Tafuta

2024.06.13 Papa akutana na washiriki wa Mkutano wa mwaka wasimamizi wa vyama vya waamini,harakati za kikanisa na jumuiya mpya. 2024.06.13 Papa akutana na washiriki wa Mkutano wa mwaka wasimamizi wa vyama vya waamini,harakati za kikanisa na jumuiya mpya.  (Vatican Media)

Papa:kufikiri kama Mungu,kushinda aina ya kufungwa na kukuza unyenyekevu!

Shauku ya Papa ni kwamba baada ya Sinodi mchakato wa kisinodi ubaki kuwa namna ya kutenda ya kudumu ya Kanisa,kwa ngazi zote,ili kuingia katika moyo wa wote,wachungaji na waamini,hadi kugeuka “mtindo wa kikanisa”shirikishi.Amesema hayo akikitana na washiriki wa Mkutano wa mwaka wasimamizi wa vyama vya waamini,harakati za kikanisa na Jumuiya mpya.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi tarehe 13 Juni 2024 amekutana na washiriki wa mkutano wa mwaka wasimamizi wa vyama vya waamini, harakati za kikanisa na jumuiya mpya zinazohamasishwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha. Akianza hotuba yake amefurahishwa kukutana nao katika fursa ya kutafakari juu yao, na kuhusu sinodi, ambayo walichagua kama tema ya kuongoza mkutano wao. Mara kadhaa, amesema amerudia kuwa “safari ya sinodi inahitaji uongofu wa kiroho kwa sababu bila mabadiliko ya ndani, haiwezekani kufikia matokeo ya kudumu.” Shauku ya Baba Mtakatifu kwa hiyo “kiukweli ni kwamba baada ya Sinodi hiyo, yaani mchakato wa kisinodi ubaki kuwa namna ya kudumu ya  kutenda kwa Kanisa, kwa ngazi zote, kwa kuingia katika moyo wa wote, yaani wachungaji na waamini, hadi kugeuka kuwa “mtindo fungamani wa kikanisa.” Haya yote, hata hivyo, yanahitaji mabadiliko ambayo lazima yafanyike kwa kila mmoja wetu, “uongofu” halisi.

Papa na washiriki wa Mkutano wa mwaka wasimamizi wa vyama vya waamini, harakati za  kikanisa na jumuiya mpya
Papa na washiriki wa Mkutano wa mwaka wasimamizi wa vyama vya waamini, harakati za kikanisa na jumuiya mpya

Imekuwa njia ndefu; kufikiria ile ya kwanza ambayo ilionesha kwamba sinodi inahitajika katika Kanisa la Kilatini na ambaye ni Mtakatifu Paulo VI, ambapo baada ya Baraza aliunda Sekretarieti ya Sinodi ya Maaskofu. Kanisa la Mashariki limehifadhi sinodi; badala yake Kanisa la Kilatini lilikuwa limeipoteza. Ni Mtakatifu Paulo VI aliyefungua hii. Na leo, karibu miaka 60, tunaweza kusema kwamba sinodi imeingia katika njia ya utendaji ya Kanisa. Suala la zaidi kuhusu Sinodi hii si kama inashughulikia tatizo hili au lile jingine, Hapana! Jambo muhimu zaidi ni nia ya parokia, ya jimbo... Ni ya ulimwengu mzima katika sinodi. Na kutoka katika mtazamo wa uwongofu huu wa kiroho, Papa Francisko alipenda kuonesha baadhi ya mitazamo, ya “fadhila za sinodi”, ambazo tunaweza kuzipata kutoka katika matangazo matatu ya Mateso katika Injili ya Marko (taz 8:31; 9:31; 10:32-34): kufikiri kulingana na Mungu, kushinda kila aina ya kufungwa na kukuza unyenyekevu.”

Papa na washiriki wa Mkutano ulioandaliwa  na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na maisha
Papa na washiriki wa Mkutano ulioandaliwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na maisha

 Papa akianza  kudadavua ya Kwanza ya  kufikiri kulingana na Mungu amesema: “baada ya tangazo la kwanza la Mateso, Mwinjili anatuambia kwamba Petro alimkemea Yesu. Yeye mwenyewe, ambaye alipaswa kuwa kielelezo na kuwasaidia wanafunzi wengine kuwa kikamilifu katika utumishi wa kazi ya Mwalimu, alipinga mipango ya Mungu, akikataa mateso na kifo chake. Naye Yesu alimwambia: “Wewe hufikirii sawasawa na Mungu, bali kulingana na wanadamu” (Mk 8,32). Hapa kuna badiliko kuu la kwanza la ndani ambalo tunaombwa kwetu: kuhama kutoka katika "wazo la mwanadamu pekee hadi mawazo ya Mungu.” Katika Kanisa, kabla ya kufanya kila uamuzi, kabla ya kuanza kila programu, kila utume, kila misheni, tunapaswa kujiuliza kila wakati: Mungu anataka nini kutoka kwangu, Mungu anataka nini kutoka kwetu, katika wakati huu, katika hali hii? Je, kile ninachofikiria, kile ambacho sisi kama kikundi tunachofikiria, kweli ni mawazo ya Mungu?

