Papa:Kanisa liko wazi kwa wote,bali miungano ya watu wa jinsia moja haiwezi kubarikiwa!
Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
“Wote, wote,wote.” Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena amesisitiza ndoto ya Kanisa lenye milango wazi na kanuni ya makaribisho, msingi mkuu wa upapa wake katika mahojiano aliyotoa kwa Norah O'Donnell, mkurugenzi wa Shirika la habari za jioni ( CBS) la Marekani, yaliyorekodiwa Mtakatifu Marta mjini Vatican mnamo tarehe 24 Aprili 2024 na sehemu ambayo ilitangazwa tarehe 19 Mei usiku kwenye kipindi cha Dakika 60.
Injili ni kwa wote”, alisisitiza Papa, kwa sisi sote tulio wadhambi: “Mimi pia ni mwenye dhambi”. Na “ikiwa Kanisa likiweka mpaka kwenye mlango wake, linakoma kuwa Kanisa la Kristo, alisema Papa Francisko ambaye alitoa ufafanuzi juu ya suala la baraka kwa miungano ya watu wa jinsia moja, ambalo katika hati ya Fiducia Supplicans ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa inazungumzia. “Baraka ni kwa kila mtu:” kila mtu anaweza kubarikiwa, lakini sio muungano wa watu wa jinsia moja, alielezea Papa, huku akifafanua kuwa: “Nilichoruhusu sio kubariki muungano.” Hii inakwenda kinyume na “sheria ya Kanisa.”
Uzazi wa kupandikiza umekuwa wa biashara
Akiwa bado anazungumzia juu ya mashoga, mwandishi huyo wa habari alikumbuka Papa aliposema kuwa “ushoga sio uhalifu.” “Hapana.” Ni ukweli wa kibinadamu, alijibu Papa Francisko. Wakati ananyanyapaa, kama katika hafla zingine, juu ya za uzazi wa kupandikiza ambao alisema “umekuwa biashara, na hii ni mbaya sana. Ni hasi sana.” Kwa baadhi ya wanawake, kwa mfano wale ambao ni wagonjwa, hata hivyo, inaweza kuwa tumaini la pekee, aliona mwandishi wa habari. “Inaweza kuwa. Tumaini lingine ni kuasili” yaani, alijibu Papa, akialika kutokwepa kanuni ya maadili.
Ukosoaji kutoka kwa wahifadhi
Alipoulizwa kuhusu ukosoaji ulioelekezwa kwake na baadhi ya maaskofu wahifadhi nchini Marekani, Papa alijibu: “Mhifadhi ni mtu ambaye anang'ang'ania kitu na hataki kuona zaidi yake. Ni mtazamo wa kujiua, kwa sababu jambo moja ni kuzingatia mila, kuzingatia hali za zamani, lakini ni jambo lingine kwa kujifunga mwenyewe katika sanduku la kidogma.”
Wito kwa nchi zilizo kwenye vita: “Simamisheni”
Katika mahojiano, yaliyofanywa kwa ajili ya maandalizi ya Siku ya Watoto Duniani mnamo tarehe 25 na 26 Mei jijini Roma, mtazamo haukuweza lakini kutokuelekeza kwa watoto wadogo, kuanzia na wale wanaoteseka vitani kama vile: Gaza, Ukraine, na watoto ambao “wamesahau jinsi ya kutabasamu”, alirudia Papa Francisko. Na ni pamoja nao akilini kwamba Askofu wa Roma alizindua wito kwa nchi zilizo katika vita kwa : “Kila mtu, aache vita.” “Acha vita.” Lazima mtafute njia ya kujadili amani. Mjitahidi kufikia amani. Amani ya mazungumzo daima ni bora kuliko vita visivyo na mwisho… Tafadhali acha. Mzungumze.”
Itikadi ni mbaya daima
Kwa kuzingatia vita vya Israel na Gaza, kisha juu ya maandamano katika vyuo vikuu na juu ya kuongezeka chuki dhidi ya Wayahudi, Papa Francisko alisisitiza kwamba: “Kila itikadi ni mbaya, na chuki dhidi ya Wayahudi ni itikadi, na ni mbaya. Kila chuki daima ni mbaya. Unaweza kuikosoa serikali moja au nyingine, serikali ya Israel, serikali ya Palestina. Unaweza kukosoa kama unavyotaka, lakini sio 'kupinga' watu. Si chuki dhidi ya Palestina au chuki dhidi ya Wayahudi.”
Wahamiaji, watu wengi “wananawa mikono”
Katika hali hiyo hiyo, Papa Jorge Mario Bergoglio, akizungumzia mateso ya wahamiaji wengi, alishutumu ukweli kwamba watu wengi “hunawa mikono": "Kuna Pontius Pilates wengi huko nje ... ambao wanaona kinachotokea, vita, dhuluma, uhalifu... Huko ni kutojali…Tafadhali, lazima tufanye mioyo yetu ihisi tena. Hatuwezi kubaki na sintofahamu, kuhusu majanga haya ya kibinadamu. Utandawazi wa kutojali ni ugonjwa mbaya sana.”Papa aidha alisistiza: "wazimu mtupu" habari, zilizotajwa na O'Donnell, kwamba Jimbo la Texas linajaribu kufunga chama cha Kikatoliki kwenye mpaka na Mexico ambacho kinatoa usaidizi wa kibinadamu kwa wahamiaji wasio na vibali. “Kufunga mpaka na kuwaacha kuna wazimu,” alisisitiza tena Papa Francisko. “Mhamiaji lazima akaribishwe. Kisha tutaona jinsi ya kusimamia. Labda tunahitaji kumrudisha, sijui, lakini kila kesi lazima izingatiwe kwa njia ya kibinadamu.”
Unyanyasaji wowote hauwezi kuvumiliwa
Katika mahojiano hayo hayakukosa kutajwa suala la unyanyasaji katika Kanisa, uhalifu ambao Papa alirudia kusema kuwa “hauwezi kuvumiliwa.”Wakati huo huo alitambua kwamba lazima tuendelee “kufanya zaid, kwa sababu "kwa bahati mbaya janga la unyanyasaji ni kubwa na lazima tuhakikishe kwamba hii sio tu kuadhibiwa lakini kwamba haitatokea tena.”