Papa kwa CEAMA na REPAM:mwaliko kwa njia mpya za Kanisa huko Ama
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kadinali Pedro Ricardo Barreto -wa Peru Rais wa Baraza la Kikanisa la Amazonia (CEAMA) katika mahojiano na Radio Vatican - Vatican News baada ya mkutano na Papa Jumatatu tarehe 3 Juni 2024 akiwa na wanachama wa CEAMA na Mtandaoa wa Kikani wa Amazoni (REPAM) alisema kuwa “Amazon inamtambua Papa Francisko kama 'babu'. Ndio wanamwita babu, na kwa watu wa Asilia, babu ni mtu mwenye busara, mtu anayeongoza, mtu ambaye hana nia nyingine zaidi ya kuwa na uwezo wa kutumikia na kutia moyo katika maisha.”
CEAMA ni tunda lililokomaa la Sinodi kwenye Amazon
Kwa mujibu wake alisema kuwa “Tulimpa Papa maendeleo ambayo tumefanya katika miaka ya hivi karibuni, baada ya Sinodi ya Kanda ya Amazonia iliyofanyika miaka mitano iliyopita, mnamo 2019. Na tumeona jinsi Mkutano wa Kanisa la Amazonia ulivyo tunda lililokomaa la mchakato huu wa sinodi ambayo imeendelezwa katika eneo lote.” Katika mkutano huo, washiriki waliweza kueleza kwa Papa wasiwasi wao juu ya mauaji ya watetezi wa mazingira na unyonyaji wa maliasili: “Uchimbaji haramu wa madini unafanya hali kuwa mbaya zaidi, kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.”
Mfano wa sinodi uwe wa Kanisa la Ulimwengu
Rais wa CEAMA alisema kwamba Papa Francisko aliwashukuru kwa kazi ambayo Kanisa linafanya katika mazingira yote muhimu ya Amazonia na aliwaeleza waendeleea kufanya kazi pamoja, wakitolea wenyewe ili uzoefu wa sinodi katika Amazoni uwe uzoefu wa mfano wa kile a,acho maisha yanayoweza kuwa katika Kanisa la ulimwengu wote.
Jubilei ya 2025 pia inahusishwa na hali ya kiroho ya sinodi
Wote kwa pamoja, wanaume na wanawake waliobatizwa ni sehemu ya watu wa Mungu walio katika hija katika historia pamoja na faraja na mahangaiko ya Mungu, lakini pia kwa huzuni na machozi ya ndugu wengi,” alisisitiza Kardinali akitazama mustakabali wa kazi ya kimisionari na sinodi katika Amazonia. Na akitazama Jubilei ya 2025, Kardinali Barreto alifafanua kwamba “Jubilei ya matumaini pia ina uhusiano wa karibu na hali hii ya kiroho ya sinodi. Tayari kuna dalili za mwanzo za shauku hii ambayo inageuka kuwa tumaini. Lakini matumaini yanatafsiriwa kuwa vitendo, katika vitendo vya kawaida.”
Uwasilishaji wa FAO wa shughuli za Sinodi ya Pan-Amazon
Jumanne tarehe 4 Juni, katika Kituo cha Sheikh Zayed cha makao makuu ya FAO mjini Roma, kumekuwa na mawasilisho ya Mijadala ya Baraza Maalum la Sinodi ya Maaskofu wa Kanda ya Amazonian, yenye mada “Njia mpya za Kanisa na kwa 'ikolojia fungamani'. Na siku ya Ijumaa tarehe 7 Juni 2024 Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana kitaandaa Kongamano la njia ya Sinodi ya Kanisa la Amazonia linalohamasishwa na REPAM na CEAMA.