Padre Manuel Blanco Rodríguez Mfranciskani aliyekuwa na umri wa miaka 85 amefariki dunia kati ya usiku wa kuamkia Ijumaa tarehe 21 Juni 2024. Padre Manuel Blanco Rodríguez Mfranciskani aliyekuwa na umri wa miaka 85 amefariki dunia kati ya usiku wa kuamkia Ijumaa tarehe 21 Juni 2024. 

Papa Francisko Atoa Heshima za Mwisho Kwa Padre Muungamishi Wake

Padre Manuel Blanco Rodríguez Mfranciskani aliyekuwa na umri wa miaka 85 amefariki dunia kati ya usiku wa kuamkia Ijumaa tarehe 21 Juni 2024. Huyu alikuwa ni Padre muungamishaji wa Baba Mtakatifu Francisko, utume aliokuwa anautekeleza kila baada ya siku kumi na tano, kwa sababu Baba Mtakatifu mwenyewe anajiona kuwa ni mchungaji na mdhambi, anayehitaji huruma na msamaha wa Mungu. Ni mtu mwema, mwenye huruma, mpole na mnyenyekevu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Padre Manuel Blanco Rodríguez Mfranciskani aliyekuwa na umri wa miaka 85 amefariki dunia kati ya usiku wa kuamkia Ijumaa tarehe 21 Juni 2024. Huyu alikuwa ni Padre muungamishaji wa Baba Mtakatifu Francisko, utume aliokuwa anautekeleza kila baada ya siku kumi na tano, kwa sababu Baba Mtakatifu mwenyewe anajiona kuwa ni mchungaji na mdhambi, anayehitaji huruma na msamaha wa Mungu. Baba Mtakatifu baada ya kupata habari za kifo cha Padre Manuel Blanco Rodríguez, Dominika, tarehe 23 Juni 2024 asubuhi na mapema, alikwenda kutoa heshima zake za mwisho kwa Marehemu Padre Manuel Blanco Rodríguez. Baada ya kuwasili na kusalimiana na wenyeji wake, Baba Mtakatifu aliwaomba wote kujumuika pamoja naye kusali masifu ya asubuhi kwa ajili ya kumkumbuka na kumwombea Marehemu Padre Manuel Blanco Rodríguez.

Padre Manuel Blanco Rodriquez amefariki dunia tarehe 21 Juni 2024
Padre Manuel Blanco Rodriquez amefariki dunia tarehe 21 Juni 2024

Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya mazishi imeadhimishwa Jumatatu tarehe 24 Juni 2024 kwenye Kanisa la “Santi Quaranta Martiri na San Pasquale Baylon” lililoko eneo la Trastevere, Jimbo kuu la Roma ambako kwa takribani miaka 40 ameishi kwenye Kanisa hili. Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 23 Juni 2024 alimkumbuka Marehemu Padre Manuel Blanco Rodríguez kuwa ni kiongozi, muungamishaji, mtu mwema, mwenye huruma, mpole na mnyenyelevu. Baba Mtakatifu aliwakumbuka na kuwaombea Wafrancisko wote, waungamishaji na wahubiri waliojisadaka bila ya kujibakiza kwa ajili ya kulitukuza Kanisa sanjari na kuupamba mji wa Roma. Shukrani nyingi kwa wote hawa alisema Baba Mtakatifu Francisko.

Padre Manuel Blanco Rodriquez amefariki dunia tarehe 21 Juni 2024
Padre Manuel Blanco Rodriquez amefariki dunia tarehe 21 Juni 2024

Padre Manuel Blanco Rodríguez alizaliwa tarehe 6 Machi 1939 huko Camarzana de Tera, nchini Hispania. Kati ya mwaka 1993 hadi mwaka 1994 alikuwa ni Jaalimu wa Falsafa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antonianum, kilichoko mjini Roma. Kati ya mwaka 2002 hadi mwaka 2008 alikuwa ni Dekano Msaidizi, Kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2011 Dekano. Kati ya mwaka 2011 hadi mwaka 2014 Makamu Dekano. Itakumbukwa kwamba, tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2011 alikuwa ni Makamu Gambera, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Antonianum. Katika maisha na utume wake, amekuwa pia ni mwandishi mahiri wa vitabu.

Tanzia
25 June 2024, 15:03