Papa atembelea kwa mara ya tatu Shule ya Sala katika Parokia ya Mtakatifu Brigida,Roma
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
Mazungumzo na karibu familia thelathini, wazee, wanandoa na vijana, waliarifiwa dakika ya mwisho ya kuwasili kwa Papa ambapo alifika katika kitongoji cha Palmola, Borgata Ottavia, nje kidogo ya magharibi ya Roma, kwa mkutano wa tatu wa “Shule ya sala” kwa mtazamo wa maandalizi ya Jubilei 2025. Kwa njia hiyo baada uzoefu wa watoto na vijana, katika Parokia zilizotangulia, tarehe 6 Juni 2024 alasiri, Baba Mtakatifu Francisko alitaka kukutana na familia, katika viunga vya magharibi vilivyokithiri vya jiji la Roma. Wakati huu hazikuwa kumbi za parokia au sinema, lakini ni karakana za mitaa iliyo na sakafu ya changarawe, ukuta wa matofali, miti na mimea ya kupanda na vifuniko pande zote na magari yaliyoegeshwa ndani na wakaazi wakitazama kutoka kwenye balkoni zao.
Katikati kiliwekwa kiti cha mkono; walioketi mbele walikuwa karibu familia thelathini, wanandoa wenye watoto, vijana, waamini wa kanisa la karibu la Mtakatifu Brigid wa Uswiss, baadhi waliofika baada ya mkutano walikuwa tayari wameevaa kandambili au nguo za nyumbani. Kama ilivyokuwa yule mwanamke ambaye alishuka ngazi huku akijaribu kurekebisha nywele zake na kusema: “Ee Mungu, ni mshangao gani na wangeweza kuniambia hapo awali!” Ilikuwa ni hali mpya kabisa kwa uteuzi wa tatu wa “Shule ya sala ambayo ni mfululizo wa mikutano ya Papa jijini Roma katika Mwaka wa Sala kwa kuzingatia mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya 2025. Kulikuwa na wanandoa wa wazazi wapya, babu na bibi, kikundi cha vijana cha parokia, watoto wachanga na kikundi cha wanawake wahamiaji kutoka Senegal, mtu wa Kiorthodox, rais wa Manispaa ya XIV, Marco Della Porta. Kwa kifupi, wanadamu mbalimbali ambao wakati wa mwisho walijulishwa kuhusu saa hii maalum ya katekisimu ya Papa alasiri.
Fiat 500 L iliingia mwendo wa saa kumi na moja jioni kwenye barabara panda ya jengo kupitia Palmarola huku kuta zikiwa bado zinaendelea kujengwa. Kimya cha awali, mitazamo michache ya macho yaliyovingirisha, na kutafuta simu kwa haraka tayari kurekodi tukio hilo,ambapo Papa akisalimu alianza kusema: "Habari za jioni “na kutoka hapo makofi na kawaida “W the Papa!” Safari miongoni mwa watu ilikuwa fupi, iliyochochewa na zawadi ya peremende, na baadhi ya selfie zilizoibiwa, na bibi mmoja aliyembembeleza Papa na mwingine aliyejitokeza kusema: “Ni nani kwa bahati angeniombea mimi mama? na Papa Francis ambaye alimbariki. Akiwa ameketi kwenye kiti cha mkono, Papa Jorge Mario Bergoglio kisha akaanzisha swali na jibu pamoja na waliokuwepo. Kwanza kabisa alitazama kufurahishwa na hali isiyo ya kawaida: “Ukuta ... mimea ... nyanya ...”, kisha akasalimu kundi mbele ya macho yake: “Nyinyi ni familia, vijana, vijana wadogo , wazee, familia daima.”
