Tafuta

2024.05.25 Papa na washiriki wa Kongamano la Kimataifa la uchungaji wa vijana. 2024.05.25 Papa na washiriki wa Kongamano la Kimataifa la uchungaji wa vijana.  (Vatican Media)

Papa:Ndoto yangu matukio 3 yasaidie vijana kusikia ujumbe wa Injili ya matumaini

Na sio kutangaza maandishi yangu,lakini kusoma Gaudete et exsultate ni wimbo wa furaha na Mkristo mwenye huzuni ni Mkristo aliye na huzuni.Furaha lazima iwe chakula cha mkristo,usemi wa mkristo na ikiwa hujui furaha ni nini,nenda mbele ya kioo.Ni hotuba ya Papa Francisko kwa washiriki wa Kongamano la kimataifa la Uchungaji wa Vijana la Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 25 Mei 2024, akikutana na Washiriki wa Kongamano la Kimataifa ya uchujaji wa vijana la Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, katika hotuba yake, awali alotoa shukrani zake kwa wale wote waliochangia mafanikio ya Siku ya Vijana Duniani huko Lisbon. Ilikuwa kazi kubwa sana, lakini ilistahili jitihada hiyo.   Kufuatia janga la uviko, na katikati ya mivutano mingi ya kimataifa, vijana walihitaji sindano ya matumaini. Papa alisema kuwa: “Siku hizo huko Lisbon zilikuwa sherehe ya kweli ya furaha ya kuwa hai na kuwa Mkristo.   Lilikuwa ni adhimisho la tumaini linaloendelea kukaa ndani ya mioyo ya vijana, kwa sababu Mungu mwenyewe analikuza na kulitia nguvu licha ya dhiki zote.

Baba Mtakatrifu amebainisha kwamba wakitiwa moyo na uzoefu huo, sasa wameitwa kufanya kazi katika kujiandaa kwa ajili ya matukio ya kimataifa yajayo, lakini pia, na zaidi ya yote, kuendelea kusindikiza na huduma ya vijana katika "nyakati za kawaida".  Papa amesema “Ninapofikiria juu ya Jubile ya Vijana mwaka ujao na Siku ya Vijana (WYD) huko Seoul miaka mitatu kuanzia sasa, "ndoto" yangu ni kwamba matukio haya yatawasaidia wengi wa vijana, ikiwa ni pamoja na wale ambao hawendi kanisani, kukutana na Yesu, na kusikia Ujumbe wa Injili ya matumaini.

Baba Mtakatifu aidha alibainisha jinsi ambavyo anawafikiria wale vijana ambao wameshuka moyo, ambao hawanyanyui tena macho yao kwenye upeo wa macho, ambao wameweka kando ndoto zao kuu na sasa wamenaswa katika hali ya kukata tamaa na kulemewa na matatizo ya maisha.  Asia ni bara changa, lililojaa maisha, bado vijana wengi, hasa katika miji mikubwa, wanakabiliwa na kupoteza tumaini na kujiondoa ndani yao, na uhusiano mdogo, masilahi kidogo.  Jambo hilo hilo linatokea duniani kote.  Kwa njia hiyo matukio ya Roma na Seoul ni fursa tulizopewa na Mungu kuwaambia vijana ulimwenguni kote: Yesu ni tumaini, kwangu, kwako, kwetu, kwa kila mtu!  Wanapojiandaa kwa matukio haya makubwa, hawapaswi kupuuza njia za kawaida, yaani, safari ya vijana katika maisha yao ya kila siku.

Papa amemaanisha aina ya huduma ya kichungaji inayojumuisha hatua ndogo, idadi ndogo, maneno rahisi na vitendo, maamuzi ya kila siku na wakati wa sherehe na maombi katika jumuiya zao. Katika suala hilo Papa amependa , kutaja mambo kadhaa ambayo hayapaswi kamwe kukosa katika kazi ya kila siku ya huduma ya vijana. Kwanza, vijana wanahitaji kusaidiwa kufikia uhakika fulani wa msingi katika maisha, kweli za moyo: “Mungu ni upendo,” “Kristo anawaokoa ninyi”, “Anaishi”, na “Roho huhuisha.” Hatupaswi kamwe kuchoka kutangaza kweli hizi nne rahisi (taz. Christus Vivit, 112-133). Vijana wanaweza kuwa na wasiwasi kuhusu habari mbaya zinazotushambulia kila siku, lakini hilo lisifiche uhakika wao kwamba Kristo mfufuka yuko pamoja nao na ana nguvu zaidi kuliko uovu wowote. Kristo yu hai!   Vitu vyote viko mikononi mwake.  Yeye pekee ndiye anayejua mustakabali wa ulimwengu wetu na wa maisha yetu binafsi. Ni muhimu kuwapa vijana fursa ya kumwona Kristo aliye hai kwa njia ya sala, adhimisho la Ekaristi na Kitubio; makusanyiko ya jumuiya, huduma kwa maskini na ushuhuda wa maisha ya watakatifu. Vijana ambao wamepata uzoefu huu wanakuwa mashahidi wa kusadikisha wa ujumbe wa Injili.

