Papa:Ekaristi itufanye kugeuka kuwa mkate uliomegeka kwa ajili ya wengine

Papa katika tafakari ya Dominika ya Siku Kuu ya Mwili na Damu ya Yesu kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana tarehe 2 Juni 2024 kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican,ameuliza maswali:je mimi ninatunza maisha yangu kwa ajili yangu tu au ni zawadi kama Yesu?Je ninatumia muda wangu kwa ajili ya wengine au nimefungwa katika udogo wangu?Na katika hali za kila siku,ninajua kushirikishana au ninatafuta daima mafao yangu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko alianza tafakari yake akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume akiwageukia waamini na mahujaji waliofika katika kusali Sala ya Malaika wa Bwana, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 2 Juni 2024 wakati Mama Kanisa katika Ulimwengu mzima anaadhimisha Siku Kuu ya Mwili na Damu ya Yesu Kristo. Katika tafakari hiyo Papa amesema: “Nchini Italia na sehemu nyingine leo ni siiku Kuu ya Corpus Domini. Injili ya liturujia ya siku inasimulia Karamu Kuu ya Yesu (Mk 14,12-26), wakati Bwana alitimiza ishara ya kukabidhi, kwa hakika katika mkate uliomegwa na kikombe kilichotolewa kwa wanafunzi.  Ni Bwana anayejitoa kwa ubinadamu wote na anajitoa yeye mwenyewe kwa maisha ya Ulimwengu.

Umati wa waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro pamoja na mvua
Umati wa waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro pamoja na mvua

Baba Mtakatifu aliongeza kusema kuwa: “Katika ishara hiyo ya  Yesu kuumega mkate kuna mantiki moja muhimu ambayo Injili inasisitiza kwa maneno: “Aliwapa wao(Mk 14, 22). Tukazie katika moyo maneno hayo:” Aliwapa wao.” Papa alikazia. Akiendela alisema: “Ekaristi kiukweli inaalika awali ya yote ukuu wa zawadi.” Baba Mtakatifu ameongeza: “Yesu alitwaa mkate, si kwa sababu ya kula peke yake, bali kwa ajili ya kuumega na kuutoa kwa wanafanuzi, huku akiwaonesha kwa namna hiyo utambulisho wake na utume wake. Yeye hakuweka kwa ajili ya maisha yake, bali alitoa kwa ajili yetu; hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho, alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akiwa na mfano wa wanadamu ili aingie katika maisha ya milele(Fil 2,1-11). Kwa maisha yake yote, Yesu alijifanya zawadi.” Papa amekazia tena: “Tukumbuke hivyo kwamba maisha yake yote Yesu alijifanya zawadi.”

Mvua haikuwakataza waamini wasisali sala ya Malaika wa Bwana
Mvua haikuwakataza waamini wasisali sala ya Malaika wa Bwana

Papa akiendelea alisema kuwa: “tunatambua kuwa maadhimisho ya Ekaristi na kushiba na Mkate huo, kama tunavyofanya hasa Dominika, siyo tendo la utamaduni uliotengenishwa na maisha au wakati rahisi wa kufarijiwa kibinafsi tu; daima tunapaswa kukumbuka kuwa Yesu kwa kutwaa mkate, aliumega na akawapa wafuasi kuwa na Muungano na  Yeye na hivyo  unatufanya kugeuka hata sisi mkate uliomegeka kwa ajili ya wengine, kuushirikisha kwa kile ambacho sisi ni na kile ambacho tunapaswa kuwa. Mtakatifu Leone Mkuu alikuwa amesema: “Ushiriki wetu katika mwili na katika Damu ya Kristo sio kitu kingine zaidi ya kutufanya kugeuka kuwa kile ambacho sisi tunakula(Sermone XII sulla Passione, 7).

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Sala ya Malaika wa Bwana
Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Sala ya Malaika wa Bwana

Kwa hiyo sisi tumeitwa kufanya nini, Swali la Papa na kujibu; “kugeuka kuwa kile ambacho tunakula na kugeuka kuwa  Ekaristi, yaani watu ambao hawaishi tena kwa ajili yao binafsi(Rm 14,7), hapana, katika mantiki ya kujilimbikizia, kutumia hovyo, badala yake kuwa  ndiyo watu ambao wanatambua kufanya maisha yao binafsi kuwa zawadi kwa ajili ya wengine.” Baba Mtakatifu akiendelea  amesema “shukrani kwa Ekaristi tunageuka kuwa manabii na wajenzi wa ulimwengu mpya: tunaposhinda ubinafsi, na kujifungulia upendo, wakati tukikuza mahusiano ya udugu, tunaposhiriki katika mateso ya ndugu na kushirikishana rasilimali na yule mwenye kuhitaji, wakati tunakuwa tayari kuwekwa talanta zetu zote, kwa hiyo tunaumega mkate katika maisha ya Yesu.”

Papa akiwa dirisha la jumba la Kitume mjini Vatican
Papa akiwa dirisha la jumba la Kitume mjini Vatican

Baba Mtakatifu ameomba kwa hiyo tujiulize maswali: “je mimi ninatunza maisha yangu kwa ajili yangu tu au ni zawadi kama Yesu? Je ninatumia muda wangu kwa ajili ya wengine au nimefungwa katika udogo wangu? Na katika hali za kila siku, ninajua kushirikishana au ninatafuta daima mafao yangu.” Kwa kuhitimisha Papa amesema: “Bikira Maria ambaye alimpokea Yes, Mkate ulioshuka kutoka Mbinguni na kujitoa kabisa pamoja na Yeye atusaidie hata sisi kugeuka kuwa zawadi ya upendo, kuungana na Yesu wa Ekaristi.”

Tafakari ya Papa wakati wa Angelus 2 Juni 2024
02 June 2024, 14:26