Na Papa alizungumza juu ya familia, juu ya changamoto na shida zake, juu ya uzuri na uwezekano wa Kanisa na jamii, katika kile alichokifafanua kwa utani kama “mahubiri” na katika mazungumzo yaliyofuata yaliyochukua karibu robo tatu ya saa. “Tunatetea familia, ambayo ni oksijeni kwa kulea watoto,” alisema. Kiukweli, kuna mabishano, kinzani, wakati mwingine hata kutengana. Papa Francisko aliita “Dhoruba”, lakini lazima msikate tamaa. Ikiwa wazazi wanagombana ni kawaida, lakini wana nafasi ya kufanya amani kabla ya siku kuisha, kwa sababu vita baridi siku inayofuata ni mbaya,” Papa Francisko alirudia mara kadhaa, akirudia maneno matatu muhimu ambayo ni rahisi sana lakini kwa wakati mmoja ni muhimu kufanya uhusiano ufanyike na haya ni kuomba: “Samahani, kupiga hodi na kushukuru”
Hata shukrani rahisi zaidi kama vile: “Asante kwa kupika chakula hiki cha jioni nzuri ...”. Na pale ambapo maneno hayafikii, lakini “ishara ndogo inatosha kufanya amani na kuanza tena siku inayofuata.” Hizi ni hatua ndogo za kila siku ambazo ni muhimu hasa kwa watoto. Kwani “Watoto wanatutazama,” Papa alisema, akinukuu filamu ya 1944 ya Vittorio De Sica. “Watoto huwatazama baba na mama” na kuteseka wanapoona kwamba hawaelewani.” Kiukweli, Papa alipendekeza wazazi waliotengana wasisemezane vibaya bali wawaelimishe watoto wao kuheshimiana. Vijana wanne kutoka parokia hiyo walimwuliza Papa jinsi gani inavyowezekana kuongeza imani leo hii: “Njia pekee ni ushuhuda,” alijibu. Na aliacha jukumu maalum kwa vijana kwamba: “Mna jukumu la kubeba historia mbele.” Na fanya hivyo bila kubakimmeanguka. Moja ya mambo mazuri kuhusu vijana ni kwamba wanainuka. Sote tunaanguka maishani, lakini jambo muhimu sio kubaki chini unapoteleza”
Mwanamume mmoja alionesha tamaa ya kuwa na kanisa kubwa zaidi katika eneo hilo ambalo lingeweza kuwa mahali pa kukutania kwa wakaaji wote majirani hao. Pia Papa alisemaza kuzungumza juu ya Kanisa kama jumuiya ya watu, na sio tu kama sehemu za ibada, ambazo hazipo katika eneo hilo la Roma kuliko katika maeneo mengine ya jiji. Mwanamke aliyetanguliwa na labda alilia alitoa shukrani zake kwa Papa: “Kutoka Siku ya Watoto Duniani, kutokana na hotuba zake, tunachopata ni wewe ni baba ambaye unaendesha jumuiya kubwa katika mambo madogo, katika mambo ya kweli. Kukuona hapa mbele ya ukuta wa matofali ndio jambo la kufurahisha zaidi ...” Kesho tunafanya sherehe ya parokia, mvua inanyesha ndani, hatuna hata simenti lakini nani anajali, tutafanya hivyo. Na uwepo wako unatufanya tujisikie kuwa wewe ni sehemu ya jamii yetu.” Alsisitiza mwanamke huyo.
Kati ya vicheko na nderemo, Papa Francisko alilenga kwa usahihi jambo hili la mwisho: “Kanisa linaanza kufanywa katika jumuiya.” Kwa mara nyingine tena wito ulirudi wa kutowapuuza wazee na kuwatunza watoto: “Mambo mawili... Parokia ambayo watoto hawasikilizwi na wazee wanafutwa si jumuiya ya Kikristo ya kweli. Msisahau, wazee ni kumbukumbu na watoto ni ahadi. Msisahau wazee ambao ni kumbukumbu ya watu wa Mungu,” alisisitiza Papa: “Ni kweli kwamba wazee wakati mwingine, kiukweli, tunawachosha. Daima wanazungumza juu ya kitu kimoja: kuhusu vita nk ... lakini tuna huruma kubwa sana.” Na watoto “wanaelewa lugha ya huruma.” Papa alisisitiza.
Wakizungumzia watoto, baba mmoja wa mapacha, alimuuliza Papa jinsi ya kudumisha imani katika nyakati hizi ngumu na jinsi ya kuwaweka watoto wao karibu na Kanisa, hata baada ya Kipaimara, maana mara baada ya sakramenti hiyo wengi hupotea. "Ushuhuda,” ilikuwa ni jibu. Kwanza kabisa, kile kinachozaliwa katika familia: “Shauri la kwanza ni kupendana kati ya wazazi kwa sababu watoto lazima waweze kuhisi kuwa mama na baba wanapenda kila mmoja. Ikibidi kugombana, usifanye hivyo mbele ya watoto, wapeleke kitandani na kubishana kadri unavyotaka.” Sawa msingi huo ni mazungumzo na watoto wenu. Msiache kamwe kuzungumza nao. Elimu inafanywa kwa njia ya mazungumzo, bila kutowaacha peke yao, bila kuwa na kashfa au kuwashinikiza, lakini pia kuwaacha huru wakati fulani.”
Papa alipendekeza na zaidi akuongeza kuwamba: “Hivi ndivyo wanavyoelimisha kwa uhuru. Waelewe kwamba wanaweza kuzungumza lolote. Kwa kila kitu. Papa kisha alisisitiza: “Mambo ya maisha hufunzwa nyumbani, si kutoka kwa wengine wanaojua wanachofundisha”. Salamu kwa kila mmoja wa waliohudhuria ilihitimisha mkutano na Papa ambaye alisambaza mkumbatio na rozari, ambaye alikubali maombi mbalimbali ya picha na ambaye pia alizungumza na “bibi Maria" iliyounganishwa kupitia Skype kwa simu ya mjukuu wake: "Hi! niombee. Asante!" Kama zawadi kwa familia hizi, Papa Fransisko aliacha mchoro ukimuonesha Bikira Maria akiwa na Mtoto Yesu: “Kwa hiyo mnaweza kuuweka ukulu”. Kumbukumbu inayoonekana ya kukutana ambayo pengine hakuna hata mmoja wa wakazi wa sehemu hii ya pembeni ya Roma angeweza kuwaza.