2024.06.07 Papa Francisko akutana na Wanafunzi 35 wa Chuo cha Kipapa cha Kikanisa cha kidiplomasia. 2024.06.07 Papa Francisko akutana na Wanafunzi 35 wa Chuo cha Kipapa cha Kikanisa cha kidiplomasia.   (Vatican Media)

Papa Francisko akutana na wanafunzi wa Chuo cha Kipapa cha Kidiplomasia

Katika mkutano na wanafunzi 35 wa Chuo cha Kipapa cha Kikanisa,Papap ametoa mwaliko wa kuwafunza wanadiplomasia wa siku zijazo wa Vatican kwa ukaribu na watu wa Mungu hasa katika nchi za utume kama kinga yenye nguvu ya ulimwengu wa kiroho.Kwa mtazamo wa vita amesema:"vita vya dunia vimeganyika vipande vipande na kuelezea shughuli za Mabalozi ili kuhimiza mazungumzo kati yao na kuwatetea waathirika.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana mjini Vatican tarehe 7 Juni 2024  na wanafunzi 35  wa Chuo cha Kipapa cha Kikanisa, taasisi ambayo inatoa mafunzo kwa wanadiplomasia wa Vatican  wa Kanisa Katoliki kwa zaidi ya karne tatu. Mapadre hao walisindikizwa na Askofu Mkuu  Salvatore Pennacchio, Mchumi na Mkuu wa Mafunzo Monsinyo Gabriel Viola na Padre wa Kiroho, Padre Orlando Torres SJ. Akiitambulisha Jumuiya hiyo, Rais aliwatambulisha hasa wanafunzi kumi na wanne ambao, baada ya kumaliza masomo yao ya kitaaluma, wanajiandaa kuondoka katika miezi ijayo kwa Mwaka mmoja wa huduma ya Kimisionari. Baada ya kusikiliza wataokwenda, Papa Francisko katika hotuba yake alikumbusha maana ya ombi lake, alilolitoa miaka minne iliyopita kwa aliyekuwa Rais wa Chuo, Askofu  Joseph Marino kwamba: "wafunze wanadiplomasia wa siku zijazo wa Vatican kuwa karibu na Watu wa Mungu, hasa katika nchi za utume wa kimisionari, za mbali zaidi."

Papa akizungumza na wanafunzi wa chuo cha kipapa cha Kidiplomasia
Papa akizungumza na wanafunzi wa chuo cha kipapa cha Kidiplomasia

Hata hivyo pamoja na kuhuisha mioyo yao,  wakiwa wachungaji, litakuwa dawa yenye nguvu dhidi ya ulimwengu wa kiroho, hatari ambayo utumishi wa kidiplomasia unaweza kuwafichua. Kisha Papa Fransisko aliwashauri wanafunzi wote, hasa wamisionari walioaga, wao waweze kusoma na kutafakari Waraka wa  kitume wa Evangelii Nuntiandi wa mtangulizi wake Mtakatifu Paulo VI, ambao unabakia kuwa muhimu hadi leo hii. Wakati wa mazungumzo hayo, yakichochewa na baadhi ya maswali kutoka kwa wanafunzi, Papa Francisko alieleza juu ya sifa za mwanadiplomasia aliyeitwa kumwakilisha mbele ya Makanisa mahalia na familia ya Mataifa kwamba: “pamoja na ukaribu ulioelezewa mwanzoni mwa mkutano, ujasiri unahitajika, kwa kazi ambayo ni muhimu kadiri ilivyo ngumu, siku zote ikiambatana na uchaji wa Mungu, yaani, uhusiano mzito sana  na Bwana.”

Papa na wanafunzi wa Kidiplomasia wa chuo cha Kikanisa
Papa na wanafunzi wa Kidiplomasia wa chuo cha Kikanisa

Miongoni mwa mada zilizoguswa, yalikuwa ni marejeo ambayo hayakosekana,  ya muktadha wa  vita  vya ulimwengu “vilivyo megeka vipande vipande na ambavyo tunapitia, hata Ulaya.” Papa alikumbuka kazi ya Mabalozi wengi wa Kitume  katika maeneo yenye migogoro ili kuhimiza mazungumzo kati ya washindani na kutetea wahanga wa vita, kulingana na kanuni za sheria za kibinadamu. Hata hivyo maswaliyaliyofuata yalimruhusu Baba Mtakatifu kurejea ujuzi ambao wanadiplomasia wa baadaye wa kipapa wanapaswa kuukuza katika miaka yao ya mafunzo jijini Roma.

Waafunzi wa Chuo cha Kikanisa cha Kipapa
Waafunzi wa Chuo cha Kikanisa cha Kipapa

Hatimaye, kwa kupata msukumo kutoka katika Maadhimisho ya Siku Kuu ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, ambayo Mama Kanisa ameadhimisha tarehe 7 Juni, Baba Mtakatifu Francisko aliwaalika wanafunzi wa Chuo cha Kipapa cha Kikanisa kuwa "ni Mapadre wanaosamehe kila jambo kwa waamini wanaowageukia katika Sakramenti ya upatanisho". Papa alsema: “Kuwa, kama Balozi wa Kitume, wachungaji wa Kesho wenye huruma.” Baada ya kuomba kumkumbuka katika sala, Baba Mtakatifu Francisko  alihitimisha mkutano huo kwa kuwabariki na kuwasalimia waliohudhuria mmoja baada ya mwingine.

Papa akutana na wanachuo cha Kidiplomasia cha Kipapa
07 June 2024, 16:49