Papa:maumivu yakiingia moyoni ni sumu,msipoteze uwezo wa kucheza
Na Sebastián Sansón Ferrari&Angella Rwezaula – Vatican.
Siku ya mwisho ya Mkutano wa Kimataifa wa Maana ulioandaliwa na Scholas Occurrentes na Benki ya Maendeleo ya Amerika ya Kusini (CAF) na Carribien ulifanyika katika Ukumbi Mpya wa Sinodi, mbele ya Papa Francisko, tarehe 23 Mei 2024 ambapo wakurugenzi kadhaa kutoka vyuo vikuu muhimu ulimwenguni na watu mashuhuru kutoka katika utamaduni, siasa na teknolojia, vijana wenye ushawishi katika jamii zao na wasanii. Madhumuni ya mkutano huo yalikuwa kutafuta suluhisho madhubuti kwa changamoto za Chuo Kikuu cha Maana, ambacho usimamizi wake ulikabidhiwa na Papa kwa Jumuiya ya Kimataifa ya Kielimu ya Scholas Occurrentes.
Teknolojia, mazingira na afya ya akili zilikuwa mada ambazo washiriki walifanyia kazi kwa siku tatu, ambao waliwasilisha hitimisho lao kwa Papa, katika mazingira ya uzoefu mkubwa na ucheshi. “Maumivu yanapofunguka kwa msaada wa wengine huzaa matunda,” alisema Papa huku akijibu swali la mwanamke kijana kuhusu jinsi ya kuendelea kupata upendo licha ya mateso yanayotesa. “Hatari ni kwamba maumivu yanakufunga - alielezea Papa Francisko na kwamba - lazima uweke moyo wako wazi kila wakati.” Na ametoa mwaliko wa kuelimisha kwa matumaini kwa sababu maumivu yanapotulia moyoni “ni sumu, daima.” Kijana mmoja alimwuliza jinsi gani sanaa ni muhimu na Papa alisisitiza kwamba “sanaa inafungua upeo. Sanaa inakuweka huru, inakuweka chini, inakufanya utembee.” Na alijiruhusu kutaja kipande cha shairi la Borges, pia akikumbuka alipokuwa mdogo na pamoja na kaka zake alitumia muda mwingi kwa bibi yao, au babu yao alipowasomea kitabu Cuore cha De Amicis yaani Moyo cha Mwandishi De Amicis.
Rapa aliingilia kati na alipofurahia mvulana mmoja wa kucheza muziki huku akiwahimiza wampigie makofi kwa mdundo na hata Papa Francisko alijiruhusu kuambukizwa nao. Kwa sababu “ufunguo wa kila kitu ni uwezo wa kucheza.” Alisema Papa na kuongeza kuwa: “Uwezo wa kweli wa kucheza ni ubunifu.”Na alisema hayo baada ya ushuhuda wa mwanadada mmoja ambaye alionesha ugumu wa kutembea na “anayetualika kukuza ushirikishwaji katika kila mazingira. Dada huyo alisimulia kuwa alikuwa mwathirika wa uonevu akiwa na umri wa miaka kumi na miwili na kwamba alikaa nje ya mfumo wa shule kwa miezi sita hadi chama cha Teresiani kilipompatia msukumo mpya na kujiamini, kuunda msingi na kukabidhi kanuni ambazo zinashikilia.
Muktadha huo hasa unamweka mwanadamu katika upekee wake katikati ya elimu. Unakuza utamaduni wa kukutana katika mtazamo unaotarajiwa na Papa wa Argentina, kiukweli, katika wazo la kuanzisha harakati za aina hii lilizaliwa, pamoja na maendeleo ya ujuzi laini, kujaribu kurejesha ustadi katika utamaduni wa kisasa. Chuo Kikuu cha Maana hakipaswi kupoteza uhusiano kati ya lugha tatu: ile ya mikono, ya moyo na ya akili. Hivyo alirudia kusema Papa Francisko, ambaye anajali sana kuhusu mwelekeo huu jumuishi wa mtu, ushirikiano wa imani na maisha, balozi wa Bolivia alizungumza katika utangulizi, huku akichukua gitaa, na akiimba wimbo na kueleza kwamba katika nchi yake, yenye mataifa 36, kuna furaha nyingi kati ya watu, juu ya yote na licha ya serikali yake kuwa umaskini na ya watoto wengi. Mkutano huo ulimalizika na Papa akiwa ameshikilia mpira wa vitambaa vichakavu mkononi mwake, ambao ulikuwa ni ishara ya mchezo. Lakini alikumbusha alivyo cheza akiwa kijana na kuwaalika kugundua fumbo lililo ndani mwake.