latvia na Uruguay; pamoja na jumuiya ya Paraguay ya Roma, ambayo inaadhimisha Siku Kuu ya Bikira Maria wa Caacupé, na Utume wa Lucerna wa Kikatoliki, Ureno. Vile vile amewasalimia vijan kutoka Parokia ya Mtakatifu Maria Mkingiwa na watawa waliokuwapo. Amewasalimu na kuwakaribisha watu wa Porto Azzurro na Terracina, na Taasisi ya Catenia ya Mtakatifu Rosa wa Roma. Hatimaye amewatakia Dominika Njie, lakini tafadhali wasisahau kusali kwa ajili yake. Mlo mwema na kwaheri ya kuonana.

Papa baada ya tafakari na sala ya Malkia wa Mbingu
19 May 2024, 13:06