Papa,Pentekoste:Tusijisalimishe katika nguvu za Ulimwengu bali kwa Roho!

Katika mahubiri ya Misa Takatifu ya Pentekoste iliyoadhimishwa katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican Baba Mtakatifu Francisko ametoa mwaliko kutangaza Injili kwa nguvu lakini bila kuwekewa masharti na kwa wema ili kila mtu akaribishwe. “Kwa Roho tunakuza tumaini la amani,udugu na haki.Mkristo sio mbabe kwa sababu nguvu zake ni nguvu za Roho Mtakatifu.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Dominika tarehe 19 Mei 2024 ameongoza misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Mjini Vatican, kwa kuudhuriwa na Makardianili, Maaskofu wakuu, Maaskofu, Mapadre, Watawa Mashemasi na waamini watu wa Mungu ambapo katika kufafanua juu ya Roho Mtakatifu katika mahubiri ya Misa ya Pentekoste alitumia taswira zinazoonekana kupingana na kwamba  badala yake ni kielelezo cha kitendo ambacho Roho anavutia ndani yetu na kurutubisha utume wa Kanisa. Kwa njia hiyo ametumia maneno ya Nguvu na Wema na pia Nguvu na Fadhila. Akianza mahubiri hayo Papa Francisko amesema: “Simulizi ya Pentekoste (Mdo 2:1-11) inatuonesha maeneo mawili ya utendaji wa Roho Mtakatifu katika Kanisa: ndani yetu na katika utume, yenye sifa mbili: nguvu na wema. Utendaji wa Roho ndani yetu ni wenye nguvu, kama inavyooneshwa na ishara za upepo na moto, ambazo mara nyingi katika Biblia zinahusishwa na nguvu za Mungu ( Kut 19:16-19).

Watumikiaji wa Misa ya Pentekoste wa Chuo Kikuu cha Kipapa la Urbaniani
Watumikiaji wa Misa ya Pentekoste wa Chuo Kikuu cha Kipapa la Urbaniani

Bila nguvu hizi, hatungeweza kamwe kuushinda uovu, wala kushinda tamaa za mwili ambazo Mtakatifu Paulo anazungumza juu yake, kushinda misukumo hiyo ya roho: uchafu, ibada ya sanamu, mafarakano, husuda... (rej. Gal 5). 19-21): kwa kuwa na Roho inawezekana kushinda, Yeye hutupatia nguvu za kufanya hivyo, kwa sababu Yeye huingia katika moyo wetu “mkavu, mgumu na baridi” (taz Sequence Veni Sancte Spiritus). Misukumo hiyo inayoharibu uhusiano wetu na wengine na kugawanya jumuiya zetu, na Yeye huingia moyoni na kuponya kila kitu. Na Yesu pia anatuonesha hili wakati, akiongozwa na Roho, anarudi jangwani kwa muda wa siku arobaini (taz Mt 4:1-11) ili kujaribiwa. Na katika wakati huo ubinadamu wake pia unakua, unaimarika na kujiandaa kwa ajili ya utume.

Baba Mtakatifu Francisko amesisitiza kuwa “Wakati huo huo, hatua ya Mfariji (Paraclete) ndani yetu pia ni ya karimu: ni yenye nguvu na yenye fadhili. Upepo na moto haviharibu au kuteketeza kile unachogusa: hujaza nyumba ambamo wanafunzi wamo na moto unatua kwa unyeti, kwa namna ya miali ya moto, juu ya kichwa cha kila mmoja. Na unyeti huo pia ni tabia ya utendaji wa Mungu ambayo tunaipata mara nyingi katika Biblia.” Na ni nzuri kuona jinsi mkono ule ule wenye nguvu na wenye nguvu ambao kwanza ulichimba madongoa ya tamaa, kisha hupanda kwa ustadi mimea midogo ya wema, "huinyunyizia," huitunza na kuilinda na upendo, ili ikue na kuwa na nguvu, na tunaweza kufurahiya, baada ya uchovu wa kupigana dhidi ya uovu, utamu wa huruma na ushirika na Mungu. Hivi ndivyo Roho alivyo: nguvu, hutupatia nguvu za kushinda, na pia umaridadi. Tunazungumza juu ya upako wa Roho, Roho hututia mafuta, yuko pamoja nasi.

Misa ya Pentekoste
Misa ya Pentekoste

Kama vile sala nzuri ya Kanisa la kale inavyosema: “Upole wako ukae pamoja nami, ee Bwana, na matunda ya upendo wako!" (Odes of Solomon, 14.6). Roho Mtakatifu, akiwa ameshuka juu ya wanafunzi na kujiweka karibu - yaani, "paraclete" Mfariji - anatenda kwa kubadilisha mioyo yao na kutia ndani yao "ujasiri unaowasukuma kusambaza kwa wengine uzoefu wao wa Yesu na tumaini linalowahuisha” (Mtakatifu Yohane Paulo II, Redemptoris missio, 24). Kama vile Petro na Yohane walivyoshuhudia baadaye mbele ya Baraza walipojaribu kuwalazimisha “wasiseme kwa njia yo yote wala kufundisha kwa jina la Yesu” (rejea:Mndo 4:18); watajibu: “Hatuwezi kukaa kimya juu ya yale tuliyoyaona na kuyasikia” (Mdo 4,20). Na kujibu hili wana nguvu za Roho Mtakatifu.

