Tafuta

2024.06.06, Papa akutana na Watawa wa mashirika mawili:wa Mtakatifu Felice wa Cantalice na Mabinti wa Mama Yetu wa Huruma 2024.06.06, Papa akutana na Watawa wa mashirika mawili:wa Mtakatifu Felice wa Cantalice na Mabinti wa Mama Yetu wa Huruma   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa akutana na watawa wa Mtakatifu Felice na Mabinti wa Mama Yetu wa Huruma

Baba Mtakatifu Francisko akikutana mjini Vatican na mashirika hayo ya kitawa wakiwa katika fursa ya Mkutano mkuu amewahimiza kufanya upya mshikamano wao kwa mapenzi ya Roho Mtakatifu katika uaminifu kwa nadhiri walizoweka na kwa unyenyekevu kwa utendaji wa Roho.Wajikabidhi kwake daima kwa ukarimu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na watawa wa shirika la Mtakatifu Felice wa Cantalice pamoja na Shirika la Mabinti wa Mama Yetu wa Huruma, mjini Vatican, Alhamisi tarehe 6 Juni 2024 ambapo akianza na salamu kwa namna ya pekee mama wakuu wa mashirika hayo na kuwashukuru kufika kwao. Hawa wamefika hapo wakiwa wanaadhimisha Mikutano Mikuu na kwamba ni vizuri katika fursa hiyo kufika kukutana na mfuasi wa Petro ili kumweleza juu ya shughuli zao,  za huduma kwa Mungu na kwa Kanisa. Huduma kwa hakika ni jambo ambalo linaunganisha shughuli za waanzilishi wao, wamefika licha ya kutoka sehemu tofauti lakini wakati huo huo ni  kipindi cha kihistoria cha karne ya 19.

Papa amekutana na mawatawa wa mashirika mawili
Papa amekutana na mawatawa wa mashirika mawili

Baba Mtakatifu amefikiria kipindi cha Sofia Camilla Truszkowska ambaye baadaye akawa Sr Angela Maria Mwanzilishi wa Shirika la Mtakatifu Felix wa Cantalice  huko Walsawnchini Poland, iliyokuwa inapitia katika vita, kwa huduma ya watoto, walemavu na vijana walio hatarini. Papa amesema inashangaza kuanzisha jambo hili  ambapo katika tukio  hilo mbele ya mizozo ya kivita ilipozidi kuwa mbaya, yeye na dada zake waliamua kuwatibu majeruhi wote, wa upande wowote.

Na kwa hiyo walipewa makosa kwa kusalitiwa na kazi ikasitishwa na mamlaka ya kiraia. Papa amefikiria jinsi ambavyo yupo Mungu mpaji, maana, baada ya kitambo ilifufuka , labda shukrani kwa sadaka zao na ujasiri wa kueneza  tena zaidi hadi Ocean na Amerika, daima chini ya msukumo wa huduma, wakati huu kwa msaada kwa wahamiaji wa Poland. Na tangu wakati huo imeenea katika sehemu nyingine nyingi za dunia. Hii ni ishara nzuri kwao, hasa wakati huu wakiwa wanafanya mkutano mkuu.

Picha ya Pamoja na watawa wa mashirika mawili
Picha ya Pamoja na watawa wa mashirika mawili

Ishara ambayo inawaalika wasiogope kupoteza usalama wa miundo na kitaasisi, ila  tu wabaki waaminifu kwa upendo! Na itawafanyia vizuri kukumbuka hili katika mikutano yao, kukukumbusha kwamba miundo sio kitu ni njia tu. Jambo kuu ni upendo wa Mungu na jirani, unaotumiwa kwa ukarimu na uhuru: “Kwa maana upendo wa Kristo unatumiliki” (2 Kor 5:14), kulingana na maneno ya Mtakatifu Paulo ambaye wamemchagua kuwa kiongozi wa kazi zao.

Baba Mtakatifu akigeukia pia shirika jingine amesema kuwa: “ na wakati huo huo wa kipindi, Nchini Italia huko Savona, kijana mwingine , mwanamke Benedetta Rosella baadaye akaitwa Sr Maria Giuseppa, alianza chini ya uongozi wa Askofu, kazi nyingine , nayo ikiwa kwa huduma ya maskini, watoto na vijana wasichana.  Hawa ni Mabinti wa Mama Yetu wa Huruma. Hata Benedettta alikiwa kijana mwenye uamuzi, aliamua kwamba, licha ya kuwa maskini, alikuwa ameacha maratajio ya urithi tajiri ili kufuata mwito wa kuwekwa wakfu, akichagua kauli mbiu: “Moyo kwa Mungu, mikono ifanye kazi!” Alianza safari mpya ya mapenzi na njia duni lakini zenye nguvu: “msalaba, picha ya Mama wa Huruma sanamu ya taji la miiba mitano, tayari kila wakati kutekeleza aina yoyote ya huduma kwanza. Na kwa wakati huu Papa ameoma aruhusiwe kushirikisha kumbukumbu yake  kibinafsi na wao

Papa akutana na watawa wa mashirika mawili
Papa akutana na watawa wa mashirika mawili

Papa akieleza amesema “Kwa hakika ni katika mojawapo ya shule zenu, huko Buenos Aires, katika kitongoji cha Flores, ambapo miaka mingi iliyopita nilipokea Sakramenti za kwanza za Kikristo. “Ninawezaje kumsahau Sr. Dolores mpendwa, ambaye nilijifunza mengi kutoka kwake na ambaye niliendelea kumtembelea kwa muda mrefu sana? Kwa hili ninamshukuru Bwana na ninyi nyote, kwa sababu huduma yangu ya sasa kwa Kanisa pia ni tunda la mema niliyopokea, nikiwa mdogo, kutoka katika familia yenu ya kitawa.” Papa kwa kuongeza “Tazameni jinsi sisi sote tulivyo vyombo katika mikono ya hekima ya Mungu! Ni nani anayeweza kufikiria atapata nini kutoka kwa ndiyo yetu ndogo?”  Kwa hiyo, Baba Mtakatifu Francisko kwa kuhitimisha amependa kuhimiza kufanya upya mshikamano wao kwa mapenzi ya Roho Mtakatifu katika uaminifu kwa nadhiri walizoweka na kwa unyenyekevu kwa utendaji wa Roho. Wajikabidhi Kwake na kutoa kila kitu, daima, kwa ukarimu. Papa anasali kwa ajili yao na hata wao amewaomba wasisahau kusali kwa ajili yake.

Hotuba ya Papa kwa watawa
06 June 2024, 16:24