2024.06.01 Papa Francisko amekutana na Wajumbe wa Chama cha Kikiristo cha Wafanyakazi nchini Italia(ACLI)katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican. 2024.06.01 Papa Francisko amekutana na Wajumbe wa Chama cha Kikiristo cha Wafanyakazi nchini Italia(ACLI)katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican.  (Vatican Media)

Papa kwa ACLI:Fungua milango,wakaribishe watu na kujenga mshikamano

Baba Mtakatifu Francisko akikutana na Vyama vya Kikiristo vya Wafanyakazi nchini Italia(ACLI)katika ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican amewaalika kuishi pamoja kwa amani kwani kunawezekana kila wakati,kwa kiwango cha kimataifa,maisha ya familia,jamii na sehemu za kazi.Katika jamii iliyogawanyika ya utamaduni wa kibinafsi inahitajika maeneo ya watu ili wafanye kazi na kupanga mipango kwa ajili ya manufaa ya wote.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, tarehe Mosi Juni 2024 alikutana na Vyama vya Wafanyakazi wa Kikristo wa Italia (ACLI) katika Ukumbi wa Paulo VI  mjini Vatican katika fursa ya  miaka themanini ya kuanzishwa kwao. Hawa walikuwa ni wawakilishi elfu sita , ambapo Papa amewakumbuka wale watu wote waliofanya kila wawezalo kwa ajili ya wafanyakazi, wastaafu, vijana, wageni na watu binafsi katika hali ya shida. Kwa njia hiyo kwenye hotuba yake amesema katika muktadha wa jamii iliyogawanyika na utamaduni wa mtu binafsi, tunahitaji mahali ambapo watu kwa pamoja wanakuza mipango kwa manufaa ya wote. Maeneo inapowezekana kukutana na watakatifu wa karibu, ambao hawaishii kwenye kurasa za mbele za magazeti, lakini wakati mwingine hubadilisha mambo kwa uzuri, shukrani kwa kujitolea na kujitolea katika huduma kwa jamii.

Papa amekutana na Wajumbe wa Vyama ha Kikatoliki vya wafanyakazi Italia
Papa amekutana na Wajumbe wa Vyama ha Kikatoliki vya wafanyakazi Italia

Baba Mtakatifu Francisko alisema uwepo muhimu wa  ACLI, katika jamii na ni sehemu yake muhimu ya kujitolea kwa amani, katika dunia hii iliyojazwa na vita vingi. ACLI iwe sauti ya utamaduni wa amani, nafasi ya kuthibitisha kwamba vita kamwe haviepukiki na wakati amani inawezekana daima; na kwamba hii inatumika katika mahusiano kati ya Mataifa na katika maisha ya familia, jumuiya na mahali pa kazi. Katika hotuba yake, Papa alielezea juu ya  mtindo ambao unapaswa kutofautisha ACLI, ambao lazima uwe maarufu, kama vile sinodi, demokrasia, amani ya Kikristo. Na mtindo maarufu unamaanisha kuwa karibu na watu, kuwa na kuhisi kuwa sehemu ya watu, kuishi na kushiriki furaha na changamoto za kila siku za jamii, kujifunza kutoka kwa maadili na hekima ya watu rahisi na inamaanisha kutambua kwamba mipango  mikubwa ya kijamii na mabadiliko ya kudumu yanatokea chini na kukutoka dhamira ya pamoja na ndoto za pamoja, kwa sababu asili ya kweli ya watu iko katika mshikamano na hisia ya kuhusika. Katika muktadha wa jamii ambayo imegawanyika tunajua hili  na utamaduni wa mtu binafsi, hitaji kubwa la mahali ambapo watu wanaweza kupata hisia hii ya kuwa mali ambayo ni ya ubunifu na yenye nguvu, hali ya ubunifu na dhabiti ya kuhusika ambayo husaidia kuhama kutoka umimi kwenda kwetu, kukuza mipango kwa faida ya wote pamoja na kutafuta njia za kuitambua. Wito wa vilabu vya Acli ni ule wa kufungua milango na kuiweka wazi, kuwakaribisha watu, kuwaruhusu kujenga vifungo vya mshikamano na hali ya kuhusishwa, kwa njia ambayo inaanza na  njia ya kuunganishwa pamoja ambayo inaongoza kwa utamaduni wa kukutana, alisema Baba Mtakatifu.

