2024.06.20 Papa amekutana na ujumbe wa Shirikisho la Kilutheri Duniani mjini Vatican. 2024.06.20 Papa amekutana na ujumbe wa Shirikisho la Kilutheri Duniani mjini Vatican.  (Vatican Media)

Papa Francisko kwa Walutheri:Yesu Kristo ndiye moyo wa uekumene!

Papa akikikutana na wajumbe kutoka Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni,amejikita kuelezea Jubilei inayokuja na 2025 na ukumbusho wa Baraza la Nikea: Yesu Kristo ndiye moyo wa uekumene.Sisi sote ni mahujai wa matumaini.Kumbukumu ya Mtaalimungu Ioannis Zizioulas:'tarehe ya muungano wa Wakristo itakuwa siku ya hukumu ya mwisho.'

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana na Uwakilishi wa Shrikisho la Kilutheri Ulimwenguni, Alhamisi 20 Juni 2024. Akianza hotuba yake, ameongozwa na kifungu cha barua ya Mtakatifu Paulo Mtume wa watu kisemacho: “Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu. (Rm 15,13). Amepanua ukaribisho kwa wote, wawakilishi wa Kanda ya Shirikisho la Kiluteri Duniani. Kwa namna ya pekee, ameshukuru kwa ukarimu, maneno na zawadi alizowewa na Rais mpya, Askofu Henrik Stubkjær; Kama vile salamu wa Mchungaji Anne Burghardt, ambaye kwa miaka kadhaa amejikita katika shughuli ya ukatibu Mkuu.

Papa amekutana na wajumbe wa Shirikisho la Kilutheri duniani
Papa amekutana na wajumbe wa Shirikisho la Kilutheri duniani

Baba Mtakatifu  amewashukuru aidha kwa ziara hiyo ambayo anaizingatia kama ishara muhimu ya udugu wa kiekumene. Kwa njia hiyo katika salamu zake za mwanzo alichagua maneno ya Mtume Paulo katika barua kwa Waroma ambayo yalisindikiza mashauriano yao ya hivi karibuni. Na hivyo “Mungu wa tumaini pia abariki sasa kutano huo.  “Kiukweli, sisi wote ni wanahija wa matumaini kama isemavyo kauli mbiu ya Mwaka Mtakatifu 2025. Tayari miaka mitatu iliyopita, wakati wajumbe wengine kutoka Shirikisho la Kilutheri Ulimwenguni walipokuja Roma,” Papa alisema kuwa walitafakari pamoja juu ya ukumbusho uliokaribisha Baraza la Kwanza la Nikea kama tukio la kiekumene. Na mwaka 2023 Papa amesema  katika hafla ya Mkutano Mkuu wa Shirikisho lao huko Krakow, Mchungaji Burghardt, pamoja na mpendwa Kardinali Kurt Koch, katika Tamko la pamoja lilisisitiza kwamba: “imani ya Kikristo ya zamani ya Nikea, ambayo tutaadhimisha Maadhimisho ya miaka 1700 katika 2025, inaunda kifungo cha kiekumene ambacho kina kitovu chake katika Kristo"(19 Septemba 2023).

 Katika muktadha huo, Wao walikumbuka kwa usahihi ishara nzuri ya matumaini, ambayo ina nafasi ya pekee katika historia ya upatanisho kati ya Wakatoliki na Walutheri. Kwa hakika, hata kabla ya mwisho wa Mtaguso wa Pili wa Vatican, Wakristo Wakatoliki na Walutheri wa Marekani, huko Baltimore, walitoa ushuhuda huu pamoja: “Imani ambayo Bwana wetu Yesu Kristo ni Mwana, Mungu kutoka kwa Mungu, inaendelea kutuhakikishia kwamba tumekombolewa kweli; kwa maana ni yeye tu aliye Mungu anayeweza kutukomboa” (The Status of the Nicene Creed as Dogma of the Church, 7 Julai 1965). Yesu Kristo ndiye moyo wa uekumene. Yeye ni huruma ya kimungu aliyefanyika mwili, na utume wetu wa kiekumene ni kumshuhudia. Baba Mtakatifu ameongeza kusema kuwa katika “Tamko la Pamoja la Mafundisho ya Kuhesabiwa Haki”, Walutheri na Wakatoliki walitunga lengo moja la “kumkiri Kristo katika mambo yote, ambaye ndiye pekee ambaye mtu anaweza kumweka imani yote ndani yake, kwa kuwa yeye ndiye mpatanishi pekee (rej. 1Tim 2:5-5 6) ambaye kupitia kwake Mungu katika Roho Mtakatifu hujitoa mwenyewe na kumimina karama zake ambazo hufanya upya kila kitu” (n. 18).”

Wakati wa kusali sala ya Baba Yetu na Wajumbe wa shirikisho la kilutheri
Wakati wa kusali sala ya Baba Yetu na Wajumbe wa shirikisho la kilutheri

Baba Mtakatifu Francisko kwa njia hiyo amesema  miaka 25 imepita tangu kusainiwa kwa Azimio hilo rasmi la pamoja. Kilichotokea mbamo tarehe 31Oktoba 1999 huko Augusta ni ishara nyingine ya matumaini katika historia yetu ya upatanisho. Kwa hiyo basi ni bora kuitunza  kwenye kumbukumbu zetu kama kitu kilicho hai kila wakati. “Miaka 25 iweze  kuadhimishwa katika Jumuiya zetu kama sherehe ya matumaini. Tukumbuke kwamba asili yetu ya kawaida ya kiroho ni “ubatizo mmoja kwa ondoleo la dhambi” (Imani ya Nicea-Constantinople) na tuendelee kwa ujasiri kama “mahujaji wa tumaini”. Mungu wa matumaini awe pamoja nasi na aendelee kusindikiza mazungumzo yetu ya ukweli na upendo kwa baraka zake.”

Baba Mtakatifu Francisko akiendelea ametazama Ioannis Zizioulas, ambaye alifariki mnamo 2023 kwamba katika safari hiyo ya uekumene, jambo zuri limekuja akilini mwake kuhusu Askofu mpendwa Zizioulas, Askofu huyo wa Kiorthodox, mwanzilishi wa uekumene, alisema kwamba alijua tarehe ya muungano wa Wakristo ambayo itakuwa  “siku ya hukumu ya mwisho!”  Lakini wakati huo huo, alisema, ni lazima tutembee pamoja, tusali pamoja na tutoe upendo pamoja, katika njia yetu kuelekea ile siku kuu ya  Umoja wa kiekumene  ambayo itakuwa hukumu ya mwisho. Alikuwa anasema hivyo Zizioulas kwa sababu alikuwa na roho ya utani. Papa Francisko amewashukuru tena kwa moyo ziara yao , na amewaalika kusali pamoja sala ya Baba Yetu , kila mtu kwa lugha yake.

Papa na shirikisho la kiluheri duniani
20 June 2024, 16:44