Papa wakati wa hotuba yake
Papa wakati wa hotuba yake

Tukumbuke kuwa mhusika mkuu wa njia ya sinodi ni Roho Mtakatifu, sio sisi: Yeye pekee ndiye anayetufundisha kusikiliza sauti ya Mungu, kibinafsi na pia kama Kanisa. Mungu daima ni mkubwa kuliko mawazo yetu, yeye ni mkubwa kuliko mawazo makuu, mitindo ya kikanisa ya wakati huu, hata karama ya kikundi au harakati zetu. Kwa hiyo, tusijichukulie kuwa sisi ni katika umoja na Mungu, hapana: badala yake, kila mara tunajaribu kujiinua ili kubadili mawazo kulingana na Mungu na si kulingana na wanadamu. Hii ni changamoto kubwa ya kwanza. Kufikiri kama Mungu. Papa amerudia kusema kwamba: “Tufikirie sehemu ya Injili wakati Bwana anatangaza Mateso, na Petro anapinga. Je alimwambia nini Bwana: wewe hauko pamoja na Mungu, wewe hufikiri kwa mujibu wa Mungu.

 Papa na washiriki wa Mkutano wa mwaka wasimamizi wa vyama vya waamini, harakati za  kikanisa na jumuiya mpya
Papa na washiriki wa Mkutano wa mwaka wasimamizi wa vyama vya waamini, harakati za kikanisa na jumuiya mpya

Pili: kushinda kila kufungwa. Baada ya tangazo la pili la Mateso, Yohane anapinga mtu ambaye alitoa pepo kwa jina la Yesu, lakini hakuwa anatoka katika kundi la wanafunzi na akasema: “Tulitaka kumzuia - kwa sababu hakutufuata!” (Mk 9:38).Yesu hakubaliani na mtazamo wake na alimwambia: “Yeyote asiye kinyume chetu yuko upande wetu” (Mk 9,40); kisha aliwaalika Mitume wote kujichunga wenyewe badala yake, ili isiwe tukio la kashfa kwa wengine (taz. Mk 9,42-50). Papa kwa njia hiyo alitoa onyo kuwa: “Tafadhali kuwa waangalifu na majaribu ya “Mduara uliofungwa.” Wale Kumi na Wawili walikuwa wamechaguliwa kuwa msingi wa watu wapya wa Mungu, walio wazi kwa mataifa yote ya dunia, lakini Mitume hawakufahamu upeo huu mkuu walijikunja na wakaonekana kutaka kutetea zawadi walizopokea kutoka kwa Bwana za  kuponya wagonjwa, kutoa pepo, kutangaza Ufalme (taz Mk 2:14) - kana kwamba ni mapendeleo.

Na hii ni changamoto kwetu pia: kutokwenda zaidi ya kile cha “mduara” wetu unafikiri, kushawishika kwamba tunachofanya ni kizuri kwa kila mtu, kutetea, labda bila kutambua, nafasi, haki au heshima “ya kikundi.” Au kuruhusu uzuiliwe na hofu ya kupoteza hisia yako ya kuwa mali na utambulisho wako, kwa sababu ya ukweli wa kufungua watu wengine na njia zingine za kufikiria, bila kutambua utofauti kama fursa, na sio tishio. Hivi ndivyo “vizio” ambavyo sote tunahatarisha kubaki wafungwa.” Papa Francisko  aidha ametoa onyo tena  kuwa makini na kujitenga na makundi binafsi, tasaufi binafsi kwamba “ni uhalisia wa kusaidia kutembea na Watu wa Mungu, lakini si marupurupu, kwa sababu kuna hatari ya kuishia kufungwa katika nyua hizi”. Sinodi inatutaka badala ya kutazama ng’ambo ya ua kwa ukuu wa nafsi, tuone uwepo wa Mungu na matendo yake hata kwa watu tusiowajua, kwa mbinu mpya za kichungaji, katika maeneo ya utume ambayo hatukuwahi kushiriki hapo awali; anatuomba tujiachie tupigwe, hata “tuumizwe” na sauti, uzoefu na mateso ya wengine: ya ndugu zetu katika imani na watu wote walio karibu nasi. Kufungua moyo wazi.

