Papa kwa Wajesuit:hata Yesu hakupata matokeo mazuri akiwa na wanafunzi wake!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Papa Francisko amekutana na Tume ya Kimataifa ya Utume wa Elimu ya Wajesuit katika hotuba hiyo (ICAJE), aliyowakabidhi wajisomee Ijumaa tarehe 24 Mei 2024, Papa anaanza kwa kuwashukuru kwa niaba ya kanisa kwa kazi ambayo wanaitwa katika maisha ya kijesuiti na katika shule ambazo wameunganishwa katika utume ambao waliamua kuungana katika shughuli za utume wa Shirika la Yesu. Ni kweli kwamba Mtakatifu Ignatius na wenzake wa kwanza hawakuzingatia umuhimu wa shule mwanzoni mwa kuanzaJumuiya. Lakini ni kweli vile vile kwamba upesi walitambua uwezo mkubwa wa kueneza Injili na kuukaribisha kwa shauku na kujitolea.
Bila shaka, shule za Kijesuit zimehakikisha kwamba, ujumbe wa Injili unaendelea kusikika miongoni mwa vizazi vipya, zikiambatana na ushupavu wa kitaaluma na kiakili unaowatambulisha. Lakini kitovu kimekuwa na lazima kiendelee kuwa Yesu. Kwa sababu hiyo, Wajesuit, kupitia programu na shughuli za masomo shuleni, wamejitolea kuhakikisha kwamba vijana wanaweza kuwasiliana na Injili, na huduma kwa wengine, na hivyo kuchangia katika manufaa ya wote. Mashirika ya Maria yalikuwa kielelezo cha thamani cha jinsi elimu ya Kijesuit ilitaka kuwaalika wanafunzi wake kuwa mawakala wa mabadiliko na uinjilishaji katika muktadha wao. Mkataba mpya wa Elimu Kimataifa, ambapo Baba Mtakatifu aliuanzisha, amesisitiza kwamba unataka kusasisha jitihada za elimu ili vijana waweze kujiandaa na kuanza kubadilisha mawazo ya elimu ya kuwa na mafanikio ya yangu binafsi tu na kuwa katika mawazo ya elimu ambayo inawaongoza kugundua utimilifu wa kweli wa maisha, wakati wa kutumia vipawa vya kibinafsi na uwezo kwa kushirikiana na wengine, kwa ajili ya ujenzi wa kijamii, kibinadamu zaidi na kidugu na katika ulimwengu.
Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe huo aliowakabidha anazidi kukazia kuwa “Tunahitaji kuhama kutoka katika utamaduni wa "umimi" hadi utamaduni wa "sisi", ambapo elimu bora inafafanuliwa hivyo kwa matokeo yake ya kibinadamu na sio matokeo yake ya kiuchumi.” Hii inamaanisha - kama nilivyorudia mara nyingi - kumweka mtu katikati ya mchakato.” Na hivyo ndivyo Padre Arrupe alivyorudia mara nyingi kwetu, akisisitiza kuwa: “kuelimisha watu kwa ajili ya wengine.” Padre Arrupe alifahamu vyema kwamba mtu aliye ubora zaidi ni Yesu, mtu wa kweli pamoja na wengine.” Baba Mtakatifu aidha anabainisha kama ambavyo wao wanajua namna iliyo bora ya kuelimisha ni kwa njia ya mfano, kuiga ndani yetu kile tunachotamani kwa wanafunzi wetu. Hivi ndivyo Yesu alivyowaelimisha wanafunzi wake. Hivi ndivyo tunavyoitwa kuelimisha katika shule zetu. Hii ndiyo sababu kila kitu unachoweza kufanya ili kuhakikisha kwamba waelimishaji katika shule zetu wanaelewa wito huu kiuhalisia ni muhimu.
Kumweka mtu katikati kunamaanisha kuwaweka waelimishaji katikati ya mafunzo, kuwapa maandalizi na uusindikizwaji ambao pia huwasaidia kugundua uwezo wao na wito wao wa kina wa kusindikizana na wengine. Kumweka mtu katikati kunamaanisha kujitenga na ile ya sisi wenyewe ili kuwatambua wengine, hasa wale ambao wako pembezoni mwa jamii zetu, na ambao sio tu wanahitaji msaada wetu, lakini pia ambao wana mengi ya kutufundisha na kutupatia. Sote tunafaidika tunapokaribisha maskini zaidi na wasio na ulinzi miongoni mwetu! Kwa kawaida, kama alivyoonyesha Papa Francisko katika barua yake alipothibitisha “Mapendeleo ya Kitume ya Kiulimwengu ya Jumuiya ya Yesu, mapendeleo ya kwanza ni ya lazima ili kuelewa maana ya elimu ya Ujumuishwaji, kwa kuwa bila uhusiano wa kweli wa waelimishaji na Bwana hakuna chochote kati ya wengine inawezekana. Kwa njia hiyo Papa anakazia kusema kuwa “Ni lazima kusisitiza juu ya hili. Kwa hiyo nina furaha kwamba mnafanya Semina ya Kimataifa ya Yogyakarta - kuweza kuzama ndani zaidi jinsi tunavyoshiriki hazina iliyofunuliwa katika Yesu na vijana - na kwamba vijana wanaweza kupata fumbo lake la ukombozi na wokovu. Lakini watafaulu tu ikiwa wataona kuwa waelimishaji wao wanakuwa ndani kama baba wa familia, wa waelimishaji wa kwanza katika familia - uhusiano huu na Mungu na heshima kubwa kwa wengine na kwa kazi ya uumbaji. Kwao vyuo vyetvyao lazima pia viwe waelimishaji wa waelimishaji, walimu wa walimu.
Papa Francisko ameonesha furaha kuweza kukutegemea ili kukuza mkataba mpya wa elimu wa kimataifa. Bila hivyo, ulimwengu wetu, ambao tayari unakabiliwa na vurugu nyingi na ubaguzi, hautaweza kuunda mustakabali uliojaa matumaini au kushinda changamoto kubwa zinazoihusu na ambazo zinatulazimisha kufahamu zaidi ukweli kwamba tunashiriki pamoja. nyumba ya dunia yetu. Kuelimisha ni kazi ya kupanda na, kama Maandiko Matakatifu yasemavyo, mara nyingi “tunapanda kwa machozi ili kuvuna kwa nyimbo” (rejZab 126:5). Elimu ni kazi ya muda mrefu, kwa uvumilivu, ambapo matokeo yake wakati mwingine haijulikani; hata Yesu hakupata matokeo mazuri akiwa na wanafunzi wake hapo mwanzo, bali alivumilia, na anaendelea kutuvumilia ili kutufundisha kuwa kuelimisha kunamaanisha kungoja, kuvumilia na kusisitiza kwa upendo.