Papa akutana na Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Wapasuaji cha wanafunzi wa zamani wa prof Ivo Pintanguy
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 23 Mei 2024 amekutana na Washiriki wa Mkutano wa Chama cha Madkatari Wapasuaji cha Wahitimu wa Zamani wa Profesa Ivo Pitanguy (AEXPI). Katika hotuba yake amewakaribisha na kuwaona na tabasamu midomoni ya kweli na siyo ya kujifanya. “Katika moja ya miradi yenu ya ushirikiano, mnajaribu kuchora kwenye nyuso za watoto wengi wagonjwa na kwa kuwasaidia, pia mnaleta kwa familia zao na kwa namna fulani, kwa jamii nzima. Asante kwa huduma hii ya busara kwa wengine.” Alisema Papa Francisko.
Kama madaktari na wakristo,nyuso ziakisi jambo kuu zaidi
Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema: “Lakini kama watu, kama madaktari, na kama Wakristo, tunajua kwamba nyuso zetu zimekusudiwa kuakisi uzuri unaopita zaidi ya kile kinachoweza kutambuliwa kwa macho ya kimwili. Uzuri ambao hauko chini ya mwelekeo uliopangwa na biashara ya mitindo, biashara ya kiutamaduni, biashara ya mwonekano, lakini ambayo imeunganishwa na ukweli wa mwanadamu, na utu wake wa karibu zaidi, ambao hatuwezi kuuharibu. Mtakatifu Paulo anatuambia: “Sisi sote, kwa nyuso zisizotiwa utaji, tukiakisi kama katika kioo utukufu wa Bwana, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo” (2Kor 3:18).
Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema “Kweli hii ya kina na iongoze mkono wetu daima, kuleta ulimwenguni sura hiyo ya Mungu iliyotiwa alama katika nafsi zetu, katika matendo mema, katika upendo unaotolewa na kuenea. Inafurahisha kwamba Maandiko yanamweleza Yesu kwetu, wakati huo huo, kama "mzuri zaidi ya wana wa wanadamu” (Zab 45:3) na kama yule ambaye, kwa sababu ya mateso, alikuja kuona hivyo “ameharibika kuwa 'mwanadamu. mwonekano wake na umbo lake ni tofauti na la wanadamu” (Isa 52:14).
Katika kitendawili hiki, Papa Francisko ameongeza kusema “Yesu anatuonesha sura yake halisi na yetu, ambayo inapita katika njia ya msalaba, kwa kukubali udogo wetu, ili kuufikia utukufu wa milele, tumaini lisilokatisha tamaa wala kunyauka (rej. 1Kor 9:9). :25.” Na kwa njia hiyo Papa amehitimsha “ Ninatamani kwamba Mungu awabariki, na kwamba Bikira awalinde na msisahau kuniombea. Asante.”