Kipengele kingine muhimu ni utambuzi wa kiroho (taz. Christus Vivit, 278-298).   Utambuzi ni sanaa ambayo wahudumu wa kichungaji wanapaswa kuwa wa kwanza kujifunza: mapadre na watawa, makatekista na viongozi wa watu wazima, na vijana wanaofuatana na vijana wengine.  Ni ujuzi ambao hauwezi kuboreshwa, lakini unapaswa kukuzwa, uzoefu na kuishi. Kwa kijana, kupata mtu mwenye uwezo wa utambuzi ni kupata hazina. Katika safari ya imani na ugunduzi wa wito wa mtu, mwongozo wa busara husaidia kuepuka makosa mengi, na uongo mwingi, wakati mwingi wa kuchanganyikiwa na "kupooza". Papa Francisko alikumbusha juu ya Katekesi yake ya Jumatano juu ya utambuzi na kuwaomba watafute katekesi hiyo. Hapo alipenda kumulika vipengele vitatu tu vya utambuzi ni sinodi, kibinafsi na kuelekezwa kwenye ukweli. 

Sinodi. Katika siku hizi za ubinafsi ulioenea, kila mtu anakwenda  kwa njia yake mwenyewe, kila mtu anaamua ni nini cha maana katika maisha, kila mtu anaweka maadili yake mwenyewe, ukweli wao wenyewe.  Katika utendaji wa utambuzi, kwa upande mwingine, Kanisa huwaweka kaka na dada zetu katika imani pamoja nasi, ili kusafiri pamoja, na sio peke yetu, na hivyo ukuaji wetu wa ndani unaboreshwa sana.   Kwa maana hiyo, utambuzi ni sinodi. Wakati huo huo, ni ya kibinafsi.   Katika ulimwengu wetu, kila kitu kimezalishwa kwa wingi na kusawazishwa.   Vijana, badala yake, wanahitaji kusindikizwa kibinafsi, kama watu binafsi. Kila mmoja wao ni wa kipekee, na kila mmoja anastahili kusikilizwa, kueleweka na kupewa ushauri unaofaa kwa umri wake pamoja na ukomavu wa kibinadamu na kiroho.   Utambuzi ni wa lazima na lazima uwe wa kibinafsi.

Pia una mwelekeo wa ukweli. Katika jamii iliyoathiriwa na habari za uwongo, ambapo wasifu wa kibinafsi mara nyingi hutungwa au kupotoshwa, ambapo watu huunda utambulisho mbadala, utambuzi huwakilisha kwa vijana njia ya uhalisi: njia ya kuibuka kutoka katika utambulisho bandia na kugundua utambulisho wao wa kweli. Utambuzi ni juu ya kuwa "halisi": mbele yako mwenyewe, mbele ya wengine, na mbele ya Mungu. Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu amependa kusisitiza umuhimu wa kuendelea kuwasikiliza vijana.   Usikilizaji wa kweli, sio ule wa "nusu nusu" au "mavazi ya dirishani".   Vijana hawapaswi kusukumwa katika kukuza mawazo na shughuli ambazo tayari zimeamuliwa na wengine, au ambazo hazikidhi mahitaji yao.  Hapana.

Vijana wanapaswa kuwezeshwa, kushirikishwa katika mazungumzo, katika kupanga shughuli, katika maamuzi.   Wafanywe kujisikia kwamba wao ni sehemu hai na kamili ya maisha ya Kanisa; na zaidi ya yote wameitwa kuwa wa kwanza kuleta ujumbe wa Injili kwa wenzao. Papa amewashukuru , kwa mara nyingine kwa kujitolea kwao na vijana kwa vijana!  Waendelee kwa ujasiri, wakiwapelekea kila mtu habari njema kwamba Yesu yu hai na ni Bwana. Huu ni ujumbe wa furaha, faraja na matumaini ambayo watu wengi katika ulimwengu wetu wanasubiri.   Amewabariki wote  kutoka moyoni, na amewamba tafadhali, wamwombee.

HOTUBA YA PAPA KWA KONGAMANAO LA VIJANA
25 May 2024, 16:31