2024.06.19 Katekesi ya Papa Francisko 2024.06.19 Katekesi ya Papa Francisko  (Vatican Media)

Papa Francisko:Wakimbizi wakaribishwe,wasindikizwe na kujumuishwa

Siku ya Kimataifa ya wakimbizi iwe ni fursa ya kuelekeza macho na usikivu wa kidugu kwa wale wote wanaolazimika kuyahama makazi yao kutafuta amani na usalama.”Amesema hayo Papa Francisko, mara baada ya Katekesi yake katika fursa ya kuelekea kilele cha Siku hiyo inayoadhimishwa kila ifikapo Juni 20 ya kila mwaka.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika salamu mbali mbali baada ya katekesi, akizungumza na waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, kwa, Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 19 Juni 2024, Papa alikumbusha Siku ya Wakimbizi Duniani, ifanyikayo kila tarehe 20 Juni ya kila mwaka “iliyotangazwa na Umoja wa Mataifa. Papa amesema “Iwe ni fursa ya kuelekeza macho ya usikivu na ya kidugu kwa wale wote wanaolazimika kuyahama makazi yao kutafuta amani na usalama. Sote tumeitwa kuwakaribisha, kuwahamasisha, kuwasindikiza na kuwaunganisha wale wanaobisha hodi kwenye milango yetu.” Papa kwa hiyo ameongeza kusema:” Ninaomba kwamba Mataifa yafanye kazi ili kuhakikisha hali ya kibinadamu kwa wakimbizi na kuwezesha michakato ya ujumuishaji.”

Papa Francisko amewakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza lugha ya Kiitaliano, kwa namna ya pekee, Papa: Chama cha Marafiki wa Kardinali Celso Costantini, wakisindikizwa na Askofu Giuseppe Pellegrini wa Jimbo la Concordia-Pordenone, katika kuadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Concilium Sinense ya Shanghai. “Na hii pia inanifanya nifikirie watu wapendwa wa China. Daima tuwaombee watu hawa watukufu na wajasiri, ambao wana utamaduni mzuri kama huu. Tuwaombee Wachina.”Papa amesisitiza

“Nina furaha kuwakaribisha wanachama wa Muungano wa Vipofu na wenye Ulemavu wa Macho wa Roma, wanachama wa Shirikisho la Wanawake, Sanaa, Taaluma, Biashara wa Sicilia, wanachama wa Ushirika wa Mshikamano wa Binetto (Bari), - hawa Wanapuglia wana nguvu, eh! , Papa ameongeza “ na waamini wa Shirika la Kidunia la Watumishi wa Maria wanaoadhimisha miaka mia moja ya kupitishwa kwa Kanuni ya Shirika lao na kutembelea makaburi ya Mitume kuamshe ari mpya ya kiroho katika moyo wa kila mtu.”

Hatimaye, mawazo ya Papa yamewaendea wagonjwa, wazee, wenye ndoa wapya na  hasa vijana.  Papa Francisko aidha amekubusha siku kuu ya Mwanzislihsi wa Shirika lake inayoandimishawa kila tarehe 21 Juni yak ila mwaka na kusema kuwa “Keshokutwa tutaadhimisha kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Luigi Gonzaga, ambaye alipenda maisha na kwa hiyo akayatumia kabisa kwa ajili ya maadili makuu ya Kikristo; awasaidie kugundua tena wito wa utakatifu katika mchango wa ukarimu na kwa ndugu zenu.” Papa Francisko ameomba kuendelea kuombea amani. “Vita daima ni kushindwa tangu mwanzo. Tunasali kwa ajili ya amani katika Ukraine inayoteswa, katika Nchi Takatifu, katika Sudan, Myanmar na popote watu wanapoteseka kutokana na vita. Tuombe amani kila siku.” Na hatimaye kwao wote amewapatia baraka.

Papa atoa wito katika fursa ya kilele cha Siku ya Wakimbizi Duninia
19 June 2024, 15:08