Papa wakati wa Misa ya Pentekoste 19 Mei 2024
Papa wakati wa Misa ya Pentekoste 19 Mei 2024

Baba Mtakatifu Francisko aidha amesema: “Na hii pia ni muhimu kwetu sisi, ambao tumekuwa na Roho kama zawadi katika Ubatizo na Kipaimara. Kutokana na Karamu kwenye  la Basilica hii, kama Mitume, tunaalikwa hasa leo hii kutangaza Injili kwa kila mtu, “siku zote tukienda mbele zaidi, sio tu kwa maana ya kijiografia, lakini pia zaidi ya vikwazo vya kikabila na kidini, kwa utume wa kweli wa ulimwengu wote.” (Redemptoris missio, 25). Na shukrani kwa Roho tunaweza na lazima tufanye kwa nguvu sawa na kwa wema sawa. Kwa nguvu zile zile: yaani, si kwa majivuno na misimamo mikali:, kwa sababu Papa amesisitiza kuwa “Mkristo si mbabe, nguvu zake ni nyingine, na nguvu za Roho; si hata kwa mahesabu na ujanja, bali kufanya hivyo kwa nguvu inayotokana na uaminifu wa ukweli, ambayo Roho hufundisha kwa mioyo yetu na kufanya kukua ndani yetu.”

Na kwa hivyo tujisalimishe, kwa Roho, na hatujisalimishi kwa nguvu za ulimwengu, lakini tuendelee kuzungumza juu ya amani kwa wale wanaotaka vita, kuzungumza juu ya msamaha kwa wale wanaopanda kisasi, kuzungumza juu ya kukaribisha na mshikamano kwa wale wanaofunga milango na kuweka vizuizi, kuzungumza juu ya maisha kwa wale wanaochagua kifo, kuzungumza juu ya heshima kwa wale wanaopenda kudhalilisha, kutukana na kutupa, kuzungumza juu ya uaminifu kwa wale wanaokataa kifungo chochote, kuchanganya uhuru na ubinafsi wa juu juu, usio wazi na utupu.” Baba Mtakatifu ameongeza: “Bila kuruhusu sisi wenyewe kutishwa na magumu, wala kwa dhihaka, wala upinzani ambao, kama ilivyokuwa zamani, haukosi kamwe katika maisha ya kitume (rej. Mndo 4:1-31).

Misa ya Pentekoste
Misa ya Pentekoste

Na wakati huo huo tunafanya hivyo kwa nguvu hii, tangazo letu linataka kuwa na ukarimu, kuwakaribisha kila mtu  na tusisahau hili: kila mtu, tusisahau mfano huo wa wageni wa karamu ambao hawakutaka kwenda: Na hivyo “enendeni kwenye njia panda za barabara na kuleta kila mtu, mzuri na mbaya, kila mtu.”.. Roho hutupatia nguvu ya kwenda mbele na kuita kila mtu, kwa wema huo… inatupatia wema wa kukaribisha kila mtu. Sisi sote, kaka na dada, tunalohitaji kubwa la tumaini, ambalo sio matumaini tu, hapana, ni kitu kingine. Tunahitaji tumaini, tumaini linafikiriwa kama nanga, pale, ufukweni, na sisi, tukiwa na kamba ili kuelekea tumaini. Tunahitaji matumaini, tunapaswa kuinua macho yetu katika upeo wa amani, udugu, haki na mshikamano. Hii ndiyo njia pekee ya maisha, hakuna nyingine.

Misa ya Pentekoste
Misa ya Pentekoste

Bila shaka, kwa bahati mbaya, mara nyingi haionekani kuwa rahisi, kiukweli wakati mwingine njia huonekana kuwa ya mateso na ya kupanda, ni kweli.” Lakini sisi tunajua kwamba hatuko peke yetu, tuna uhakika huu kwamba kwa msaada wa Roho Mtakatifu, pamoja na zawadi zake, pamoja tunaweza kutembea na kuifanya iweze kupitika  zaidi  hata kwa wengine pia. Baba Mtakatifu Francisko aidha amewambia waamini kwamba: “tufanye upya imani yetu mbele ya Mfariji karibu nasi, na tuendelee kuomba: Njoo, ee Roho wa Muumba, uzitie nuru nia zetu, uijaze mioyo yetu neema yako, uongoze hatua zetu, uipatie dunia amani yako.” Amina. Amehitimisha. 

Katika misa hiyo maombi yalikuwa ni ya ulimwengu ambapo ombi  kwa lugha ya kichina: "Baba wa Mwanga utakatifuze Kanisa na sakramenti za Pasaka ili liweze kuangazwa katika Ulimwengi Neema ya Umoja Kidugu."

Misa ya Pentekoste
Misa ya Pentekoste

Kwa lugha ya Kifilippino: "Mungu wa Maisha unayelisha mawazo ya amani kwa ubinadamu mzima, uwajalie watawala wa mataifa ili kutafuta daima mazungumzo na maelewano kati ya watu."

Kwa lugha ya kifaransa: "Baba wa kila faraja unayetunza kila kazi ya mikono yake uwajalie wanaoteseka kiroho na kimwili ili wasikie ukaribu wa Jumuiya ya kikristo."

Waamini wa mataifa mbali mbali
Waamini wa mataifa mbali mbali

Na kwa lugha ya Kiswahili: "Baba wa Upendo ambaye hutoa karama za Roho wako Mtakatifu kwa ukarimu ruhusu familia kukua kwa furaha katika ukarimu na upendo wa kiinjili."

Misa ya Papa ya Pentekoste 19 Mei
19 May 2024, 12:14