Tafuta

2024.06.03 Papa akutana na washiriki wa Mazungumzo kwa ajili ya Fedha fungamanishi na endelevu. 2024.06.03 Papa akutana na washiriki wa Mazungumzo kwa ajili ya Fedha fungamanishi na endelevu.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa Francisko:Pesa lazima zitumike kuhudumia na sio kutawala!

Papa amekutana na wanachama wa Taasisi ya Centesimus Annus na wale wanaoshiriki katika mazungumzo ambayo yamekuza kwa ushirikiano na Mpango wa “Prospera-Progetto Speranza.Amebainisha alivyosoma kwa shauku matokeo ya kazi waliyofanya katika miaka hii miwili,kuanza mazungumzo kati ya fedha,ubinadamu na dini:si rahisi.Wamechagua kuanzisha Majadiliano haya na wawakilishi wa mfumo wa kifedha wa Italia.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 3 Juni 2024 amekutana mjini Vatican na kusalimiana na Rais, wanachama wa Taasisi ya Centesimus Annus na wale wanaoshiriki katika Mkutano wa Mazungumzo ambayo yamekuzwa kwa ushirikiano na Prospera-Progetto Speranza, ukiongozwa na mada:  “ Mazungumzo ya Fedha Endelevu Kabisa,” liohamasisha na Mfuko wa  Centesimus Annus Pro Pontifice.  Papa amebainisha alivyosoma kwa shauku matokeo ya kazi waliyofanya katika miaka hii miwili, kuanza mazungumzo kati ya fedha, ubinadamu na dini: si rahisi. Wamechagua kuanzisha “Majadiliano” haya na wawakilishi wa mfumo wa kifedha wa Italia. Mwanauchumi aliwahi kuniambia: mazungumzo kati ya uchumi na falsafa, dini na ubinadamu yanawezekana. Mazungumzo kati ya fedha, taalimungu na ubinadamu, hata hivyo, ni magumu sana. Hii ni ya kushangaza! Baba Mtakatifu aidha katika hotuba hiyo amesema “Mfumo huu wa kifedha wa Italia una historia ya kale nyuma yake, ambayo, kwa mfano, “Monti di Pietà” walikuwa na kichocheo kikubwa cha kuwasaidia maskini zaidi bila kuangukia katika mantiki ya ustawi, na mikopo iliyopendekezwa ili kuruhusu watu kuwa na uwezo wa kufanya kazi na, kupitia shughuli ya mtu mwenyewe, kugundua tena utu sahihi.

Papa amekutana na wajumbe wa Centesmus Anus
Papa amekutana na wajumbe wa Centesmus Anus

Kiukweli amesema Papa “kuwasaidia maskini kwa pesa lazima iwe dawa ya muda ya kukabiliana na dharura. Kusudi la kweli linapaswa kuwa kuwaruhusu maisha yenye heshima kupitia kazi (Laudato si', 128).” Papa amebainisha alivyo vutiwa pia na lengo kuu ambalo wamejiwekea, ambalo ni kufikiria pamoja na viongozi wakuu wa ulimwengu wa fedha juu ya uwezekano kwamba dhamira ya kufanya vizuri na ya kutenda mema inaweza kwenda pamoja. Kwa maneno mengine, wamejipa kazi nzuri: kuchanganya ufanisi na uendelevu kamili, ujumuishaji na maadili. Wanasema kwa hakika kwamba imani yao ni kwamba mafundisho ya kijamii ya Kanisa yanaweza kuwakilisha dira. Ili hili lifanyike kiukweli, ni muhimu si kuacha wakati wa kuhimiza, lakini kuwa na uwezo wa kuangalia utendaji wa fedha, kushutumu vipengele dhaifu na kufikiria hatua madhubuti za kurekebisha.

Papa amependa kutoa mfano. Katika kile kinachoitwa siglo de oro -katika  karne ya 16 - biashara ya pamba nchini Hispania ilikuwa soko lililokuwa na maendeleo ambalo lilihamisha mtaji mkubwa wa kiuchumi. Wataalimungu wa Kihispania wa wakati huo walianza kujadili aina hiyo ya biashara na kutoa tathmini za kimaadili ambazo zilibadilika na mabadiliko katika muktadha wa kihistoria. Kwa hakika, vita vya Flanders vilimaanisha kwamba wale waliofanya kazi moja kwa moja katika kuzalisha na kukata manyoya hawakupata tena malipo ya kutosha kwa ajili ya kazi yao, na hivyo wakashutumu mfumo huo wa kifedha, wakionesha udhaifu wake na kuomba uadilifu mkubwa zaidi. Wataalimungu wa Kihispania waliweza kuingilia kati kwa sababu walijua mchakato huo wa kazi, na kwa hiyo hawakujiwekea kikomo kwa kusema: ”Lazima tutafute manufaa ya wote”, lakini walielezea kile ambacho kilikuwa kibaya na kuomba hatua sahihi za mabadiliko kwa manufaa ya wote; bila shaka.

Papa amekutana na wajumbe wa Centesmus Annus
Papa amekutana na wajumbe wa Centesmus Annus

Papa amesema kwamba, wao wanajua taratibu za kifedha, na hii ni mali yao kubwa, lakini wakati huo huo pia ni wajibu mkubwa. Ni juu yao kuelewa jinsi ya kuhakikisha kuwa ukosefu wa usawa unapungua. Papa amerudia kukazia kuwa “Narudia, kwamba ukosefu wa usawa unapungua.” Kwa sababu “marekebisho ya kifedha ambayo hayapuuzi maadili yangehitaji mabadiliko makubwa ya mtazamo kwa upande wa viongozi wa kisiasa [...]. Pesa lazima zitumike na sio kutawala!” (EG 58). Papa akiendelea alibainisha jinsi ambavyo aliwahi kumsikia mkosoaji wa kisiasa akisema: “Katika nchi hii tunatawala kutoka mifukoni mwetu:” Kwa kuongeza Papa amesema “hii ni mbaya! Kwa hiyo wao wamefanya kazi katika viwango vitatu: mawazo, uthabiti na ushujaa wa mema. Papa anakubali kwamba ni lazima kamwe kutopoteza mtazamo wa uthabiti, kwa sababu hatarini ni hatima ya maskini zaidi, ya watu wanaojitahidi kutafuta njia za maisha yenye heshima.

Kazi waliyofanya huko Milano ni ya kutia moyo, na pengine inaweza kuwa wazo zuri kuieneza kwa vituo vingine vya kifedha pia, kutangaza mfano wa mazungumzo ambayo hueneza na kuleta mabadiliko ya dhana. Kiukweli, dhana ya kiteknolojia inabakia kutawala; kuna hitaji la utamaduni mpya, wenye uwezo wa kutoa nafasi kwa maadili thabiti vya kutosha, kwa utamaduni na hali ya kiroho (Laudato si', 105). Papa amewashukuru kwa kazi waliyofanya. Ameshukuru Wanachama wa Mguko wa Centesimus Annus kwa mpango wao! Amewahimiza kuendelea na kueneza njia na mtindo huu. Mazungumzo ni njia bora kila wakati, hata kuboresha nyumba yetu ya kawaida. Amewabariki na kukuomba tafadhali wamwombee.

Papa amekutana na wanachama wa Mfuko wa Centesmus Annus
03 June 2024, 12:33