Ujumbe wa Papa wa Siku 110 ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani 2024
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mungu anatembea na watu wake ndiyo Kauli mbiu inayoongoza Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa Siku ya 110 ya Wahamiaji na Wakimbizi duniani itakayoadhimisha tarehe 29 Septemba 2024. Baba Mtakatifu katika ujumbe huo anabainisha kuwa mnamo tarehe 29 Oktoba 2023 ilihitimishwa Sehemu ya Kwanza ya Mkutano Mkuu wa XVI wa Sinodi ya Maaskofu, ambayo ilituruhusu kujikita kwa kina katika Sinodi ya kina kama wito asili wa Kanisa. “Sinodi inajiwakilisha kimsingi kama safari ya pamoja Watu wa Mungu na kama mazungumzo yenye matunda ya karama nyingi na huduma katika huduma ya matukio ya Ufalme(kutoka katika utangulizi wa Mhutasari).
Mkazo uliowekwa juu ya ukuu wa sinodi unaruhusu Kanisa kugundua upya asili yake ya kwenda, ya watu wa Mungu katika mwendo kwenye historia, ya hija tunaweza kusema kukumbia kuelekea Ufalme wa Mbingu (Lg,49). Hii inakuja tu kuhusu simulizi ya kibiblia ya kitabu cha Kutoka, ambayo inawakilisha Watu wa Israeli katika safari kuelekea nchi ya ahadi: safari ndefu ya utume kuelekea uhuru ambao unajieleza na ule wa Kanisa kuelekea mkutano wa mwisho na Bwana. Kwa namna hiyo inawezekana kuona katika wahamaiaji wakati wetu, kama ilivyokuwa ya kila kipinidi na sura hai ya watu wa Mungu katika safari kuelekea kwao. Safari zao za matumaini zinatukumbusha kuwa “uraia wetu kwa dhati huko mbinguni na hapo tunasubiri kama Mwokozi Bwana Yesu Kristo (Fil 3,20).
Picha mbili, ile ya kutoka katika Biblia na ile ya wahamiaji zinawakilisha kuwasilisha mambo kadhaa yanayofanana. Kama ilivyokuwa watu wa Israeli wa wakati wa Musa, wahamiaji mara nyingi wana kimbia hali za kukandamizwa na kunyanyaswa, ukosefu wa usalama, ubaguzi, ukosefu wa matarajio ya maendeleo. Kama wayahudi katika jangwa, wahamiaji wanakutana na vizingiti vingi katika safari yao: wamejaribiwa na kiu na njaa; wamechoka na uchovu na ugonjwa; wanajaribiwa kwa kukata tamaa. Lakini hali halisi msingi ya kutoka, kila kutoka, ni kwamba Mungu anatangulia na anasindikiza safari ya watu wake na watoto wake wote wa kila wakati na mahali.
Uwepo wa Mungu katikati ya watu ni uhakika wa historia ya wokovu: “Bwana , Mungu wako, yuko nawe; hatakuacha(Dt 31,6). Kwa watu waliotoka Misri uwepo huo unajionesha katika mitindo tofauti: ndani wingu mfano wa moto unaelekeza na kuangaza njia (Kut 13,21); Na hema la kukutania ambalo lilikuwa likitunza sanduku la agano, lilifanya ukaribu wa Mungu uonekane (rej.Kut 33,7). Na nyoka ya shaba inahakikisha ulinzi wa kimungu(Hes 21, 8-9) na mkate na maji (Kut 16-17) ni zawadi za Mungu wa watu walio na njaa na kiu. Hema ni mtindo wa uwepo kwa namna pendwa ya Bwana. Wakati wa ufalme wa Daudi, Mungu alikataa kufungwa katika hekalu ili kuendelea kukaa katika hema na hivyo kuweza kutembea na watu wake, “kutoka hema moja hadi nyingine na kutoka kao moja hadi lingine (1Cr 17,5). Wahamiaji wengi wanafanya uozefu wa Mungu msindikizaji wa safari, kiongozi na tena mwokozi. Kwake yeye wanajikabidhi kabla ya kuanza safari na kwake wanamkimbilia katika haki za mahitaji. Kwake yeye wanatafuta faraja wakati wa kukata tamaa. Shukrani Kwake, kuna wasamaria wema katika njia ndefu.
Kwake Yeye, katika sala, wanamkabidhi matumaini yao. Ni Biblia ngapi, Injili, vitabu vya sala na rosari vinawasindikiza wahamiaji katika safari zao ili kukatisha majangwa, mito, mabahari na mipaka ya kila bara! Mungu hatembei na watu tu, bali hata na watu wake, kwa maana ya kwamba anajitambulisha na wanaume na wanawake walioko katika safari kupitia historia, kwa namna ya pekee na walio wa mwisho, maskini, walio pembezoni, kana kwamba kuendeleza fumbo la Umwilisho. Kwa njia hiyo kukutana na mhamiaji, kama kwa kila kaka na dada ambaye anahitaji ni kukutana na Kristo. Alitwambia Yeye mwenyewe. Ni Yeye anayebisha hodi katika mlango wetu na njaa, kiu, mgeni, uchi, mgonjwa, mfungwa, akiomba kukutana naye na kusaidiwa (Mahubiri misa washiriki wa Mkutano wa “Liberi dalla Paura,” Sacrofano 15 Februari 2019).
Hukumu ya mwisho kama ilivyosimuliwa na Matayo sura ya 25 katika Injili yake haiachi shaka:“Nilikuwa mgeni na mkanikaribisha(Mt 25,25) na tena "amini nawambia: kila lolote mlilofanya kwa mmoja wa ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi (Mt 25,40)." Kwa hiyo kila mkutano, katika safari ndefu, inawakilisha fursa ya kukutana na Bwana; na ni fursa iliyojaa wokovu, kwa sababu katika dada au katika kaka mwenye kuhitaji msaada wetu yumo Yesu. Kwa maana hiyo, maskini wanatuokoa, kwa sababu wanaturuhusu kukutana na uso wa Bwana(Ujumbe wa Siku ya III ya Maskini 17 Novemba 2019). Katika Siku hii iliyojikita kwa wahamiaji na wakimbizi Baba Mtakatifu anabainisha kuwa tuungane katika sala kwa ajili ya wote ambao wamelazimika kuacha nchi zao katika kutafuta hali ya maisha yenye hadhi. Tuhisi katika safari pamoja na wao, tufanye sinodi pamoja na kuwakabidhi wote kama ilivyo Mkutano wa sinodi ijayo, “kwa maombezi ya Bikira Maria ishara ya uhakika wa tumaini na faraja katika safari ya Watu, waaminifu wa Mungu (Relazione di Sintesi, Per proseguire il cammino).
Ujumbe huo unahitimishwa kwa sala ambayo Baba Mtakatifu anasali hivi: Mungu, Baba Mwenyezi, sisi ni Kanisa lako la mahujaji, njiani kuelekea Ufalme wa Mbinguni. Kila mmoja wetu aishi katika nchi yake, lakini kana kwamba sisi ni wageni. lakini kila nchi ni nchi ya kigeni kwetu. Tunaishi duniani, lakini tuna uraia wetu mbinguni. Usituache tuwe mabwana wa sehemu hiyo ya dunia uliyotupatia kama makazi ya muda. Utusaidie tusiache kamwe kutembea, pamoja na kaka na dada zetu wahamiaji, kuelekea makazi ya milele ambayo umetuandalia. Fungua macho yetu na mioyo yetu ili kila kukutana na wenye shida, tugeuke kukutana na Yesu, Mwanao na Bwana wetu. Amina.