Papa atuma telegramu ra rambi rambi kufuatia kifo cha Kardinali Kelvin Edward Felix
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe Mosi Juni 2024 ametuma Telegramu za rambi rambi kufuatia na kifo cha Kardinali Kelvin Edward Felix kilichotokea tarehe 30 Mei 2024. Katika Telegram hiyo, Baba Mtakatifu anaelekeza kwa Askofu Mkuu Gabriel Malzaire wa Jimbo Kuu la Castries huko Jamhuri ya Dominica. Baba Mtakatifu Francisko anabainisha kuwa baada ya kupokea taarifa za kifo hicho cha Askofu Mstaafu wa Castries, Kardinali Kelvin Edward Felix. Salamu hizo za rambi rambi na sala ni kwake yeye, makuhani, watawa na waaamini walei wa Jimbo Kuu, ikiwa ni pamoja na Kanisa la Indiana ya Magharibi. (West Indias).” Baba Mtakatifu Francisko anamkumbuka “kwa kina na shukrani Kardinali huyo kwa miaka mingu aliyojikita katika huduma ya kiaskofu huko Mtakatifu Lucia hasa kwa jitihada za kukuza elimu kwa vijana na michango yake kwa Kanisa kupitia Carribien.” Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu anabainisha kuwa: “kwa hiari kabisa ninaungana nanyi katika kuiwakilisha roho yake kwa upendo na huruma za Baba Yetu wa Mbinguni. Kwa wale wote wanaoshiriki Misa ya Mazishi ya Mkristo na wote wanaoomboleza kufuatia na kifo chake kwa tumaini la uhakika wa ufufuko”, Papa ametoa "Baraka zake ziwe faraja na amani katika Bwana aliyefufuka."
Wasifu wake
Kardinali Kelvin Edward Felix, Askofu Mkuu mstaafu wa Castries (Mtakatifu Lucia, Antilles, India ya Magharibi, alizaliwa huko Roseau, nchini Dominica, tarehe 15 Februari, 1933. Alisoma katika seminari ya Mtakatifu Yohane Vianney huko Trinidad. Alipewa Daraja Takatifu ya Upadre tarehe 8 Aprili 1956. Alikuwa Padre wa kwanza wa Jimbo kutoka Roseau na Padre wa kwanza wa Kikatoliki kupewa daraja huko Jamhuri ya Dominika. Baada ya miaka kadhaa ya kazi ya uchungaji huko Dominica, kuanzia 1962 alijiunga na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis Xavier huko Nova Scotia, ambako alipata shahada ya elimu mwaka 1963; mnamo 1967, alimaliza Shahada ya Uzamili katika sosholojia na anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Notre Dame huko Indiana. Aliendeleza masomo yake ya uzamili katika sosholojia katika Chuo Kikuu cha Bradford, Yorkshire, Uingereza, na kuhitimu mwaka wa 1970.
Baada ya miaka kadhaa ya kazi ya uchungaji huko Dominika, kuanzia 1962 alihudhuria Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis Xavier huko Scotia Mpya, ambako alipata shahada ya elimu mwaka 1963; mnamo 1967, alimaliza Shahada ya Uzamili katika sosholojia na anthropolojia katika Chuo Kikuu cha Notre Dame huko Indiana. Aliendeleza masomo yake ya uzamili katika sosholojia katika Chuo Kikuu cha Bradford, Yorkshire, Uingereza, na kuhitimu mwaka wa 1970. Akiwa Uingereza alifanya juhudi kubwa kusaidia jamii ya wahamiaji wa Dominika. Alifundisha katika Seminari ya Mtakatifu Yohane Vianney na aliwahi kuwa profesa wa Sosholojia katika Chuo Kikuu cha India Maghari cha Mtakatifu Augustino.
Aliteuliwa kuwa askofu mkuu wa Castries tarehe 17 Julai 1981, na kuwekwa wakfu wa kiaskofu mnamo tarehe 5 Oktoba mwaka huo huo. Utawala wake wa kichungaji wa Jimbo uliendelea hadi tarehe 15 Februari 2008. Amewahi kuwa rais wa Baraza la Makanisa ya Visiwa vya Carribien na , Rais wa Baraza la Maaskofu wa Antilles na msimamizi wa kitume wa jimbo la Bridgetown, Barbados, na kama mjumbe wa Baraza la Kipapa, Baraza la Kipapa la Familia, Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na Baraza la Sinodi la Amerika Kusini. Aliundwa na kutangazwa kuwa Kardinali na Baba Mtakatifu Francisko katika Kikao cha Baraza la tarehe 22 Februari 2014, kwa Jina kupewa Kanisa la Mama yetu wa Afya huko Primavalle). Kadinali Kelvin Edward Felix alifariki tarehe 30 Mei 2024.