Papa na Jumuiya mpya za kikanisa na Harakati za Kanisa
Papa na Jumuiya mpya za kikanisa na Harakati za Kanisa

Hatimaye, jambo la  tatu ni kukuza  unyenyekevu. Baada ya tangazo la tatu la mateso, Yakobo na Yohane waliomba nafasi za heshima karibu na Yesu, ambaye badala yake alijibu kwa kuwaalika kila mtu kuzingatia ukuu wa kweli sio kutumikiwa, lakini kutumikia, kuwa mtumishi wa wote, kwa sababu yeye mwenyewe alikuja kufanya hivyo. (rej.Mk 10,44-45). Papa Francisko amesisitiza kuwa “Tunatambua hapo kwamba uongofu wa kiroho lazima uanzie na unyenyekevu, ambao ni mlango wa kuingia fadhila zote. Katika hilo Papa ameeleza masikitiko yake kuwa huwa anasitikita anapokutana na wakristo wanaojidai, kwamba “ kwa sababu mimi ni kuhani kutoka hapa, au kwa sababu mimi ni mlei kutoka  huko, kwa sababu ninatoka kwenye taasisi hii… Hili ni jambo baya. Unyenyekevu ni mlango, ni mwanzo.” Na hii pia inatusukuma kujiuliza: je, ninatafuta nini hasa katika mahusiano na ndugu zangu katika imani? Kwa nini ninatekeleza mipango fulani katika Kanisa? Na ikiwa tunatambua kwamba kwa namna fulani kiburi kidogo au majivuno yameingia ndani yetu, basi tunaomba neema ya kurudi kwenye uongofu kwenye unyenyekevu. Ni wanyenyekevu tu, kiukweli, hutimiza mambo makuu katika Kanisa, kwa sababu wale walio wanyenyekevu wana misingi imara, iliyojengwa juu ya upendo wa Mungu, ambao haushindwi kamwe, na kwa hiyo hautafuti kutambuliwa kwingine.

Na hatua hii ya uongofu wa kiroho pia ni ya msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa la kisinodi: mtu mnyenyekevu tu ndiye anayethamini wengine, na anakaribisha mchango wao, ushauri, utajiri wa ndani, bila kuleta umimi bali  wa sisi na ya Jumuiya. Papa kwa hilo ameongeza kusema kuwa: “Ninaumia tunapokutana Wakristo - kwa lugha ya Kihispania tunasema Yo me mí conmigo para mí, yaani, “Mimi, pamoja nami, kwa ajili yangu, daima kwa ajili yangu.” Lakini Papa ameongeza: “Wakristo hawa wako katikati, hapana? Inasikitisha”? Ni mtu mnyenyekevu anayetetea ushirika katika Kanisa, akiepuka migawanyiko, kushinda mivutano, anajua jinsi ya kuweka kando mipango yake mwenyewe ya kuchangia mipango ya pamoja, na hii ni kwa sababu anapata furaha katika kutumikia na sio kufadhaika au kinyongo.  Kuishi sinodi, katika kila ngazi, ni kweli haiwezekani bila unyenyekevu.

Kadhalika Baba Mtakatifu akiendelea pia amesema: “Na ninataka kusema kwa mara nyingine tena, kusisitiza jukumu na harakati za kikanisa katika hili. Harakati za kanisa ni kwa ajili ya huduma, si kwa ajili yetu wenyewe. Inasikitisha unapohisi kwamba mimi ni wa hii, ya nyingine, kana kwamba ni kitu bora zaidi. Harakati za kikanisa zinapaswa kutumikia Kanisa, sio ujumbe wenyewe, bali kiini cha kikanisa. Inakuwa ni Mimi kwa ajili ya kuwahudumia.”  Kwa njia hiyo Papa Francisko amewatakia kwamba mawazo haya yawe na manufaa kwao katika safari yao, katika vyama na harakati zao, katika mahusiano yao na Wachungaji na kwa uhalisia wote wa kikanisa; na nimatumaini kwamba mkutano huo na nyakati zingine zinazofanana na hizo zitawasaidia kuboresha karama zao kutoka katika mtazamo wa kikanisa, wa kutoa mchango wao wa ukarimu na wa thamani katika uinjilishaji. Na ndiyo ambayo sisi sote tumeitwa, lakini kila wakati kuwa makini kwa kujiuliza: je, mimi ni mfuasi wa harakati ya kikanisa, ni wa chama au ni wa Kanisa? Ni katika harakati zangu, katika ushirika wangu kwa Kanisa, kama hatua ya kusaidia Kanisa, lakini harakati zilizofungwa lazima zifutwe, sio za kikanisa. Amewabariki, akiwatakia waendelee mbele na wasali kwa ajili yake. Walisali salamu Maria na hatimaye kuwabariki.

Papa na harakati za Kanisa
13 June 2024, 14:51