Tafuta

2024.05.25 Papa na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa  "Somos Community Care" 2024.05.25 Papa na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa "Somos Community Care"  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa:Utunzaji na utaalamu ni zawadi mbili za thamani kubwa kwa wale wanaoteseka

Katika Mkutano na washiriki wa mkutano wa kimataifa uliohamasishwa na ‘Somos Community Care,’chama kisicho cha kibiashara cha madaktari,Papa alishirikisha wakati wa huruma katika maisha yake ya zamani yaliyohusishwa na daktari wa familia kwamba:daktari wa familia huimarisha uhusiano wa kibinadamu na ana uwezo wa kutoa joto na usaidizi wa kitaalamu kwa sababu yeye anajua wagonjwa wake na wapendwa wao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumamosi tarehe 25 Mei 2024, Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican na washiriki wa mkutano wa kimataifa uliohamasishwa na ‘Somos Community Care,’ chama kisicho cha kiserikali cha madaktari ambapo awali ameonesha furaha ya kukutana nao na kumsalimia Daktari Ramon Tallaj, mwanzilishi wa SOMOS Community Care, na Askofu Mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Chuo cha Kipapa cha Maisha.   Kwa pamoja, katika siku hizi, wamezingatia umuhimu wa kutathmini upya jukumu na uwepo wa daktari wa familia katika huduma ya afya na nyanja ya kijamii.   Hii ni nzuri sana, kwa sababu daktari wa familia ni takwimu ya msingi, ambayo inachanganya uwezo na ukaribu.   Baba Mtakatifu amesisitiza na kuongeza jinsi ambavyo alipenda kujikita kwa ufupi vipengele viwili vya utume huu vilivyochukuliwa kwa usahihi kutoka katika ufahamu wa daktari wa familia: awali ule wa kuwa daktari na ule wa  kuwa "wa familia".

Kwanza, daktari, yaani, yule anayetoa huduma. Sayansi leo hii imepiga hatua kubwa, ikituruhusu kupata matibabu ambayo hayakuwa ya kufikiria miongo michache iliyopita, Papa Francisko amebainisha. Hata hivyo dawa, hata ya juu zaidi ya teknolojia, lakini daima  kwanza kabisa kukutana ni ile ya mwanadamu, inayojulikana na matibabu ya kujali, ukaribu na kusikiliza. Tunapokuwa wagonjwa, tunamtazama daktari, kuwa sio tu mtaalamu mwenye uwezo, lakini pia kuwa uwepo wa kirafiki tunaweza kutegemea, ambaye hutia ujasiri katika uponyaji na ambaye, hata wakati haiwezekani, hatuachi peke yetu, lakini anaendelea kututazama  kwa macho na kusaidia, mpaka mwisho. Mtakatifu Luka, ambaye Mtakatifu Paulo anamwita “daktari mpendwa” (Kol 4:14), mwenzake, lieleza matendo ya Yesu kwa wagonjwa kwa njia hii (taz.Lk5:12-26; 8:40-56) kwamba akawakaribia, akaingia nyumbani mwao, akazungumza nao, akawasikiliza, akawakaribisha katika mateso yao na kuwaponya.

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Francisko ameeleza kuwa “Daktari wa familia vile vile yuko na yuko karibu, akitoa huduma ya joto na ya kitaalamu, kwa sababu anajua wagonjwa wake na wapendwa wao kibinafsi na hutembea nao, siku baada ya siku, hata kwa gharama ya sadaka ya kibinafsi. Hii inatupeleka kwa sababu ya pili ya kwa nini jukumu la daktari wa familia ni la thamani: kuwa mshiriki wa familia. Mwelekeo huu wa jamii wa huduma, ambao unahitaji "kuweka mazingira ya kila mgonjwa katika mahusiano yake" na katika "mahusiano yake ya kijamii na ya kijumuiya.” Uwepo wa daktari wa familia, kiukweli, husaidia kuunda mtandao wa upendo, kushirikiana na mshikamano karibu na mtu mgonjwa, kwenda zaidi ya awamu za uchunguzi na matibabu.

Hii huimarisha uhusiano wa kibinadamu na kubadilisha mateso kuwa wakati wa ushirika wa kuwa na uzoefu pamoja, kunufaisha sio mgonjwa tu, bali pia mlezi, wanafamilia na jumuiya iliyopanuliwa.  Mbinu hii husaidia kuzuia hatari kwamba mtu anayeteseka na wale walio karibu naye watakamatwa ndani ya mfumo ukiritimba na wa kiufundi kupita kiasi; au mbaya zaidi, kutokana na kuwa waathrika wa mtazamo wa soko ambao hauhusiani kidogo na afya, hasa linapokuja suala la wazee na waliodhaifu. Utunzaji na ujuzi ni zawadi mbili za thamani kubwa kwa wale wanaoteseka! Kwa hiyo, Papa amesema kuwa, kazi wanayofanya ni muhimu. Amepyaisha baraka zake kwenye mpango wao na kuwaombea.  Amehitimisha akioma na wasisahau kumwombea tafadhali.

Hotuba ya Papa kwa Somos care
25 May 2024, 16:07