2024.06.06  Papa amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Makleri. 2024.06.06 Papa amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Makleri.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Fransisko:Mafunzo ya seminarini hayatoshi yanahitaji mwendelezo wa kudumu!

Papa amekutana na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Makleri.Katika mkutano huo amesisitiza mambo matatu:malezi,umakini wa miito na huduma ya ushemasi wa kudumu ambapo utambulisho ndiyo kiini cha tafakari:“Zingatieni ishara za Roho,mkiwa wakomavu katika mwelekeo wa kibinadamu na wa kiroho ili kutafuta lugha zinazofaa kwa ajili ya uinjilishaji.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican katika Ukumbi wa Clementine tarehe 6 Juni 2024 na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Makleri ambapo katika mkutano wao wamejikita katika mambo matatu: malezi endelevu ya mapadre, kuhamasisha miito na ushemasi wa kudumu. Katika hotuba yake Papa Francisko alisisitiza jinsi ilivyo muhimu kwa mapadre kuishi ndani ya mtandao wa mahusiano ya kidugu kwa sababu safari haifanywi peke yao na kupendekeza ubunifu hasa kwa kumsikiliza Roho Mtakatifu ili kukabiliana na changamoto za sasa.” Papa akianza tafakari yake amewasalimu kwa moyo mkunjufu  huku akitumia fursa hiyo kutoa shukurani zake kwa mapadre na mashemasi wa dunia nzima na kusema: “Mara nyingi nimeonya dhidi ya hatari za ukasisi na mambo ya ulimwengu wa kiroho, lakini ninajua vizuri sehemu  kubwa ya mapadre wengi wanafanya yote wawezayo kwa ukarimu na roho ya imani kwa ajili ya mema ya watu watakatifu wa Mungu, wakibeba uzito wa dhiki nyingi na kukabiliana na changamoto za kichungaji na kiroho ambazo wakati mwingine si rahisi.”

Papa amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Makleri
Papa amekutana na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Makleri

Papa Francisko alipenda pia kusema neno juu ya kila moja ya mada tatu ambazo zimekuwa katika kazi ya Mkutano Mkuu akianza na ile kuu ya mafunzo ya mapadre. Papa amesema: “Mafunzo ni ambayo, lazima yawe ya kudumu, hata zaidi katika ulimwengu unaobadilika kila mara kama huu wa sasa. Kwa hiyo haiwezekani kufikiri kwamba mafunzo yaliyopokelewa katika Seminari yatatosha. Badala yake, tunaitwa kuunganisha, kuimarisha na kuendeleza kile tulicho nacho katika Seminari, kwa njia inayotusaidia kukomaa katika mwelekeo wa kibinadamu, kukua kiroho, kutafuta lugha zinazofaa kwa uinjilishaji, kuimarisha kile tunachohitaji, kushughulikia vya kutosha masuala mapya ya wakati wetu.”

Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Wakleri
Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Wakleri

Suala la upweke ambalo mara nyingi mapadre wanakumbana nalo limekuwa pia chachu kwa  Papa Fransisko ambapo amesema: “Safari haifanywi peke yako, akibainisha kwamba ni mapadre wangapi ambao hawawezi kutegemea neema ya kusindikizwa na bila mwokozi huyo anayewakilishwa na hisia ya kuwa mali. Kwa njia hiyo kufuma mtandao imara wa mahusiano ya kidugu ni kazi ya kipaumbele ya malezi endelevu hasa kuanzia kwa “Askofu, mapadre kati yao wenyewe, jumuiya kuelekea wachungaji wao, wanaume na wanawake watawa, vyama vya kitume, harakati kwamba ni muhimu mapadre wajisikie kuwa nyumbani.” Kama Baraza la Kipapa la Makleri, Papa Francisko aidha amebainisha kuwa tayari limeanza kutengeneza mtandao wa kimataifa kwa njia hiyo ameongeza kusema: Ninapendekeza mfanye kila muwezalo kuhakikisha kuwa wimbi hili linaendelea na kuzaa matunda duniani kote."

"Kupungua kwa miito ya kipadre na maisha ya kuwekwa wakfu ni moja ya changamoto kubwa kwa Watu wa Mungu, Papa Francisko, alisisitiza lakini mgogoro huo pia unahusu wito wa ndoa. Kwa sababu hiyo, alieleza, katika ujumbe wa  hivi karibuni zaidi  katika  Siku ya Kuombea Miito Ulimwenguni, ili kutilia mkazo wa kuombea miito yote ya Kikristo, hasa kwa wito wa kimsingi ambao ni kufuasa,  unaowaunganisha wabatizwa wote.” Papa hata hivyo ameonya kwamba: “Hatuwezi kujisalimisha kiukweli kwamba kwa vijana wengi hawana dhana ya kutoa uhai na kwamba imetoweka kabisa kwenye mtazamo wa upeo wao. Badala yake, tunapaswa kutafakari pamoja na kubaki makini kwa ishara za Roho na kwamba wanaweza kutekeleza jukumu hili kwa shukrani kwa Shirika la Kazi za Kipapa la Miito ya Kipadre. "Ninawaalika muanzishe tena ukweli huu, kwa njia zinazofaa nyakati zetu.”

Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Makleri.
Mkutano wa Papa na washiriki wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Kipapa la Makleri.

Baba Mtakatifu katika hotuba yake amekabiliana na mada ya tatu ya kikao hicho kuhusu: Ushemasi wa kudumu, ambao utambulisho wake maalum unatiliwa shaka leo hii. Mwaliko wa Papa ni kuchangia katika tafakari ya huduma hii kama ilivyopendekezwa na ripoti ya muhtasari wa kikao cha kwanza cha mkutano mkuu wa kawaida wa Sinodi ya Maaskofu wa mwezi  Oktoba 2023, unaolenga  zaidi ya yote “ushemasia wa  upendo na huduma kwa maskini.” Kusindikiza na tafakari na maendeleo haya ni kazi muhimu sana ya Baraza la Kipapa la Makleri. Baba Mtakatifu amelihimiza Baraza hilo kufanyia kazi kwa hilo na kuweka nguvu zote muhimu katika kukabiliana nalo.  Aidha ametoa mwaliko huo zaidi ili watu wa Mungu wawe na wachungaji kadiri ya moyo wa Kristo, wakisindikizwa na Maria, kielelezo cha kila wito.

Hotuba ya Papa kwa Baraza la Kipapa la Makleri
06 June 2024, 17:49