Salamu za Papa kwa washiriki wa Vyama vya Kikristo vya wafanyakazi Italia
Salamu za Papa kwa washiriki wa Vyama vya Kikristo vya wafanyakazi Italia

Hata hivyo akifafanua alisema kuhusu mtindo wa sinodi, ni ule wa kufanya kazi pamoja, kushirikiana kwa manufaa ya wote, hili ndilo linaloshuhudiwa na watu walio katika nyanja mbalimbali za kiutamaduni, kijamii, kisiasa na hata kikanisa wanaohusika na ACLI, ambao Baba Mtakatifu kwa hakika amewaalika kuchanganya pamoja na nguvu zingine za kijamii, kuunganisha na kukuza mipango ya pamoja na zaidi ya yote kuzingatia wadhaifu ili hasiwepo  anayeachwa nyuma. Aidha Baba Mtakatifu ameelezea mtindo wa kidemokrasia, uaminifu kwa demokrasia, ambao unahitajika sana leo hii , na ambap daima umekuwa kipengele tofauti cha vyama vyao(ACLI.) Kwa njia hiyo kidemokrasia ni ile jamii ambayo ndani yake kuna nafasi kwa kila mtu, katika hali halisi na sio tu katika matamko na kwenye karatasi. Hii ndiyo sababu kazi nyingi wanazofanya ni muhimu, hasa kusaidia wale walio katika hatari ya kutengwa: vijana, ambao mipango ya mafunzo ya kitaaluma inalenga hasa; wanawake, ambao mara nyingi wanaendelea kuteseka aina za ubaguzi na ukosefu wa usawa; wafanyakazi na wahamiaji dhaifu zaidi, ambao katika ACLI wanapata mtu mwenye uwezo wa kuwasaidia kupata heshima kwa haki zao; na hatimaye wazee na wastaafu, ambao kwa urahisi sana wanajikuta wametupwa na jamii. Na hii ni dhuluma. Kwa hiyo Papa Francisko alipendekeza kuwa sio kutoa msaada tu, bali kukuza hadhi ya wa kila mtu na kuhakikisha kila mtu anaweza kupeleka rasilimali na mchango wake.

Papa na wajume wa vyama vya Kikatoliki vya wafanyakazi Italia
Papa na wajume wa vyama vya Kikatoliki vya wafanyakazi Italia

Kuhusu mtindo wa amani, Baba Mtakatifu Francisko hata hivyo  alikumbusha  kwamba uwezo wa kuombea, yaani, kujiweka kati ya washindani, kuweka mkono juu ya bega la wote wawili na kukubali hatari ambayo inajumuisha kama  Kardinali Martini alivyo zungumza wakati wa mkutano wa mkesha wa maombi kwa ajili ya amani, na kubainisha maana ya kujitolea kwa amani. Wale wanaojua jinsi ya kuwa na msimamo wazi hujenga amani, lakini wakati huo huo hujitahidi kujenga madaraja, kusikiliza na kuelewa pande mbalimbali zinazohusika, kukuza mazungumzo na upatanisho. Kuombea amani ni jambo linaloenda mbali zaidi ya maelewano rahisi ya kisiasa, kwa sababu linahitaji kujihusisha na kuthubutu hatari. Baba Mtakatifu amesisitiza kuwa Ulimwengu wetu, tunajua, una alama ya migogoro na migawanyiko, na ushuhuda wao kama wapatanishi, kama waombezi wa amani, ni wa lazima na wa thamani zaidi kuliko hapo awali.

Papa akisali na kubariki sanamu aliyozawadiwa
Papa akisali na kubariki sanamu aliyozawadiwa

Hatimaye, Baba Mtakatifu amefafanua juu ya  mtindo wa Kikristo ambao  ni ule unaomtazama Mungu na kuongozwa na maisha ya Yesu, na  kwamba kuchukua mtindo wa Kikristo haimaanishi tu kutoa muda wa maombi katika mikutano lakini pia kukua katika ujuzi na Bwana na katika roho ya Injili, ili iweze kupenyeza kila kitu wanachofanya na matendo yetu yana mtindo wa Kristo na kumfanya awepo ulimwenguni. Mwaliko wa Baba Mtakatifu  Francisko kwa ACLI, mbele ya maono ya kiutamaduni ambayo yanahatarisha kufuta uzuri wa utu wa mwanadamu na kuisambaratisha jamii, ni kukuza ndoto hiyo mpya ya udugu na urafiki wa kijamii ambayo sio tu kwa maneno iliyotajwa  katika Waraka wa Baba Mtakatifu wa  Fratelli tutti.  Bali ni kwa vitendo vya ndoto ya Mtakatifu Francis wa Assisi na watakatifu wengine wengi, Wakristo na wamini wa imani zote.

Papa na ACLI
01 June 2024, 13:58