Papa:kusoma na kutafakari mahubiri ya Padre Tantardini ni vizuri kwa roho zetu
Papa Francisko
Kitabu hiki kinakusanya mahubiri ya Padre Giacomo Tantardini, kuhani wa asili ya Lombardia ambaye alitekeleza utume wake kwa shauku kuu karibu kabisa katika Mji wa Milele. Kwa miaka mingi mahubiri yake yamewalisha kiroho maelfu ya vijana na wazee waliojazana kwenye Basilika ya Mtakatifu Lorenzo Nje ya Ukuta, kila Jumamosi jioni. Hakuna aliyekengeushwa alipohubiri: kila neno lilibaki moyoni na kuakisi maisha. Ni katika kanisa hilo la kwanza la Kikristo, ambapo masalio ya shemasi Mtakatifu Lorenzo yanaheshimiwa, ndipo nilipokutana pia na Padre Giacomo. Kama vile tayari nilipata fursa ya kukumbuka katika Siku 30 za kila mwezi za kifo chake mnamo 2012, taswira ya mwisho niliyonayo juu yake ni “wakati wa sherehe ya kipaimara huko Mtakatifu Lorenzo Nje ya Ukutaa, akiwa amefunga mikono na macho wazi na mshangao, akitabasamu na umakini kwa wakati mmoja” (Rafiki yangu Padre Giacomo, Siku 30, n. 5, 2012).
Tayari alikuwa mgonjwa sana, tuliomba kwa ajili ya afya yake ... na alitushukuru kwa ishara ya matumaini ya kupona na, wakati huo huo, ya uaminifu. Uamuzi wa Familia yake wa kuchapisha maandishi(kutoka 2007 hadi 2012) sio tu kumbukumbu ya kuhani huyu, ambaye alikuwa mwana wa kiroho wa Padre Luigi Giussani. Kwa kusoma na kutafakari mahubiri yake kutakuwa na manufaa kwa roho zetu hata leo, kwa sababu yanatujulisha kiini cha asili cha maisha ya Kikristo. Daima kuna hitaji katika Kanisa ya kurejesha yaliyo muhimu. Kwa muda mrefu sana tumepunguza Ukristo kwa kanuni za sheria au jitihada za hiari, lakini kila maadili hatimaye hutuacha na hisia ya kushindwa na huzuni. Katika tafakari za Padre Giacomo, mhusika mkuu daima ni Neema, kwa sababu alikuwa anajua, baada ya uzoefu, kwamba mpango wa Mungu daima huzuia na kutarajia kila nia yetu, kuwasha tamaa ya mema kwa ajili yetu na kwa jirani, hasa zaidi katika shida.
Padre Giacomo daima alisindikizwa na neno “Neema” na neno lingine, ambalo linafanya kuwa halisi: “kivutio”, kwa sababu Bwana daima hutuvutia na changamsho la ubinadamu wake. Mojawapo ya matukio ya mara kwa mara ya kiinjili katika mahubiri ya Padre Giacomo ni kugeuzwa kwa Zakayo: “msaliti wa watu”, ambaye mabadiliko yasiyotarajiwa yalitokea kwa wakati, baada ya kuupanda mti kwa udadisi, alikutana na macho ya Yesu: “Zakayo alishuka mbio chini akijazwa na furaha... mwonekano huo ni tafakari safi ya kutazamwa; huu ndio mtazamo pekee ambao hauko hoi, huu ndio mtazamo pekee uliojaa furaha, huu ndio mtazamo pekee ambao mwanadamu hana, kwa sababu unatazamwa tu”(Mahubiri 3 Novemba 2007).
Hii ndiyo sababu sala inakuwa kipimo muhimu zaidi cha maisha. “Yeye aombaye ameokoka” ni kauli mbiu ya Mtakatifu Alphonsus Maria de' Liguori ambaye, haishangazi, Padre Giacomo alimpenda sana. Maombi sio kutoroka kwa ibada kutoka kwa ulimwengu mbaya. Ni kuuliza, kutoka ndani ya kina cha mtu mwenyewe, nini kinatoa maana na uwezekano wa furaha katika maisha. Ni kuomba kwamba Yeye Mwenyewe aje kuishi katika maisha yetu: “Kwa matumaini ya kusema: “Njoo”. Mtoto hana tumaini la bure kwa mama yake, mtoto anatumaini kuwa mama yake yuko karibu naye, kwa hivyo hata tumaini la Kikristo, tumaini la Kikristo linaoneshwa katika swali kwa kusema: "Njoo, njoo" (Mahubiri 1 Desemba 2007).
Ni lugha rahisi, ile ya Padre Giacomo, lakini katika kurasa hizi unaweza kuhisi msongamano wa usomaji wake, kutoka katika mawazo ya kitaalimungu ya Mtakatifu Augustino wake mpendwa hadi ile ya kishairi ya Charles Péguy, vile vile hadi njia ndogo ya Mtakatifu Teresa wa Mtoto Yesu: “Ninapokuwa mfadhili ni Yesu pekee anayetenda ndani yangu,” hii ni nukuu yake aliyopenda zaidi. Kuna mahubiri mengi yanayogusa moyo. Kinachogusa zaidi hakika ni cha mwisho, kilichoandikwa mnamo Jumamosi tarehe 31 Machi 2012 siku chache kabla ya kifo chake, ambacho kinaishia na sentensi rahisi, inayotamkwa kwa shida , tunasoma katika kitabu, kwa sauti dhaifu: “Inapendeza sana kujiruhusu kwenda mikononi mwa Mwana wa Mungu.” Maisha yake yote na mahubiri yalikuwa katika maneno hayo kumi yaliyotolewa kwa marafiki zake na kwetu sote.