2024.05.20 Papa amekutana na Uwakilishi wa Viongozi wa Chuo Kikuu cha Loyola cha  Chicago. 2024.05.20 Papa amekutana na Uwakilishi wa Viongozi wa Chuo Kikuu cha Loyola cha Chicago.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa kwa viongozi wa Chuo Kikuu Loyola:kuwa mashahuda wa tumaini na ndoto

Papa akikutana na viongozi wa Chuo Kikuu cha Loyola,Chicago,amesisitiza kuwa kuna haja ya wanaume na wanawake walio tayari kufanya kazi ili ulimwengu uwe na amani katika mabadiliko ya haraka na changamoto zinazoongezeka.Jukumu la Vyuo vikuu ni muhimu,elimu,pamoja na usambazaji wa maarifa pia ni dhamira na njia ya kutoa mafunzo kwa watu wenye uwezo wa kujumuisha maadili.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na wakuu wa Bodi ya  Chuo Kikuu cha Loyola kutoka Chcango Nchini Marekani, Jumatatu tarehe 20 Mei 2024, wakiwa katika hija na kuona mahali ambapo alizaliwa na kukua Mtakatifu Ignatius wa Loyola. Baba Mtakatifu amesema kuwa “Kuondoka ni mfano wa wale wanaotafuta maana ya maisha” (Spes non confundit, 5): daima kuweka ndani hamu hii ya kutembea, kuhiji. Uzoefu wao wa kutembelea maeneo ambayo yalichagiza maisha na hali ya kiroho ya Ignatius hakika umekuza na kuwatia moyo katika safari yao ya kielimu na ya kibinafsi. Na imekuwa ni ziara katika mizizi. Kwa hivyo warudi kwenye mizizi yao ili kusonga mbele.

Viongozi wa Chuo Kikuu cha Loyola, wa Chicago wamekutana na Papa
Viongozi wa Chuo Kikuu cha Loyola, wa Chicago wamekutana na Papa

Papa Francisko amesema kuwa: “Huwezi kusonga mbele bila mizizi, ambayo wanachukua nguvu: wanachukua nguvu kutoka katika mizizi. Kwa hivyo ni kurudi kwenye mizizi yao ili kusonga mbele. Mizizi ya Taasisi yao iko katika uzoefu wa Mwanzilishi, ambaye daima alimtanguliza Mungu na alikuwa akitafuta daima mapenzi ya Mungu. "Kusonga mbele kutumikia." Njia yake ya kiroho, iliyo na utambuzi na kujitolea kwa haki, iendelee kuhamasisha na kuongoza maisha na matendo yao., Baba Mtakatifu amewashauri. Chuo Kikuu cha Loyola, amesema kwa hakika, kimetiwa moyo na mapokeo ya Jumuiya ya Yesu, iliyosimikwa katika utambuzi na matendo. Tamaduni hii inawaalika leo kutafuta ukweli kupitia mafunzo ya dhati, kusikiliza kwa uangalifu na kuchukua hatua kwa ujasiri. Amewahimiza kudumu kwenye njia hii, kuwa mashahidi wa matumaini katika ulimwengu ambao mara nyingi una migawanyiko na migogoro. Kwa kuongezea Papa alisema: “Namshukuru Mungu kwamba kuna migogoro, lakini migogoro inatatuliwa kwa ngazi nyingine, ya juu zaidi.

Papa na Viongozi wa Cho Kikuu cha Loyola, cha Chicago
Papa na Viongozi wa Cho Kikuu cha Loyola, cha Chicago

Migogoro hutuongoza kutembea kwenye  barabara isiyo rahisi kutokealabyrinths) na tunatokea kwenye barabara hiyo (labyrinth)kwa juu lakini hatuko peke yetu. Migogoro inatusukuma kufanya kazi. Kwa hiyo, wadumu kwenye njia hiyo, ambayo inakufundisha kukuza hisia muhimu, uwezo wa kutambua na unyeti kuelekea changamoto za kimataifa; kujiuliza kila mara swali: Chuo Kikuu chetu kinawezaje kuchangia kufanya ulimwengu kuwa mahali pazuri zaidi? “Daima jitahidi kwa bora zaidi!” Papa alisisitiza Katika wakati wa kihistoria ulio na mabadiliko ya haraka na changamoto zinazozidi kuwa ngumu, jukumu la taasisi za kitaaluma ni muhimu. Mna kazi sio tu ya kuunda akili nzuri, lakini pia kukuza mioyo ya ukarimu na dhamiri zinazozingatia utu wa kila mtu.

Elimu inafanywa kwa ngazi tatu:kichwa,moyo na mikono

Elimu “inafanywa kwa viwango vitatu: kwa kichwa, kwa moyo na kwa mikono.” Papa amewasihi wafikirie kile wanachohisi na kufanya, kusikia wanachofikiria na kutenda  kile wanachofikiria na kuhisi. Lakini daima katika maelewano, mambo matatu. Elimu, pamoja na upitishaji wa maarifa, ni dhamira na mbinu ya kuwafunza watu wenye uwezo wa kujumuisha maadili ya upatanisho na haki katika kila nyanja ya maisha. Akili, moyo na mikono haviwezi kukua vyema tofauti, na kwa pamoja wanaweza kujihusisha na ukweli na mahitaji ya wakati huo. Papa amewatakia kuwafundisha waotaji ndoto, na kuwa wao mwenyewe kwanza kabisa! Ili kusonga mbele maishani, lazima wawe na ndoto. Papa amesema: “Mtu ambaye amepoteza uwezo wa kuota anakosa ubunifu, anakosa mashairi, na maisha bila ushairi hayafanyi kazi.”

Kukuza udadisi wa kiakili na sio gumzo linaloharibu

Papa amewahimiza tena  kukuza udadisi wa kiakili,  ambao sio gumzo, na ambayo inadhuru, bali udadisi wa kiakili,  wa roho ya ushirikiano na usikivu kuelekea changamoto za enzi tunayoishi, kuendeleza urithi wa Mtakatifu Ignatius. Kuna haja kwa wanaume na wanawake ambao wako tayari kuweka ujuzi wao katika huduma ya wengine, kufanya kazi kwa ajili ya siku zijazo ambapo kila mtu anaweza kukuza uwezo wao na kuishi kwa heshima na hadhi na ulimwengu unaweza kupata amani. Hii inanigusa sana leo hii: katika hali ya shida ya utaratibu wa ulimwengu inaonekana kwamba upeo wa matumaini haupo. Na huwezi kuishi bila matumaini. Tusisahau matumaini, ambayo ni nanga, kwenye fukwe wakati tunashikamana na kamba. Matumaini kamwe hayakatishi tamaa!” Papa amewakabidhi, hasa, mazungumzo ya kiutamaduni na ya kidini kama zana ya kukuza maelewano, ushirikiano na kujenga madaraja kati ya mila, tamaduni na mitazamo tofauti ya ulimwengu. Mungu awabariki na kuwasindikiza katika safari yao, safari ya maarifa na huduma. Kwa kuhitimisha Papa alisema: “Nanawaombea, lakini tafadhali, mniombee. Kwa sababu kazi hii si rahisi! Asante.”

Hotuba ya Papa kwa viongozi wa Chuo Kikuu cha Chicago- Marekani
20 May 2024, 17:24